Niobi ni elementi haba na metali ya mpito yenye namba atomia 41 katika mfumo radidia. Hutokea ndani ya mitapo na rangi yake ni ya kijivu ikisafishwa.

Niobi (Niobium)
Kipande cha bati la niobi
Kipande cha bati la niobi
Jina la Elementi Niobi (Niobium)
Alama Nb
Namba atomia 41
Mfululizo safu Metali ya mpito
Uzani atomia 92.90638
Valensi 2, 8, 18, 12, 1
Densiti 8.57 g/cm³
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 2750  K (2477 °C)
Kiwango cha kuchemka 5017  K (4744  °C)
Asilimia za ganda la dunia 1,8 · 10-3 %
Hali maada mango
Mengineyo Jina la kale: Colombium

Niobi ni metali laini yenye rangi ya kijivu. Tabia zake zafanana sana na Tantali. Niobi tupu inayokaa hewani inapata ganda la oksidi lenye rangi ya kijivu-buluu.

Kutokea

hariri

Haitokei kama elementi tupu lakini ndani ya mitapo mbalimbali kwa kawaida pamoja na Tantali.

Huchimbwa pale ambako mashapo yamekusanya kiasi kikubwa cha niobi ndani yake kwa mfano Brazil na Kanada. Kuna pia akiba zisizotumiwa bado huko Nigeria, Kongo (Kinshasa) na Urusi. Mwaka 2006 jumla la tani 60,000 ilitengenezwa.

Matumizi

hariri

Niobi hutuumiwa hasa katika aloi za feleji na metali kadhaa. Aloi hizi huwa ni imara sana.


  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Niobi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.