Titani ni elementi na metali yenye namba atomia 22 na alama Ti katika mfumo radidia wa elementi. Ni elementi mpito inayotafutwa sana kwa sababu ni nyepesi na imara sana na haiathiriwi rahisi kikemia, yaani haishikwi na kutu.

Titani
Jina la Elementi Titani
Alama Ti
Namba atomia 22
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 47.867
Valensi 2, 8, 10, 2
Ugumu (Mohs) 6.0
Kiwango cha kuyeyuka 1941 K (1668 °C)
Kiwango cha kuchemka 3560 K (3287 °C)
Asilimia za ganda la dunia 0.41 %
Hali maada mango

Kwa hiyo inatumiwa kama sehemu za aloi za chumapua mbalimbali kwa mfano kwa eropleni au mashine zinazokusudiwa kwa kazi kwenye maji ya chumvi au baharini.

Huchimbwa hasa Australia, Skandinavia, Amerika ya Kaskazini, Malaysia na Afrika Kusini.

Barani Afrika imeanza kuchimbwa pia Kenya, Msumbiji na Sierra Leone. Katika nchi hizo makampuni yanayoichimba pamoja na serikali zimepingwa mara nyingi kwa sababu ya hatari kwa ajili ya mazingira kutokana na uchimbaji na usimamizi hafifu.

  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Titani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.