Nenda kwa yaliyomo

Ukombozi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mkombozi)
"Kuvuka Bahari ya Shamu" kadiri ya Nicholas Poussin. Tukio hilo la karne ya 13 KK ndilo ukombozi wa msingi kwa taifa la Israeli.

Ukombozi, katika dini nyingi, ni msamaha au ondoleo la dhambi zilizopita na kinga dhidi ya laana na mateso mbalimbali, ya milele au ya muda.

Kwa kawaida ukombozi unasadikiwa kupatikana kwa njia ya kafara au sadaka fulani.

Kati ya dini zinazofundisha ukombozi, kuna Uhindu, Ubuddha na dini za Abrahamu, hasa Ukristo na Uislamu.

Katika aina kadhaa ya Ubuddha, ukombozi unaweza ukapatikana kwa juhudi za mhusika, anapofaulu kubandukana na tamaa zote.[1]

Katika Uyahudi, ukombozi ni ule ambao Mungu aliwatoa Wanaisraeli kutoka Misri, halafu kutoka Mesopotamia.[2]

Katika teolojia ya Ukristo, ukombozi ni hasa ule uliofanywa na Yesu kwa kulipia dhambi za wote msalabani halafu kufufuka mtukufu.[3][4]Waamini wanashiriki kiibada tukio hilo kwa njia ya ubatizo kwanza, na kwa kushiriki ekaristi maisha yao yote.

Katika Uislamu, ukombozi unafikiwa kwa kutofanya tendo lolote lisilolingana na dini hiyo.[5][6] Muislamu akifanya dhambi anatakiwa kumrudia Mungu kwa toba na matendo mema, kama sala na sadaka.[7][8][9]

Katika Ukristo

[hariri | hariri chanzo]

Mkombozi wa watu wote ni Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu, Bwana wetu. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yoh 3:16). “Katika yeye, tunao ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi” (Kol 1:14). “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti; ili, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi tuwe hai kwa mambo ya haki” (1Pet 2:24).

Yesu aliteswa hadi kuuawa msalabani ili abebe kwa upendo na kufidia dhambi za watu wote, alivyotabiriwa: “Tulimdhania ya kuwa amepigwa, amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona” (Isa 53:4-5). Tangu mwanzo Wakristo wanakiri kwa ufupi kwamba, “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo Maandiko” (1Kor 15:3). “Alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema” (Tit 2:14). “Alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote” (1Tim 2:6). “Ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa” (Eb 2:14-15).

Mungu Baba alihusika sana na sadaka ya Mwanae, kwa sababu “Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake… Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye” (2Kor 5:19,21).

Ajabu la ukombozi wa namna hiyo ni kwamba, “tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake” (Rom 5:10). “Hili ndilo pendo: si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanae kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu” (1Yoh 4:10). “Wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote” (1Yoh 2:2).

Kwa kuwa tumekombolewa kwa damu azizi ya Mwana wa Mungu, tunaonywa kwamba, “Mlinunuliwa kwa thamani, sasa basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu” (1Kor 6:20). “Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake” (1Pet 2:21) katika kuvumilia na kusamehe. Ndivyo alivyofanya Stefano kwa waliompiga mawe mpaka akafa: “Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, ‘Bwana, usiwahesabie dhambi hii’. Akiisha kusema haya akalala” (Mdo 7:60).

Jina lenyewe "Yesu" maana yake ni “Mungu Mwokozi”: alichaguliwa jina hilo kabla hajazaliwa, akitabiriwa kuwa “yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao” (Math 1:21). “Hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Mdo 4:12).

  1. Spiro, Melford (1982). Buddhism and Society: A Great Tradition and Its Burmese Vicissitudes. ku. xiv.
  2. "Reb on the Web". Kolel: The Adult Centre for Liberal Jewish Learning. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-21. Iliwekwa mnamo Novemba 1, 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Morris, Leon (1962). Redeemer, Redemption, 'The New Bible Dictionary'. Grand Rapids: William B. Eerdmans Publishing Company. ku. 1078–1079.
  4. "Redemption." Christian Classics Ethereal Library at Calvin College. July 2, 2009. http://www.ccel.org/s/schaff/encyc/encyc09/htm/iv.vii.lxxxv.htm
  5. Hava Lazarus-Yafeh (1981). Some Religious Aspects of Islam: A Collection of Articles. Brill Archive. uk. 48. ISBN 9789004063297. Iliwekwa mnamo 18 Februari 2015.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Yahiya Emerick (1 Nov 2011). The Complete Idiot's Guide to Islam, 3rd Edition. Penguin. ISBN 9781101558812. Salvation and redemption: Islam says our sincere faith and virtuous actions get us into heaven, not just a one-time conversion moment. {{cite book}}: |access-date= requires |url= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Mahmoud Mustafa Ayoub. "The Idea of Redemption in Christianity and Islam". BYU. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-13. Iliwekwa mnamo 18 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Chawkat Georges Moucarry (2001). Faith to Faith: Christianity & Islam in Dialogue. Inter-Varsity Press. uk. 110. ISBN 9780851118994. {{cite book}}: |access-date= requires |url= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Hava Lazarus-Yafeh (1981). Some Religious Aspects of Islam: A Collection of Articles. Brill Archive. uk. 48. ISBN 9789004063297. Iliwekwa mnamo 18 Februari 2015.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  • Redemption, BBC Radio 4 discussion with Richard Harries, Janet Soskice and Stephen Mulhall (In Our Time, Mar. 13, 2003)
  • ukombozi
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.