Ushairi 50 & QSNS 0706 851 439

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 113

USHAIRI 50 NA MASWALI

Page | 1
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 1
Soma shairi lifuatalo kwa makini halafu ujibu maswali yanayofuata
1. Naja sasa ni ndiyani, naja kwetu Mzalendo
Naja nirudi nyumbani, nilowekwa nako kando
Kwetu’ mi nakutamani, kulo na mwingi uhondo
Nijaye ni yule nyundo, misumari hadharini

2. Naja kwingine kuwapi, kulojaa langu pendo?


Huenda nende kwinginepi, sawa nako kwa muundo?
Kaa kwingine anapi, ela kwenye lakwe gando?
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

3. Naja nije rudi papo, panigedeme mgando


Ningaambwa kwetu hapo, kwamba kwanuka uvundo
Sitakwenda penginepo, tarudi kuko kwa mwando
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

4. Naja sitapakimbiya, ningambwa kuna vimondo


‘Takuja kuvilekeya, vinganijiya kwa vundo
nilipozawa tafiya, sikimbii kwenda kando
nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
5. Naja hiwa ‘mekomaa, kuzidi nilivyo mwando
Tena n’najiandaa, kwa fikira na vitendo
Kwetu nije kuifaa, na kuitiliya pondo
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

6. Naja na ingawa naja, siwaeki mifundo


Moyo wangu ushatuja, mawi nalotendwa mwando
Ela wataoningoja, na vyao viwi vitendo
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

7. a) Eleza jinsi ‘uzalendo’ wa mshairi unavyojitokeza katika beti za 1


na 2 alama 4
b) Fafanua jazanda zinazopatikana katika mshororo:
Kaa kwingine anapi, ela kwenye lakwe gando? alama 2
c) Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari alama 4
d) (i) Katika ubeti wa 5 mshairi amebadilika Eleza alama 2
(ii) Ananuia kufanya nini pindi arudipo? Alama 2
e) Eleza ujumbe unaopatikana katika ubeti wa 6 alama 2
f) Andika maneno haya katika kiswahili sanifu
alama 2
a. Mwando
b. Ningambwa
g) Kibwagizo cha shairi kinampa sifa gani mshairi? Alama 2

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 2
Soma shairi hili kisha ujibu maswali.

Jukwani naingia, huku hapa pasokota,


Kwa uchungu ninalia,hii tumbo nitaikata,
Msiba mejiletea,nimekila kiso takata,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Wazee hata vijana,wote umewasubua,


Huruma nao hauna,heshima kawakosea,
Ukambani na Sagana,hata mbwa wararua,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Wahasibu ofisini,kibwebwe mejifunga,


Miaka mingi vitabuni,ili wasikose unga,
Nadhari wanadhamini,hesabu wanazirenga,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Wapenzi wa kiholela,pia wanakuogopa,


Baada yao kulala, wana wao wanatupa,
Wakihitaji chakula,wanachokora mapipa,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Wafugaji hata nao,kama dawa wakwamini,


Hawajali jiranio,wamesusia amani,
Wanaiba ng'ombe wao,na kuzua kisirani,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Nayo mizozo ya maji, kaonekana kwa mara,


Hiyo nayo ni dibaji,sababu sio harara,
Njaa wahepe wenyeji, huo ndio mkarara,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Ningeweza kukuuza,ingekuwa siku njema,


Tena kwa bei ya meza,sokoni nimesimama,
Wala tena singewaza,kuhusu wali na sima,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Hatima umefikika,naenda zangu nikale,


Mate yanidondoka,kwa mnukio wa wale,
Naomba kwenda kukaa,wala sio nikalale,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Maswali
i Lipe anwani mwafaka shairi hili. (Alama 2)
ii Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu. (Alama 2)
iii Huku ukitolea mifano mwafaka, taja arudhi zilizotumiwa katika ubeti wa
Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
tatu. (Alama 4)
iv Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (Alama 4)
v Thibitisha kuwepo kwa idhini ya ushairi. (Alama 2)
vi Taja madhila anayoelezea mtunzi wa shairi hili yaletwayo na tumbo.
(Alama 4)
vii Elezea maana ya maneno yafuatayo. (Alama 2)

(a) Dibaji

(b) Harara

USHAIRI WA 3
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
LAU HAKUNA MAUTI. Na Abdalla Said Kizere
1. Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

2. Dunia ingetatana, na kizazi katikati,


Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,
Vipi tungelioana, na kuzaa hatuwati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
3. Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,
Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,
Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

4. Walakini Subuhana, kapanga sisi na miti,


Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti
Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

5. Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,


Kwa uwezowe Rabana, kaipanga madhubuti,
Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

6. Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati,


Sote tungeambatana, kama ukosi na shati,
Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

7. Peleleza utaona, hayataki utafiti,


Kama tungelikongana, ingekuwa ni bahati,
Vipi tungesukumana, katika hiyo hayati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
8. Mbele sitokwenda tena, hapa mwisho nasukuti,
Yaoleni waungwana, shauri yake Jabaruti,
Yote tuloelezana, katenda bila senti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

MASWALI
a) Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza (alama 2)
b) Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi (alama 4)
c) Eleza umbo la shairi hili (alama 4)
d) Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano (alama 4)
e) Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi (alama 2)
f) Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika
shairi hili (alama 2)
g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kulingana na shairi (alama 2)
(i) Tiati _________________
(ii) Shani_________________

USHAIRI WA 4
Soma shairi lifuatalo, kisha ujibu maswali; (alama 20)
Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwendani,
Afiya yangu dhahili, mno nataka amani,
Nawe umenikabili, nenende sipitalini,
Sisi tokea azali, twenda zetu mizimuni,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
Mababu hawakujali, wajihisipo tabani,
Tuna dawa za asili, hupati sipitalini,
Kwa nguvu za kirijali, mkuyati uamini,
Kaafuri pia kali, dawa ya ndwele Fulani,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mtu akiwa halali, tumbo lina walakini,


Dawa yake ni subili, au zongo huauni,
Zabadi pia sahali, kwa maradhi yalondani,
Au kwenda wasaili, wenyewe walo pangani,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mtu kwenda sipitali, ni kutojuwa yakini,


Dakitari k’ona mwili, tanena kensa tumboni,
Visu vitiwe makali, tayari kwa pirisheni,
Ukatwe kama figili, tumbo nyangwe na maini,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Japo maradhi dhahili, kuteguliwa tegoni,


Yakifika sipitali, huwa hayana kifani,
Wambiwa damu kalili, ndugu msaidieni,
Watu wakitaamali, kumbe ndiyo buriani,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
Mizimu wakupa kweli, wakueleze undani,
Maradhiyo ni ajali, yataka vitu thamani,
Ulete kuku wawili, wa manjano na kijani,
Matunda pia asali, vitu vyae chanoni,
Nafwatani sipitali, na dawa zi mlangoni?

MASWALI – USHAIRI (ALAMA 20)


a) Lipe kichwa mwafaka shairi hili. (alama 2)
b) Mtunzi alikuwa na lengo gani alipotunga shairi hili? (alama 2)
c) Mbona mshairi hataki kwenda hospitali? (alama 4)
d) Kwa kuzingatia muundo wa shairi hili, eleza mbinu zilizotumika
(alama 6)
e) kwa nini mshairi alitumia ritifaa katika ushairi? (alama 2)
f) Andika maana ya maneno yafuatayo yalivyotumika katika shairi
(alama 4)
i) Dhahili
ii) Azali
iii) Sahali
iv) Tumbo nyangwe

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 5
1. Soma shairi lifuatalo kwa makini kisha ujibu maswali.
Niokoa Muokozi, uniondolee mashaka.
Kuyatukua siwezi, mjayo nimedhikika
Nimekithiri simanzi, ni katika kuudhika
Mja wako nasumbuka, nipate niyatakayo.

Mja wako nasumbuka, nataka kwao afua


Nirehemu kwa haraka, nami nipate pumua
Naomba hisikitika, na mikono hiinua
Mtenda ndiwe Moliwa, nipate niyatakayo.

Mtenda ndiwe Moliwa, we ndiwe Mola wa anga


Mazito kuyaondoa, pamoja na kuyatenga
Ukauepusha ukiwa, ya pingu zilonifunga
Nikundulia muwanga, nipate niyatakayo

Muwanga nikundulia, nipate toka kizani


Na huzuni n’ondolea, itoke mwangu moyoni
Mambo mema niegheshea, maovu nisitamani.
Nitendea we Manani, nipate niyatakayo.

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
Igeuze yangu nia, dhaifu unipe mema
Nili katika dunia, kwa afia na uzima
Moliwa nitimizia, yatimize yawe mema
Nifurahike mtima, nipate niyatakayo.

