Paladi
Paladi ni dutu sahili ya metali na elementi. Namba atomia yake ni 46 katika mfumo radidia, uzani atomia ni 106.42. Katika mazingira ya kawaida ni metali laini yenye rangi fedha-nyeupe inayohesabiwa kati ya metali za mpito. Alama yake ni Pd. Huhesabiwa kati ya elementi ya kundi la 10 (kundi la Platini).
Paladi (Paladium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Paladi (Paladium) |
Alama | Pd |
Namba atomia | 46 |
Uzani atomia | 106,42 u |
Valensi | 2, 8, 18, 18, 0 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 1828,05 K (1554,90 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 3236 K (2963 °C) |
Tabia
haririPalladi ni metali na elementi nyepesi kati ya elementi ya kundi la Platini. Kati ya elementi za kundi hilo lina kiwango cha kuyeyuka cha chini. Humenyuka haraka lakini haioksidishi bado kwenye halijoto ya wastani. Huhesabiwa kati ya metali adimu.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Paladi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |