Rutheni
Rutheni ni elementi na metali haba sana duniani. Kikemia ni elementi ya mpito yenye kifupi cha Ru na namba atomia 44 katika mfumo radidia.
Rutheni (Ruthenium) | |
---|---|
Lulu ya gramu 1 ya Rutheni tupu
| |
Jina la Elementi | Rutheni (Ruthenium) |
Alama | Ru |
Namba atomia | 44 |
Mfululizo safu | Metali ya mpito |
Uzani atomia | 101.07 |
Valensi | 2, 8, 18, 15, 1 |
Densiti | 12.45 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 2607 K (2334 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 4423 K (4150 °C) |
Hali maada | mango |
Mengineyo | haba sana |
Tabia
haririHutokea katika mitapo ya platini au pamoja na madini mengine ya elementi za kundi ya 10 katika mfumo radidia. Rutheni ni metali ngumu na kechu yenye rangi nyeupe-kijivu inayopatikana kama fuwele.
Matumizi
haririMatumizi yake ni katika aloi pamoja na platini, paladi, titani na wakati mwingine pia dhahabu kwa kusudi la kuongeza ugumu wa aloi hizi. Magusano ya umeme ya platini au paladi hudumu muda mrefu kama rutheni imeongezwa.
Jina
haririJina la "ruthenium" linechaguliwa 1844 na mfumbuzi wa kwanza aliyekuwa Mjerumani Mrusi Karl Klaus kwa heshima ya Urusi kwa sababu "Ruthenia" ilikuwa jina la Kilatini kwa Urusi.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rutheni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |