Zonalmas Prog
Zonalmas Prog
Zonalmas Prog
MASS PROGRAMME
KUINGIA: -
(A) TWENDE NYUMBANI MWA BWANA
(Twende nyumbani mwa Bwana -hoya) x2
(Tuimbe tushangilie ,tupige vigelele tupige makofi hoya hoya ) x2
(B) NYANYUKENI
Nyanyukeni, waumini wote tufanye shangwe,kwa nderemo,kwa vigelegele na kwa
vifijo x2
(Kweli Bwana) asifiwe x3 mwathani arogoco x2
2. Uwezo wake Bwana Mungu haupimiki kwa mizani, mipango yake kwetu sisi
haiwezi kubadilishwa.
3. Enyi pigeni tarumbeta vinubi hata na matari, tuimbe wimbo wake musa na ule
wa mwanakondoo.
4. Pazeni sauti zenu kwa shangwe hata na vifijo tupatiane utukufu tumpe Bwana
siku zote.
(C) UBANI-SALA YANGU
(Sala yangu naipae mbele yako, kama moshi wa ubani)X2
MISA-MISA 1
BWANA ‘TUHURUMIE:-
Bwana utuhurumie X3
Kristu Utuhurumie x3
Bwana uthurumie X3
UTUKUFU:-
Utukufu juu mbinguni, na amani duniani, (kwao watu wote wa mapenzi) mema x2
1. Twakusifu (Baba) twakuheshimu (Baba) twakuabudu (Baba) twakutukuza (Baba)
twakutukuza ewe Baba.
4. Kuume kwa Mungu (Baba) unapoketi, (Baba) U Mtakatifu (Baba) ‘tuhurumie ewe
Baba.
5. Pamoja nawe (Baba) Roho Mtakatifu (Baba) kwa utukufu (Baba) wa Mungu milele
yote.
NENO
(A) INASONGA MBELE
T/B: Inasomga mbele injili
All: inasonga,inasonga mbele injili inasonga mbele X2
ALLELUYA- SUBUKIA
SADAKA
(A) LETENI SADAKA KAMILI
(Leteni sadaka kamili ghalani ) x2 ili
(chakula kiwemo katika nyumba yangu, asema Bwana, Bwana wa majeshi) x2
1. Mukanijaribu kwa njia hiyo - asema Bwana
Nitafungua milango ya mbingu- ,,
Na kuwamwagia baraka tele- ,,
3. Mtakachokiomba nitawapa- ,,
Nitawapa vyeo na mali nyingi - ,,
Na kuondoa umasikini- ,,
4. Nitawalinda na kuwasitawisha - ,,
Nanyi mtazaa matunda bora - ,,
Yatakayo dumu milele yote - ,,
(B) TAZAMA
Tazama Bwana tunakuja kwako (leo), twaleta sadaka zetu mbele
yako,tunakuomba Mungu Baba pokea.
2. Mahangaiko ya njaa sipati,zawadi hii yatoka kwa Mungu, kwa nini nisinyanyuke
nikamshukuru Mungu.
MATEGA
(A) BABA TUNALETA VIPAJI
1. (a) Baba tunaleta vipaji twakuomba sana pokea-Baba tunaleta twakuomba sana
pokea
(b) Twaja kushukuru kwa yote ‘ulotujalia wanao-Baba tunaleta twakuomba sana
pokea
Sop: Baba tunasema-asante asante
Alto: Kutupa uzima-asante asante
Tenor: Kwa kutukomboa-asante asante
Bass: Kutuweka huru-asante asante
2. a) Mkate na divai twaleta twakuomba sana pokea, baba tunaleta twakuomba sana
pokea.
b) ndiyo kazi yetu wanao twakuomba sana pokea, ---------------
3. a) Mazao ya mashamba twaleta twakuomba sana pokea, ------------------
b) Hata ni kidogo twaleta twakuomba sana pokea, -------------
4. a) Nazo fedha zetu twaleta twakuomba pokea, ---------
b) Utupe baraka twaleta twakuomba sana pokea, ----------------
(i) (Holy holy holy, (holy,holy) father almighty, Holy Holy Holy,Holy Holy Holy )x2
(ii) (Heaven and earth are filled with your Glory, Holy……………………………………) x2
KOMUNIO: -
(A) KAMA AYALA
Kama ayala aioneavyo kiu mito ya maji, ndivyo nami ninavyo kuonea kiu Mungu
wangu.X2
2. Umeniumba kwa ajili yako, ndio maana sishibishwi, utanituliza nafsi yangu
Mungu wangu uliye hai.
3. Karibu Bwana moyoni mwangu niishi ki Ekaristia, ili nipate raha ya kweli
nikupendeze siku zote.
(B) TUJONGEENI MEZANI
SHUKRANI:
(A) MAISHA YANGU
1. Maisha yangu (yote) nakutolea (wewe) eeMungu wangu (Bwana) unipokeke
(kwako) X2
(Bwana Maisha yangu mimi nampa-Bwana maisha yangu yote nampa Bwana,
nilivyo navyo vyote nimali ya Bwana
Maisha yangu yote nampa Bwana) X2
(B) NOTA
2. Enyi wasomi tuambieni, wanasayansi tujibuni, katika mambo ya mbinguni, nini kinafanyika
duniani.
3. Tumetambua kule mbinguni, hakuna kwenda ofisini,wala kumbi za burudani,hata kilimo
hakuna lakini.
4. Kumbe furaha za dunia hii, ni upumbavu ni wazimu, na anasa za zafaa nini, sisi waimbaji
tumeamua.
5. Waumini wote furahini, makasisi shangilieni,nanyi watawa jiungeni, kwa waimbaji hakuna
matata.
6. Upendo wake ni wa ajabu, fadhili zake za milele,huruma yake ni amini, msamaha wake
unashangaza
MWISHO- CHEREKO