Europi
Europi (Europium) ni elementi ya kikemia yenye alama Eu na namba atomia 63, maana yake kuna protoni 63 katika atomu. Europi imepangwa kwenye jedwali la elementi katika kundi la lanthanidi. Ni elementi inayotendana haraka sana na hewa au unyevu, hivyo inahitaji kutunzwa ndani ya viowevu visivyotendana nayo.
Europi | |
---|---|
Jina la Elementi | Europi |
Alama | Eu |
Namba atomia | 63 |
Mfululizo safu | Lanthanidi |
Uzani atomia | 151.964 |
Valensi | 2, 8, 18, 25, 8, 2 |
Densiti | 5.264 |
Kiwango cha kuyeyuka | °K 1099 |
Kiwango cha kuchemka | °K 1802 |
Hali maada | mango |
Europi ni metali laini sana: inaweza kukatwa kwa kisu. Kama haikuoksidika rangi yake ni nyeupe ya kung'aa.
Ilisafishwa mara ya kwanza kwenye mwaka 1901 ikapewa jina la bara la Ulaya (Europa). [1]
Matumizi ya europi hutumia tabia ya mmemetuko (phosphorescence) wa kampaundi zake. Ni elementi adimu.
Marejeo
hariri- ↑ "Periodic Table: Europium". Royal Society of Chemistry.
Viungo vya Nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Europi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |