Historia ya Romania
Historia ya Romania inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Romania.
Historia ya awali
[hariri | hariri chanzo]Homo sapiens aliishi katika eneo hilo walau kuanzia miaka 40,000 iliyopita.
Kabla ya kutekwa na Warumi mwanzoni mwa karne ya 2, walikuwepo makabila ya Wathraki, hasa Wadacha na Wagete.
Chini ya Dola la Roma kwa miaka 165 kulikuwa na wahamiaji wengi walioingiza lugha ya Kilatini.
Baadaye nchi ilitekwa na makabila mengine mbalimbali.
Katika karne za kati kulikuwa na falme ndogo tatu: Wallachia, Moldavia na Transilvania, nazo ziliendelea kuwa na madaraka fulani hata chini ya Dola la Osmani hadi karne ya 18 au 19.
Historia ya kisasa
[hariri | hariri chanzo]Romania ilianzishwa mwaka 1859 kwa kuunganisha Moldavia na Wallachia kwenye mto Danube ikapewa jina hilo mwaka 1866, ikajikomboa kutoka dola la Osmani mwaka 1877.
Kutokana na vita vikuu vya kwanza, Transilvania, Bukovina na Besarabia viliungana na Ufalme wa Romania.
Katika vita vikuu vya pili, Romania iliunga mkono Ujerumani dhidi ya Muungano wa Kisovieti hadi mwaka 1944.
Wakomunisti waliteka nchi na baada ya vita kwisha, Romania ilipoteza maeneo mbalimbali na kulazimishwa kujiunga na Mapatano ya Warshawa kama jamhuri ya kisoshalisti.
Baada ya mapinduzi ya mwaka 1989, Romania ilielekea demokrasia na uchumi wa soko huria.
Baada ya kujiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 2007, Romania imeanza kustawi na kwa sasa inaongoza pamoja na Malta zikiwa na ongezeko la 5% kwa mwaka.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Romania kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |