MAISHA NI KUSUDI

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 17

UTAMBULISHO

Samuel Benjamini Mazota; mwalimu kwa huduma, kiongozi kwa asili, mwandishi
kwa kipaji/kupenda, mwanasiasa & mwanamuziki kwa kuchagua. Ni mhandisi kwa
ujuzi na mjasiriamali kwa lazima.
Ni mwanaume kwa utambuzi (SIJAOA).
Kwa neema ya Mungu ni Vice President wa BYF Tanzania – Taasisi inayojihusisha na
masuala ya vijana kuwasaidia wazifikie ndoto zao (BYF – Dare to Dreams),
Mwanafunzi na Kiongozi wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma –
Gavana, AISEC & ROTARACT Member, East Africa Brand ambassador wa
Elitebookstores, M/Mwenyekiti wa EEMC – CIVE, Former Publicity Secretary – UVCCM
& EEMC (UDOM), na ni kijana mwenzenu in my 20`s.

SHUKRANI
Awali ya yote ninatambua nafasi ya Mungu katika kunipa nafasi ya kuwa
muwasilishaji katika kongamano hili la watu wakuu sana na wazuri kama wewe.
Pili; ninawashukuru sana na kuwapongeza viongozi na waandaaji wa Programu hii.
Kwanza kwa kuiandaa pili kwa kuona ninafaa kuwa miongoni mwa walimu wa
darasa hili., na kutoa mchango wangu kwa kizazi changu. Kwangu mimi siichukulii
kikawaida kabisa nafasi hii ambayo angeweza kupewa mtu mwingine.
Tatu; ninawapongeza watu wote mlioko hapa ambao mmelipa gharama mbalimbali
za fedha, muda, maandalizi na hapa ninamaanisha waandaaji na kila mmoja aliyeko
hapa. Na nikuhakikishie haujapoteza muda, hautabaki kama ulivyo tukio hili
litakapomalizika.
YOUTH IS THE BEST TIME OF LIFE
Kwa mujibu wa UN watu wenye umri kati ya miaka 15 mpaka 24 but there is no
universally agreed international definition of Youth age group. Kwetu Tanzania mtu
mwenye umri wa miaka 18-35 kama mimi na wewe ni KIJANA.
Takwimu zinaonyesha kote duniani vijana ndio chachu ya maendeleo na mabadiliko,
Franz Kafka aliwahi kusema “YOUTH IS HAPPY b’se IT HAS THE ABILITY TO SEE THE
BEAUTY”. Youth is the best time to be rich and the best time to be poor. YOUTH
WITHOUT PURPOSE IS A DANGEROUS POSSIBILITY, ALWAYS.
Here's a lighthearted story to kick off a session about purpose, with a mix of humor
and a deep message for young people:

### Story: The Chicken That Wanted to Fly


Once upon a time, there was a chicken named Chiku. Chiku lived on a farm, but he
had big dreams—dreams that didn’t quite fit in with farm life. You see, Chiku
wanted to fly. He would stand on top of the chicken coop every morning, flapping
his wings with all his might, watching the eagles and hawks soar high in the sky. He
was convinced that he was meant to do the same.

One day, Chiku decided he’d finally take a leap of faith. He climbed up to the top of
the tallest fence on the farm, closed his eyes, and jumped, flapping his wings as
hard as he could! For a brief moment, he felt the rush of the wind, a sense of
freedom… until he crash-landed straight into a haystack, feathers everywhere.

The other chickens clucked and laughed, telling him, “You’re a chicken, not an
eagle! Chickens don’t fly!”

But Chiku was stubborn. Every day, he tried and tried, jumping off fences, trees,
even the farmer’s tractor. And every day, he landed in something different—a
puddle, a pig pen, a pile of manure. But he just wouldn’t give up.

One day, an old owl visited the farm and saw Chiku practicing his “flying.” The owl
said, “Young chicken, maybe you’re meant for something different than soaring in
the sky. There’s a purpose for everyone, but not everyone is meant to be an eagle.”

Chiku felt disappointed. “But if I’m not meant to fly, then what am I meant to do?”

The owl thought for a moment, then said, “Why don’t you try focusing on what
chickens do best?”

So Chiku decided to give it a shot. He started working on his pecking skills,


scratching around the farm, and leading the other chickens in finding the best
worms and grains. Eventually, Chiku became the most respected chicken on the
farm. He found his purpose not in trying to be something he wasn’t, but in being the
best version of himself—a chicken with great leadership, resilience, and
determination.

### Lessons for Youth and Purpose:


1. **Don’t Compare Your Purpose to Others**
Just because someone else seems to be soaring in one area doesn’t mean that’s
what you’re meant to do. Eagles were born to fly high, but chickens have their own
role to play.

2. **Stay True to Who You Are**


Often, we spend too much time trying to fit into molds that don’t suit us.
Recognizing your unique strengths can lead you to your purpose faster than trying
to be something you’re not.

3. **Be Persistent, But Flexible**


Chiku’s persistence was valuable, but his purpose became clear only when he
shifted his perspective. Sometimes, finding your purpose means being open to
change and looking within to see what you’re naturally good at.

4. **Embrace the Journey**


Chiku didn’t figure out his purpose overnight. Purpose is something you grow into
by embracing different experiences, learning from setbacks, and adjusting your
direction along the way.

5. **Find Purpose in Service to Others**


Chiku’s true fulfillment came when he led and helped his fellow chickens. Purpose
isn’t always about big dreams but often about how you use your strengths to uplift
others around you.

Start with this story and these lessons, and you’ll set a strong foundation for helping
the youth explore their own unique paths to purpose.
UTANGULIZI

▶️Moja ya janga kubwa linalowakumba wanadamu sio umaskini, sio magonjwa; ni


JANGA LA KUTOKUJUA KUSUDI LA KUISHI KWAO.
Tuna wachungaji wengi, tuna waalimu wengi, waimbaji wengi, wanataaluma wengi,
n.k ambao hawajui KUSUDI la kuumbwa kwao.
▶️Ile unafanya chochote haimaanishi unapatia, na haimaanishi uko sahihi. Ile
unapongezwa na watu wengine na matokeo unayaona sio kigezo ya kuwa uko
kwenye uelekezo sahihi.

▶️Watu wengi wakiulizwa wao ni kina nani wanapata shida sana kujielezea na
wengine hushindwa kabisa kujua wao ni kina nani kwa sababu hawajui kusudi lao
kwani wangejua kusudi lao ingekua rahisi kujua wao ni kina nani na isingewapa
shida kujitambulisha mbele za watu wengine

▶️Amua kulijua kusudi lako ili iwe rahisi kuiambia dunia wewe ni nani.

▶️Wengi wenu hapa kila mtu kuna kitu anafanya; na wakati mwingine anafanya
vizuri na matokeo yanayonekana, lakini kama unafanya na hujui kama ni kusudi
unaweza baadae kuja kujuta

▶️Wakati mwingine tunafikiria kuimba, kuhubiri, kufundisha, kuponya watu,


Kufanya charity kuna mfurahisha Mungu. Ukweli ni kuwa ukifanya hayo yote nje ya
kusudi la Mungu kukuumba HUMFURAHISHI MUNGU.
Ni kutokujua nini Mungu alikuwa anawaza wakati anakuumba, ni kutokujua kusudi
ni kutokujua KAZI YA MSINGI Mungu amekuleta duniani kuifanya.
Mungu hajajuleta duniani kufanya kila kitu ingawa una huo uwezo wa kufanya kila
kitu, kusudi ndio mpaka wa kukusaidia wewe kutokufanya kila kitu. Hata Mungu ana
uwezo wa kufanya mambo yote lakini bado hafanyi hayo yote.

Kusoma hakuna maana; kumtumikia Mungu hakuna maana; kufundisha hakuna


maana; kutafuta hela
hakuna maana na kumtumikia Mungu kwa namna yoyote kama UTAKUWA
HUJUI/HUTAMBUI KUSUDI
la hayo unayoyafanya ambalo kimsingi ndilo kusudi la kuombwa kwako.
Mfano: Wewe ni Mzazi; umeondoka kazini na umeacha maagizo kwa watoto wako.
Dunia sasa hivi ina vurugu nyingi sana na watu wako busy sana lakini hawajui nini
wanafanya na kwanini wanafanya, kwa Sababu hawajui Kusudi lao
TAFAKURI:
#1: Jambo gani moja ambalo uko tayari kufa unalifanya? Uko tayari kufa kama
utazuiwa kulifanya ili ulifanye?
#2: Ikitokea umebakiza siku ya leo tu kuishi, na kesho yako ni ama uwe mbinguni
au jehanamu? Mambo gani matano ambayo utayafanya kwa kuzingatia umuhimu na
uchache wa muda ulio nao.
#3: Kwanini unasoma? Baada ya kusoma kwanini utafanya utakachofanya? Halafu
iweje? Na iweje?
Jibu lako katika maswali yote uliyouliza kama itakuwa ni wewe tu na sio wengine
ujue HILO SIO KUSUDI LA ELIMU YAKO.
Tafakari hizi zitakupelekea kuona kuwa yamkini taaluma uliyonayo sio ya maana.
Fedha itakosa maana. Elimu yako itakosa maana.
Lakini pia matokeo utakayoyapata katika tafakari hizi yanatupa picha kuwa hayo
uliyoyapata kama majibu ndiyo mambo ambayo unatakiwa kuyafanya kila siku.
Ndiyo unatakiwa kuwekeza muda, fedha na nguvu zako zote kuyafanya.
Hayo ndiyo mwanzo wa UTAMBUZI wa KUSUDI LA KUUMBWA KWAKO

▶️ Mambo yote yanakosa maana pale ambapo YANAPOFANYWA bila JIBU LA SWALI
LA KWANINI. Mungu amekuleta duniani kwa kusudi ambalo usipolifanya ni sawa na
kupoteza MUDA DUNIANI.
KUSUDI LA UWEPO WA KITU, LINA NGUVU KULIKO KITU CHENYEWE

▶️Kusudi la Mungu kukuumba lina nguvu kuliko wewe mwenyewe.

Kindly, allow me to Read with you some BIBLE SCRIPTURES - For Believers buT
inaweza kukusaidia pia na wewe mwingine pia
“Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya
ubaya.”
— Mithali 16:4 (Biblia Takatifu)
Hekima za kuchukua hapa;
■God is too smart to do anything without knowing it's purpose. The purpose starts
before the actual thing. And this smartness should be adaptive to us.
■Bila kujali unajua au haujui ni muhimu sana ujue kuwa Mungu amevifanya vitu,
mambo na wewe kwa kusudi; hakukurupuka kukuumba wewe. KIMSINGI hakuna
chochote ambacho Mungu amekiumba bila Kusudi.
■Ile kwamba haujui kusudi la Mungu kukumba haimanishi kuwa Mungu alikurupuka
kukuumba, Mungu alikufikiria kwanza kabla hajakuumba.
■Kama Mungu amewafanya wabaya kwa kusudi la kutekeleza ubaya siku ya ubaya;
utagundua kuwa wewe ambaye alikuumba kwa sura na mfano wake lazima
alikuumba kwa kusudi.
■Mungu hakupi kusudi la kuumba baada ya kukuumba; amekuumba kwa kusudi.
Kuna sababu alitaka isababishwe na wewe ndiye msababishaji. Hivyo kusudi la
kuumbwa kwako haliombi kwa Mungu akupe; unaomba kwa Mungu akujulishe ili
uligundue.
■Kujua kusudi ni kujua nini kilikuwa kwenye AKILI ya Mungu wakati anakuumba,
anakufanya.
KILA JAMBO MUNGU AMELIFANYA KWA KUSUDI: BANGI, NETI
■ Ukweli mwingine ambao unapaswa kuujua kwa uzito wake ni kuwa;
Kila jambo, kila kitu ambacho Mungu AMEKIFANYA, lipo kusudi la yeye kukifanya.
■Ni Mungu ambaye ameumba/amefanya
a) Mwanadamu -Lipo kusudi la jumla la kukufanya mwanadamu na lipo kusudi
maalumu kwako la kukufanya mwanadamu
b) Jinsia (ke/me) - Kuna kusudi la wewe kuwa wa hiyo jinsia la jumla na la binafsi
c) Nafasi (mke/mume/n.k)
d) Ndoa na familia
Matendo 13:36 ; "Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika
kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu."
Hekima za kuchukua hapa;
■Mungu amekusudia kifo chako kitokane na wewe kuwa umemaliza kulitumikia
kusudi la Mungu. Hata hivyo lazima ujue kuwa Kusudi la kuumbwa kwako
limefungwa kwenye muda ambao umepewa kuishi hapa duniani.
Ikitokea muda wako wa kuishi duniani umeisha na hujajua kusudi la kuumbwa
kwako Utakufa na utakwenda kuwajibishwa huko.
■ Kusudi la kuumbwa kwako ni kwenye kizazi chako. Kizazi chako kikipita
wanapaswa kuja wengine kutumikia kizazi chao. Kizazi huwa kina lugha yake, tabia
zake, miondoko yake; hivyo unapaswa kuhakikisha UMETUMIKIA SHAURI LA BWANA
kwenye kizazi chako. Ukipishana na kizazi chako Utakuwa ZILIPENDWA kwenye
hicho kizazi na ukiwa huna legacy yoyote.
Moja ya mambo unapaswa kuyaepuka sana ni "Ni kuwa historia isiyo na chochote
ukiwa bado unaishi"
■ Wanaoishi na kulitumikia kusudi la Mungu muda wao wa kuishi duniani ukiisha
huwa hawafi bali WANALALA. Kulala ni kupumzika sio kuteseka.. Ni uchaguzi wako
kufa au kulala.
KUSUDI SIO NINI?

▶️Kusudi sio Taaluma (Daktari; Mwalimu; n.k)

▶️Kusudi sio Kipaji au karama

▶️Kusudi sio ajira fulani

▶️Kusudi sio huduma

▶️Kusudi sio kiasi fulani cha fedha.


Haya yote ni RASILIMALI za kukusaidia kulitimiza kusudi la Kuumbwa kwako.
Mfano; Kama Daktari, kusudi lake ni kukomesha vifo vya wamama wajawazito, sio
lazima awe daktari kutimiza kusudi hilo.
NB: Tazama vizuri hapo kwenye Kusudi sio nini maana watu wengi wanachanganya
sana, ukiwa na kipaji fulani au kiwango fulani cha fedha hImaanishi ndio kusudi
lako, hizo zote ni Rasilimali za kukusaidia kulitimiza kusudi, hivyo unapaswa kwanza
kulifahamu kusudi ili uweze kutafsiri raslimali.
KUSUDI/MAONO/WITO NI NINI?

▶️Kusudi ni sababu ya asili ya uwepo wa kitu kilipokuwa kinaumbwa au


kinatengenezwa.
MANUAL simu, gari nk

▶️Kusudi ni matokeo ya kujibu vizuri SWALI la KWANINI?

▶️Maono ni kusudi la Mungu lililofunuliwa ndani ya mtu/kitu.

▶️Wito ni kusudi lililoitikiwa baada ya kufunuliwa ndani ya mtu


KWA SABABU:
1. KUSUDI ndilo linaamua UJUMBE utakaotoa.
Mtu anaweza kutambua kusudi la mtu kwa kusikililiza ujumbe mkuu anaotoa mtu
katika kila jambo analofanya.
2. KUSUDI lina nguvu kuliko kitu chenyewe.
Hakuna lolote lenye maana pale ambapo kusudi halijulikani.
3. KUSUDI ndilo linamsaidia mtu KUJITUMIA, KUTUMIKA na KUTUMIWA vizuri.
"Wherever purpose is unknown misuse is inevitable" -Myles Munroe

▶️Kutokujua kusudi la Mungu kuweka SEX; ndipo tuna Uzinzi na Uasherati. (Ni tendo
lile lile ambalo
likitumika sawasawa na kusudi la Mungu linaitwa tendo la ndoa

▶️Mungu aliumba BANGI, inaonekana haina maana pale kusudi lake linapokosekana

▶️Nawewe kwa kutokujua kusudi lako unaweza kujitumia, kutumika au kutumiwa


kama bangi.

▶️Kuna watu wanahubiri, wanachunga, wanafundisha, n.k halafu bado hawajui


kwanini wanafundisha.
Mfano: "Mama yako kama alikuagiza upike maharage na akija apike wali mle usiku.
Wewe
ukaanza kufanya usafi wa nyumba, vyombo, ukaogesha watoto. Na mpaka anarudi
akakuta hujapika maharage, Atakupongeza?"
4. Kusudi ndilo linaamua KIWANGO CHA MAFANIKIO yako.

▶️Uchumi; ndoa; afya; ufaulu wako; ushawiashi wako.

▶️Kusudi ndilo linaamua kiwango cha fedha unatakiwa kumili; aina ya usafiri
unatakiwa kusafiria; aina nyumba unatakiwa kuishi.

▶️Kusudi ndilo linaamua kiwango cha ufaulu wako; kiwango cha elimu yako
5. KUSUDI ndilo huvuta na kuwafukuza aina ya watu kwako.
Kusudi linakuchagulia watu wa kuambatana nao.
6. KUSUDI linaamua ulishe nini Nafsi yako; roho yako na mwili wako.
Taarifa na chakula. Kusudi linakuamulia taarifa za kusikiliza; watu wakuwafatilia;
aina ya
mafundisho; aina ya movie; n.k
7. Kusudi ndilo humwepusha mtu na MASHINDANO.
Nionyeshe watu wenye mashindano nikuonyeshe watu wasiojua kusudi la kuumbwa
kwao.
8. Kusudi ndilo linakusaidia kutambua kuwa kuna njia nyingi za kufanya jambo
moja(kulitimiza)
Wengi wakifeli Udaktari; uhandisi wanakata tamaa na wengine kuishia kujiua kwa
sababu hawajui kusudi la kuumbwa kwao.
9. Uzuri wa kitu umefungwa kwenye kusudi lake. Hakuna kozi nzuri na mbaya;
Chochote kilichofungwa kwenye kusudi lako ndicho kinachovuta fedha, na ndicho
kitakupa jina.
10: Ni rahisi kutambua VIWEKEZO vyote ambavyo Mungu amekuumbia ili
kukusaidia kuliishi, kulitumikia na kulifia kusudi la kuumbwa kwako.
Kusudi litakusaidia kuomba viwekezo na rasilimali zingine ambazo hauna na unaona
zinaweza
kukusaidia kulitimiza kusudi.
DIMENSIONS YA KUSUDI
1. General
2. Specific
- Kusudi la mwanadamu limegawanyika katika sehemu kuu mbili; Biblia inasema
Yesu aliponya, alilisha watu mikate pamoja kufufua wafu hiyo ikiwa ni kusudi dogo
kutekeleza lile kuu la kukomboa ulimwengu. Yesu angeridhika na kuishia kwenye
yale makusudi madogo tu ya kulisha mikate na kuponya wagonjwa pasi na
kutekeleza Kusudi lake kuu labda leo kusingekua na historia ya Ukristo
Hupaswi kupuuzia kusudi kuu la kuumbwa kwako. Unapaswa Kulijua, kuliishi na
kulifia

UHUSIANO ULIOPO KATI YA NAFASI “Position” NA KUSUDI “Purpose”

ADAMU
UHUSIANO ULIOPO KATI YA KUSUDI NA MUDA

UHUSIANO ULIOPO KATI YA KUSUDI NA JINA

UHUSIANO ULIOPO KATI YA KUSUDI NA ELIMU

HATUA ZA KUFUATA ILI UWEZE KUTAMBUA KUSUDI MAALUMU LA


KUUMBWA KWAKO/NAMNA YA KULITAMBUA KUSUDI LA KUUMBW KWAKO
Mchungaji wangu James Kalekwa amewahi kuniambia kuwa *"Mwanadamu anakuja
duniani kama mtu mmoja, anapaswa kuondoka duniania kama taasisi"*
Taasisi huwa zina
■Maono/vision/purpose statement
■Mission statement
■Mifumo ya kuziendesha
Hivi ndivyo kila mmoja anapaswa kuwa; sasa ili ufikie kiwango cha kuwa taasisi
kinachoanza sio mfumo ni maono. Maono ndiyo yataamua aina ya mifumo
utakayojenga, mission statements(strategies)
Ndio maana kama mmeshagundua ninatamani muwe TAASISI yenye mifumo na
miongozo
Na hiyo inawezekana kwa kutambua kusudi. Mtu akitaka kukufahamu au
kujitambulisha atatazama MAONO YAKO
Hivi mnajua kila Chuo kina VISION yake lakini Wanafunzi huwa mnajiunga na chuo
bila hata kujua maono yake?
Taasisi zozote ambazo unazijua duniani zinatambulika kwa maono au kusudi
lakeUDOM ina vision statement yake;
UDOM ina vision statement yake; UDSM, Mzumbe
Lakini ni ajabu mtu anaweza akagraduate na hajui maono ya Chuo alichosomea 😀
Anyway tuyaache hayo; hakikisha hayampati mtoto wako
1. REJESHA MAHUSIANO YAKO NA MUNGU WAKO. (Mpokee Yesu)
Muumba ndiye anayejua KUSUDI lako, sio wazazi wako, waalimu wako, mazingira,
matatizo, n.k
Kuna watu ambao shida ndizo zimeyatafsiri maisha yao, wazazi wao, n.k. Ni kweli
Mungu anaweza kutumia watu, mazingira, vitu, shida, n.k lakini wengi sio hivyo.
"Kujitambua nje ya Mungu ni kujivuruga, na kujitafuta nje ya Mungu ni kujipoteza"
Kwa kuwa kujitambua nje ya Mungu ni kujivuruga na kujitafuta nje ya Mungu ni
kujipoteza hatua ya kwanza ya kutambua kusudi la kuumbwa kwako ni kuwa ndani
ya Mungu wako na yeye awe ndani yako.
Kumtambua Mungu ni kujitambua wewe. Kadri unavyomtambua Mungu ndivyo
unaendelea kujitambua.
Tukirudi kwenye Vitabu vitakatifu
1. BIBLIA
Mhubiri 7:29; "Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu,
lakini wamebuni mavumbuzi mengi. "
2. QURAN TUKUFU
SURA AL - FAATIHA (JUZU 1, ALI LAAM MIIM)
Sura hii inasema Mtu ameumbwa kwa ajili ya 'ibaadat' yaani kumwabudu Mwenyezi
Mungu na Kuwa Karibu naye wakati wowote, na ya kwamba daima mtu anahitaji
msaada wake ili kulitimiza kusudio la kuumbwa kwake
Kusudi sio lako, na kwa kuwa sio lako hulijui, na ili ulijue lazima uwe na mahusiano
mazuri na anayelijua. Hivyo hatua ya kwanza ya kujua kusudi lako kwa umaalumu
lazima ni UREJESHO WA MAHUSIANO YAKO NA ALIYEKUUMBA.
Hatuulizi mambo ya Vodacom, Tigo. Ukitaka kujua kwanini Vodacom ipo? huendi
kuuliza kwenye duka la Tigo wala huendi kwa wafanyakazi wa Vodacom unakwenda
kwa mwanzilishi wa Vodacom .
Ukitaka kujua kwanini TECNO zipo, usijiloge kwenda SAMSUNG watakwambia yaliyo
kwa ajili ya faida yao sio yako wala sio ya kusudi
Hivyo UHUSIANO WAKO NA MUNGU UNAPASWA KUWA SAWA UNAPOANZA SAFARI
YA KUJITAFUTA, NA KUTAFUTA MAPENZI YA MUNGU KWAKO
Ina maanisha nini kurejesha mahusiano yako na Mungu
i. Kama ulikuwa umegombana na Mungu kwa namna yoyote, Unapaswa upatane
naye.
Sura AL-FAATIHA inayo Maombi yaliyokamilika yanayotosheleza kabisa haja za
mwanadamu.
Mwishoni maombi hayo yanatoa maonyo kwamba ikitokea mtu amepotea na akawa
mbali na Mwenyezi Mungu anapaswa kugeuka kwa Ar-Rahmaan (Mungu wa
Rehema)

ii. Umpokee Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako, upate msamaha wa
dhambi.
Baada ya mahusiano yako na Mungu kuwa Mazuri

2. OMBA (Muombe Mungu akufunulie kusudi lako).


Na hapa ile njia ambayo Mungu huwa anakupatia majibu ya unayomwomba ndiyo
kwa asilimia kubwa ataitumia kukupatia majibu yako.
Aliyekuumba anajua kwanini alikuumba. hivyo ukimuuliza atakwambia.Ni kiburi cha
hali ya juu sana, kuomba Mungu akupe mke na hujajua kusudi la kuumbwa kwako
na hujamwomba.
Ni kiburi kuomba Mungu akupe ada ya shule wakati hujui kwanini alikuumba na
hujaomba.
Ni kiburi kumwomba Mungu ufaulu mtihani na hujawahi kuomba akujulishe kwanini
alikuumba
Ukitaka kujua kwanini TECNO walitengeneza TECNO huendi kuwauliza IPhone.
Unakwenda kuwauliza TECNO.
Aliyekuumba anajua kwanini alikuumba, hivyo ukimuuliza atakwambia.
Wangapi kati yetu huwa wanaomba vitu kwa Mungu wao? Wangapi huwa
wanapokea vitu kwa Mungu walivyoomba? Wangapi wanajua kusudi la kuumbwa
kwao?
Ni kiburi kiwango cha lami, kuomba Mungu akupe mke na hujajua kusudi la
kuumbwa kwako na hujamwomba. Ni kiburi kuomba Mungu akupe ada ya shule
wakati hujui kwanini alikuumba na hujaomba. Ni kiburi kumwomba Mungu ufaulu
mtihani na hujawahi kuomba akujulishe kwanini alikuumba
Kuomba kujua kusudi la Mungu kukuumba ni MAPENZI YA MUNGU. Kama unataka
kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu omba kujua kwanini alikuumba.
"OMBENI NANYI MTAPEWA, ... KWA KUWA KILA AOMBAYE HUPOKEA" Mathayo 7:7,8
Ukiomba Mungu atakujulisha kupitia
i. Ndoto/maono -(Usipuuze ndoto na maono utayaona)
ii. Watumishi wake -(Usije hata siju moja wanayoyasema watu hasa
watumishi na watu
wanaokuzunguka). Watu huwa wanatutambua na kutuita kwa huduma tunazozitoa
kwao.
iii. Sauti yake mwenyewe (Tenga muda wa kusikiliza wakati unaomba - Paulo
na Barnaba)
Matendo 13:1 -3
"Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao
ni Barnaba, na
Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa
kunyonya wa mfalme
Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga,
Roho Mtakatifu
akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha
kufunga na kuomba,
wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao."
iv. Neno lake (Hakikisha unasoma Neno la Mungu)
Mtu mmoja aliomba akasema "Mungu kama hunijulishi kwanini uliniumba bora
uniue, sababu sina maana ya kuishi nasijui kwanini naishi"
So amka, lala, kula, n.k. moja ya jambo unafanya ni KUOMBA
Maisha yako hayana tofauti na maisha ya mbuzi kama hujui kwanini Mungu
alikuumba.
Namaanisha hivi maisha yako hayana tofauti na ya paka/mbwa kama hujui kwanini
unaishi.
Ndio maana mtu asiyejua kusudi anaweza kuwa mbaya zaidi kuliko hata wanyama.
Hivyo ni hatari kuishi na haujui kwanini unaishi. Omba ujue kwanini unaishi.
Na kwakuwa ni mapenzi yake; ATAKUJULISHA
KWA KUWA KILA AOMBAYE HUPOKEA
NIAMINI MIMI;
MOJA YA VITU VINAVYONGEZA THAMANI YAKO BINAFSI NI KUJUA KUSUDI
(KUKITAMBUA KWA UJUMLA WAKE)
Kusudi litakuchagulia hata watu wa kutembea nao, mahali pa kwenda, ule nini,
usome nini, NA KWA KUFANYWA HIVYO AUTOMATICALLY UNAKUWA tofauti na watu
wa kawaida

3. KUTAFUTA
Hatua hii sio mbadala kabisa wa mbili zilizopita. Unapoendelea kutafuta huku
ukiomba Mungu anakufunulia kupitia kutafuta kwako.
Kwa kuwa kila ATAFUTAYE HUPATA (Mathayo 7:8b)

Kutafuta huku kunahusisha AKILI yako ambayo nayo ni Mungu amekupa.

Mungu ameonya kutokuitegemea akili yako ndio maana unatakiwa kuomba na kuwa
na mahusiano naye mazuri. Lakini amesisitiza sana UITUMIE AKILI YAKO IPASAVYO.
Kwenye KUTAFUTA njia utakayoitumia hapa ni KUTAFUTA NI KWA KUJIULIZA
MASWALI MAGUMU ambayo wengi huwa hampendi kujiuliza na kujijibu au kuulizwa
kabisa
Nasisitiza kuwa UNAENDELEA KUJITAFUTA HUKU UKIENDELEA KUJIULIZA.
MKUMBUKE UNACHOFANYA NI PURPOSE DISCOVERY. Tayari kusudi lipo na Mungu
analijua. Na alikuumba nalo. Unachofanya ni kuligundua.
Sasa miongoni mwa TOOL ya kukusaidia kuligundua hilo kusudi ni kwa KUJIULIZA
MASWALI ndani ya Mungu.
Swali lolote utakaloulizwa au kujiuliza unatakiwa kulijibu kiwango chako cha majibu
ikiwa ni Mungu```

Ask and think on paper


Hatua hii unatakiwa kuwa nayo makini nayo sana. Maswali yote ambayo unajiuliza
na kuyajibu unatakiwa uwe unaandika.
Kila jibu la swali lolote unalojiuliza hakikisha majibu yako yote unaandika
BAADHI YA MASWALI YATAKAYOKUSAIDIA KUJITAFUTA NA KUJIPATA:
a) What makes you uncomfortable when others are comfortable?
"Your assignment will keep you uncomfortable when others are comfortable" Solly
Mahlangu
Yatima; watoto wa mtaani; wajane; Wagonjwa;
Kuna watu hapa ambao tunaweza kupishana na watoto wa mtaani na isitusumbue
lakini kuna mtu hawezi kuridhika.

That's your assignment

Kuna watu hawapendi kuona vitu vinafanywa kwa ukawaida, hata kama wengine
wameridhika kwao MIOYO YAO INAPATA SHIDA KABISA
b) Ni alama gani uko tayari kuiacha kwenye mioyo ya watu, utakapondoka duniani.
Nini utakuwa mchango wangu kwa ulimwengu? Nini itakuwa ladha yako
utakayoiacha duniani?
Kusudi ni kwa ajili ya watu sio wewe.
Eg. Mother Teresa
c) Ni ujumbe gani ambao unauona katika kila unachokifanya? Kama unaimba,
unachora, unahubiri, n.k
"Kusudi lako linaamua ujumbe utakaoutoa". Ambwene Mwasongwe; Paul Clement;
Abiudi Misholi –FARAJA (Faraja Band);

Jumbe zako zinaweza zikawa ni za KUONYA; KUKARIPIA; KUKOSOA; KUTOA MAWAZO


MBADALA; KUFARIJI; KUREJESHA; n.k
Ni
d) Aina gani ya watu na ujumbe wao unapenda kufatilia? Mimi napenda waalimu
wenye details. Niko tayari kuhudhuria mkesha wa mafunzo kuliko mkesha wa kusifu
na kuabudu.
Aina hiyo ya watu, aina hiyo ya mafundisho, aina hiyo ya taarifa zinaendana kabisa
na kile Mungu amekuleta duniani kukifanya.
Mkumbuke tulisema kuwa KUSUDI Huwa linaamua aina ya jumbe utakazotoa, sasa
kikanuni kabisa huwa ni kuwa HUWEZI KUTOA AMBACHO HAUNA. UJUMBE
UTAKAOTOA KWA SEHEMU KUBWA UNAAMULIWA SANA NA UJUMBE UTAKAOKULA.
"What you eat reveals who you are"
Jiulize na ujijibu ni aina gani ya jumbe, aina gani ya watu ambao unapenda
kuwafitilia. Hata ukijua kusudi lao kusudi lako litakuwa halipishani sana na wao.
Lakini pia KUSUDI/PURPOSE/VISION huwavuta watu na kuwafukuza watu.
Vision attracts and repels people
Kwa hiyo watazame hao watu
Ukiangalia tu hapo unaweza kuelewa kusudi langu ni lipi;
Sasa ukumbuke maswali hayo yanakusaidia pale ambapo huchagui maswali ya
kujibu.
# Swali la kujibu:
AINA GANI YA WATU UNAWAFITILIA, AINA GANI YA JUMBE UNAFATILIA SANA, N.K
e) Uko tayari kutoa rasilimali zako (muda, fedha, vitu) kutoa mchango gani kwa
watu bila kutarajia malipo?
"Kusudi ni mchango au ladha yako kwa ulimwengu na watu wanaokuzunguka.
Kusudi ni chumvi na nuru ya ulimwengu"
Kipi ambacho uko tayari kujitolea kufanya kwa ajili ya watu wengine bila kulipwa?.
Andika yote hayo
Kama sio moja ni mengi andika yote
f) Kwanini unafanya hicho chochote unachokifanya? Jibu lako likiwa sio kwa ajili
yako; kweli na nia ya dhati kabisa linakupelekea kwenye utambuzi wa kusudi lako.
Hivyo angalia NIA YA KILA KITU AMBACHO UNAFANYA
Nia yako ya kuimba; nia yako ya kuhubiri; nia yako ya kufundisha; nia yako ya
kufanya charity; nia ya kuongoza; n.k
Andika yote, na majibu uandike yale ambayo kwa moyo mkunjufu sio kwa ajili
yako```
g) Ni Jambo gani moja ambalo uko tayari kufa unalifanya? Na Uko tayari kufa kama
utazuiwa kulifanya ili ulifanye?
h) (i) Ni jambo gani au mambo gani ambayo Uko tayari kufanya bila kulipwa
chochote?
(ii) Ni jambo gani ambalo utaendelea kulifanya hata kama unafedha zote
zinazosubiri matumizi na sio matumizi yanayosubiri fedha? Utakuwa ukifanya nini?
"Tafuteni nanyi mtaona; kwakuwa kila atafutaye huona" Mathayo 7:7-8.
4. Jishughulishe kuyahudumia maisha ya Watu wakati ukisubiri uhakikisho wa
kusudi na wito wako.
Hakuna yeyote ambaye amepewa au amethibitishiwa cha kufanya na kujitambua
akiwa hafanyi
chochote. Mathayo 7:7, 8 "Bisheni nanyi mtafunguliwa"
"Kumtumikia Mungu ni kuwatumikia watu. Huwezi kumtumikia Mungu kama
huwatumikii watu."
Ndio maana Mungu anatambua hata viongozi wa kisiasa na serekali kuwa ni
watumishi wake.

KULIISHI NA KULIFIA KUSUDI


1. ANDIKA KUSUDI LAKO/MAONO/WITO WAKO

▶️Vitu vyote vya msingi na Vya maana na Vyenye MATOKEO huwa VINAANDIKWA,
usiassume unafahamu. ANDIKA.

▶️Iandike Njozi yako; Vision Statement


2. WEKA MPANGO MKAKATI WA NAMNA YA KULIISHI

▶️Kusudi lako unatakiwa kuliishi kila siku, kila wiki na kila mwezi.

▶️Chochote unachokifanya katika maeneo yote ya maisha kinaathiri moja kwa moja
KUSUDI lako kwa
namna chanya

▶️Hakikisha una njia nyingi, una rasilimali nyingi za kulitimiza kusudi lako. Kama
issue ni kuokoa vifo
vya mama wajawazito hakikisha sio lazima uwe daktari kulitimiza hilo.```
3. TAFUTA TAARIFA na MAARIFA MENGI YATAKAYOKUSAIDIA KULIENDESHA KUSUDI
LAKO.
"It's information that drives the vision"
-Bishop David Oyedepo
a)Omba Mungu akupe details zote za msingi kukusaidia kufahamu kila kitu kuhusu
kusudi lako
b)Jifunze; SOMA, sikiliza;
HUWEZI WAPA KITU AMBACHO WEWE HUNA - Tafuta Maarifa Mengi.
Mfn; Financial freedom - 20x Age
GROWTH IS INTETIONAL
4. TAKE THE FIRST STEP

▶️Anzia ulipo, anza na ulicho nacho


"Wengi wetu hatufanikiwi kuanza katika tunayoyafanya kwa sababu huwa huwa
tunahangaika kusubiri
tuwe na tusivyokuwa navyo ili tupate tusivyokuwa navyo wakati tulitakiwa kutumia
tulivyonavyo
kupata tusivyokuwa navyo."

▶️Don't dispise humble beginnings


5. JITOE, NA UWE TAYARI KUFA UKILITUMIKIA KUSUDI.
Maisha yako yote yawe ni Kuishi kwa ajili ya wengine

APPRECIATIONS
1. Somo hili limekusaidiaje na kukujenga vipi kiufahamu kuhusu kusudi?
2. Ni hatua zipi utachukua ili uweze kujua kile umeumbiwa kufanya na uanze
kukiishi kabla hujatoweka duniani
I thank all the participants who have attended the sessions, raised pertinent
questions and shared experiences on discovering the Purpose. I would like to
congratulate all of you for your dedication and active engagement in the learning
experience. Indeed, I have heard a lot of good feedback.

I would like to take this opportunity to appreciate Mr. Elijah for the time and effort
you invested in preparation for this symposium. You are appreciated for all you do.
Thank you so much.

Yours,
MAZOTA S.B

You might also like