Nairi
Alpha Gruis, α Gruis, Alnair Nairi
Kundinyota | Kuruki (Grus) |
Mwangaza unaonekana | 1.7 |
Kundi la spektra | B6 V |
Paralaksi (mas) | 32.29 ± 0.21 |
Umbali (miakanuru) | 101 |
Mwangaza halisi | -0.72 |
Masi M☉ | 4 |
Nusukipenyo R☉ | 3.4 |
Mng’aro L☉ | 263 |
Jotoridi usoni wa nyota (K) | 13920 |
Majina mbadala | Al Na'ir, α Gru, CD−47° 14063, FK5 829, GCTP 5339.00, Gl 848.2, HD 209952, HIP 109268, HR 8425, SAO 230992 |
Nairi (ar., lat. & ing. Alnair pia α Alfa Gruis [1], kifupi Alfa Gru, α Gru) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Kuruki (Grus) na nyota angavu ya 31 kwenye anga ya usiku.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Nairi inayomaanisha “ng'avu” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema النّيّر al-nair wakimaanisha „ ng'avu ". Waarabu walihesabu nyota hii katika kundi la Hutu Junubi. Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Alnair" [3] .
Alfa Gruis ni jina la Bayer kwa sababu Alfa ni herufi ya kwanza katika Alfabeti ya Kigiriki na Nairi ni nyota angavu zaidi katika Kuruki - Grus.
Tabia
[hariri | hariri chanzo]Nairi iko umbali wa miakanuru takriban 101 kutoka Jua letu. Ina mwangaza unaoonekana wa mag 1.7 na mwangaza halisi ni -0.72. Spektra yake ni ya aina ya B6[4] au B7 [5]. "B" inamaanisha ni nyota ya safu kuu inayoyeyunganisha hidrojeni kuwa heliamu; inawezekana imeshafika tayari mwisho wa hatua hii na itahamia karibuni kuyeyunganisha heli kwa elementi nzito zaidi.
Kama nyota nyingi zinazofanana nayo inazunguka haraka kwenye mhimili wake kwa kasi ya angalau kilomita 236 kwa saa katika kanda ya ikweta yake.[6]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Gruis ni uhusika milikishi (en:genitive) wa "Grus" katika lugha ya Kilatini na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa, Beta, Gamma Gruis, nk.
- ↑ ling. Knappert 1993
- ↑ Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
- ↑ Gray, R. O.; et al. (July 2006), uk. 51 (HIP 109268)
- ↑ Malagnini, M. L.; Morossi, C. (November 1990), uk. 1018 (HD 209952)
- ↑ Kaler, Al Nair
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Constellation Guide:Grus
- Grus, kwenye tovuti ya Ian Ridpath, Star Tales, iliangaliwa Oktoba 2017
- ALNAIR (Alfa Gruis), kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 331 (online kwenye archive.org)
- Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
- Lane, Edward William : An Arabic - English Lexicon by in eight parts – 1872 (Grus Collection Arabic Materials Digitized Text Version v1.1 of reprint Beirut – Lebanon 1968) online hapa
- Gray, R. O.; et al. (July 2006), "Contributions to the Nearby Stars (NStars) Project: spectroscopy of stars earlier than M0 within 40 pc-The Southern Sample", The Astronomical Journal, 132 (1): 161–170 online hapa
- Hoffleit, D.; Warren, W. H. Jr. "HR 8425, database entry". The Bright Star Catalogue (5th Revised (Preliminary) ed.). CDS. Retrieved 5 September 2015. online hapa
- Malagnini, M. L.; Morossi, C. (November 1990), "Accurate absolute luminosities, effective temperatures, radii, masses and surface gravities for a selected sample of field stars", Astronomy and Astrophysics Supplement Series, 85 (3): 1015–1019, online hapa