Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Kazakhstan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Kazakhstan inahusu eneo la jamhuri ya leo yenye jina hilo.

Jina la nchi limetokana na Wakazakhi ambao ni taifa la watu wanaotumia Kikazakhi, mojawapo ya lugha za Kiturki.

Eneo liliwahi kuwa sehemu ya milki mbalimbali lakini tangu karne ya 15 Wakazakhi walijaribu kuungana mata kadhaa bila mafanikio ya kudumu.

Tangu karne ya 17 milki ya Urusi ilianza kuenea katika Asia ya Kati na hadi mwaka 1865 eneo lote la Kazakhstan lilitawaliwa na Urusi.

Baada ya mapinduzi ya Urusi ya 1917 Wakomunisti walichukua nafasi ya Matsar wa awali wakafanya nchi kuwa jamhuri yenye kiwango cha kujitawala ndani ya Jamhuri ya Kirusi ya Umoja wa Kisovyeti.

Mwaka 1936 nchi ilipewa cheo cha jamhuri kamili ndani ya Umoja wa Kisovyeti, ikijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kikazakhi". Katika miaka iliyofuata Warusi na watu wa mataifa mengine ya Umoja huo walihamishwa nchini hadi Wakazakhi kubaki kuwa chini ya nusu ya wakazi wote.

Miaka 1990/1991 wakati wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti jamhuri ilijiondoa polepole. Kiongozi wa chama cha kikomunisti cha Kazakhstan Nursultan Nasarbajew alitangaza uhuru na kuwa rais wa kwanza akiendelea kutawala hadi mwaka 2019.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Kazakhstan kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.