Elisha
Mandhari
Elisha (kwa Kiebrania אֱלִישַׁע, Elisha, yaani "Mungu wangu ni wokovu", kwa [[Kigiriki Ἐλισσαῖος, Elissaios au Ἐλισαιέ, Elisaie, kwa Kiarabu الْيَسَع Elyasaʿ) alikuwa nabii anayetajwa katika Biblia na katika Qur'an.
Katika Biblia
Elisha alifanya unabii wake katika ufalme wa kaskazini wa Israel wakati wa wafalme Yoram, Yehu, Yehoahaz na Yehoashi [1]
Elisha alikuwa mwana wa Shaphat kutoka Abel-meholah aliyepata kuwa mfuasi wa nabii Elia (Kitabu cha kwanza cha Wafalme 19:16–19).
Baada ya huyo kuchukuliwa mbinguni katika kisulisuli (Kitabu cha pili cha Wafalme 2:9), Elisha alikubaliwa kama mkuu wa wanafunzi wake ("wana wa manabii") akajulikana nchini kwa karama zake, zikiwa ni pamoja na uponyaji.
Kwa miaka sitini (892–832 KK) alikuwa nabii (2Fal 5:8).
Tanbihi
- ↑ Achtemeijer, Paul L. ed., and Dennis R. Bratcher, Ph.D. "Elisha." HaperCollins' Bible Dictionary. New York, New York: HarperCollins Publishers, 1996.
Viungo vya nje
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Elisha katika Internet Movie Database – Animated depiction of the life of Elisha
- "Eliseus" article from The Catholic Encyclopedia
- Prophet Elisha in Carmelite Tradition
- Prophet Elisha Orthodox icon and synaxarion