Kampaundi
Kampaundi (pia: msombo) ni dutu iliyoundwa kwa kuungana kwa elementi mbili au zaidi za kikemia katika hali thabiti kati ya masi au atomi zake. Atomi zake zashikwa kwa muungo kemia kuwa molekuli za dutu hiyo.
Tofauti ya kampaundi na mchanganyiko wa elementi
haririKampaundi ni tofauti na mchanganyiko wa elementi. Kwa mfano mchanganyiko wa atomi mbili za hidrojeni na atomi moja ya oksijeni ni gesi ya oksihidrojeni inayowaka rahisi kwa njia ya mlipuko. Mchanganyiko huu si thabiti. Lakini kama atomi zilezile zaingia katika muungo kemia zaunda dutu mpya ya H2O yaani maji.
Kampaundi hupatikana kwa hali maada mbalimbali kama vile gesi, mango au kiowevu.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kampaundi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |