Nenda kwa yaliyomo

Kinywa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kielelezo cha kinywa cha binadamu

Kinywa au mdomo ni uwazi ndani ya kichwa mwenye shughuli tofauti kwa binadamu na wanyama wengi wenye uti wa mgongo.

  • ni mahali pa kuingiza chakula mwilini hivyo ni chanzo cha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula
  • ni nafasi ya kuingiza hewa mwilini hivyo pamoja na pua ni chanzo cha mfumo wa upumuo
  • ni mahali pa kutokea kwa sauti ambako sauti inayotengenezwa kooni inapokea umbo lake kwa msaada wa ulimi na midomo hivyo ni sehemu muhimu ya uwezo wetu wa kuwasiliana na wengine.

Kinapatikana kwa karibu wanyama wote wenye seli nyingi lakini kwa wanyama sahili kazi yake ni kuingiza chakula pekee.

Sehemu za kinywa cha binadamu ni pamoja na: meno, ulimi na fizi.

Mdomo wa mto

[hariri | hariri chanzo]

Neno mdomo hutumika pia kwa sehemu ya mto ambako unaishia kwa kuingia katika bahari, ziwa au, kama ni tawimto, katika mto mkubwa zaidi. Kisawe ni mlango wa mto.

Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kinywa kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.