Nyuki-jasho
Nyuki-jasho | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Halictus quadricinctus
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Nusufamilia 4, jenasi 17 katika Afrika ya Mashariki: |
Nyuki-jasho (kutoka kwa Kiing. sweat bees ni nyuki wadogo sana hadi kiasi wa familia Halictidae katika familia ya juu Apoidea ya oda Hymenoptera waliovutiwa na jasho, haswa spishi ndogo, ili kulamba chumvi. Hii ni familia kubwa yenye takriban spishi 4500 na jenasi 17 katika Afrika ya Mashariki. Zinatokea mabara yote isipokuwa Antakitiki.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Ukubwa wa nyuki-jasho ni mm 4-11. Kwa ujumla rangi yao ni nyeusi au kahawia mara nyingi pamoja na mistari ya nywele njano au nyeupe kwenye fumbatio, lakini wengine ni kijani, buluu au urujuani au wana fumbatio nyekundu. Baadhi yao wana mabaka njano mwilini, haswa madume. Kwa sababu familia hii ina spishi nyingi sana, zinatofautisha sana na haiwezekani kutoa maelezo ya nyuki hawa wote pamoja. Tembelea kurasa maalum kwa habari zaidi.
Takriban spishi zote za nyuki-jasho huonyesha viwango mbalimbali vya ujamii, ingawa wachache ni wapweke. Wanaweza kuwa karibu sana wa kijamii kama nyuki-asali. Pia kuna spishi za kidusia (nyuki-kekeo), haswa katika jenasi Sphecodes, ambazo zinafanana kwa kiasi fulani na nyigu na pia hupatikana katika Afrika ya Mashariki.
Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]
|
|
|
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Halictus aegypticola
-
Halictus brunnescens
-
Nomia amabilis
-
Spatunomia rubra
-
Sphecodes albilabris
-
Thrinchostoma fulvum