(a)Shairi hili ni la bahari gani? Eleza. (alama 2)


(b) Taja madhumuni ya shairi hili. (alama 3)
(c) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
(d) Thibitisha namna uhuru wa kishairi unaibuka katika shairi. (alama 4)
(e) Andika ubeti wa pili katika lugha sufufu. (alama 4)
(f) Toa maana ya:
(i) Nimedhikika
(ii) Muwanga nikundulia
(iii) Nifurahike mtima (alama 3)

USHAIRI WA 6
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Wataalamu muwe macho, vuani moto muenge,
Muenge hicho ambacho, cha watu wenye mawenge,
Mawenge yenye kijicho, kiswahili wakivunge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.

Sichafue kiswahili, barakala tuwapinge,


Apige kila hali, wasiguse tuwainge,
Tuwainge wende mbali, kiswahili tujijenge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.
Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Sichafue yetu lugha, waharibu Wabanange,


Wabanange iwe nyagha, waiweke tengetenge,
Lugha kuitwa; ulugha, lafidhi watia denge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.

Tuichange heshima, na ulugha tuupinge,


Tuhifadhi kwa salama, na kisingio unyonge,
Kelele za maamuna, si watu ni visinge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.

Kasema sheikh Amri, kiswahili tukisenge,


Kistawi kinawiri, kitumike kwenye bunge,
Hii ni yetu fahari, lugha yetu tuichunge.
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.

Kikipatwa na maradhi, kwa sindano tukidunge,


Kila jama kutidhi, kipatwe hapo tupunge,
Tukitia mfawadhi, kama kunde na kihenge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.

MASWALI
(a) Ni mtindo gani aliotumia mshairi katika kutunga ubeti wa 1 na 2.
(fafanua kwa kutoa mfano)(alama 4)

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
(b) Mshairi ametoa mapendekezo kadha katika shairi kuhusu jinsi ya
kuimarisha na kuhifadhi lugha ya kiswahili. Taja na ufafanue matano kati ya
hayo. (alama 5)
(c) Mshairi anazungumza na akina nani? Anazungumzia nini? (alama 4)
(d) Mshairi ametumia tamathali mbalimbali kuwasilisha ujumbe wake. Taja
mifano mitatu tofauti ya tamathali hizo. (alama 3)
(e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi.
(alama 4)
(i) Muenge
(ii) Barakala
(iii) Mtawadhi
(iv) Maamuma.

USHAIRI WA 7
6. i) Una moyo gani N’nakuuliza Wangu mhisani
Na kiasi gani Unavyojiweza Ijapo tufani
Ukiwa laini Utajipoteza Usijibani
Kusimama Pweke Kwataka Makini

ii) Zitavuma pepo Zitapupuliza Uanguke chini


Ela uwe papo Unajikweleza Na kujiamini
Utikiishapo Umejiuiza Pigo la moyoni
Kusimama Pweke Kwataka Makini
Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

iii) Utie migati Ya kutuoteza Hapo aridhini


Kwa nia na dhati Usiogeuza Au kuihini
Zidate baruti Uwe wapuuza Welele usoni
Kusimama Pweke Kwataka Makini

iv) Sishike vishindo Na mauzauza Ya kukuzaini


Kita kama nyundo Ukinuiliza Unayoamini
Na uje mkondo Utadikimiza Kujipa mizani
Kusimama Pweke Kwataka Makini

v) Wengine wasiwe Unaoweleza Yaliyo maani


Wewe ndiwe Unaoweleza Yaliyo maani
Ela kichukuwe Pia kujikaza Katika midani
Kusimama Pweke Kwataka Makini

a) Lipe kichwa shairi hili (al 2)


b) Kwa nini kusimama pweke “kwataka makini ’’ (al 2)
c) Ni hatua gani zinazopendekezwa mtu anayenuia kusimama
pweke? (al 5)
d) Andika arudhi za shairi hili (al 5)
e) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi hili
(al 6)

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
i) Muhisani
ii) Migati
iii) Vishindo
iv) Kweleza
v) Mizani

USHAIRI WA 8
Soma shairi lifuatalo na kisha ujibu maswali yafuatayo.

UKUBWA JAA
Dunia yetu dunia, watu wanakufitini,
Dunia huna udhia, watu wanakulaani,
Dunia huna hatia, wabebeshwa kila zani,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Dunia umenyamaza, umetua kwa makini,


Dunia vitu mejaza, watu wanataka nini?
Dunia wanakucheza,binadamu maluuni,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Dunia mtu akose, hukutia mdomoni,


Dunia hebu waase, hao watu mafatani,
Dunia chuki mpuse, muipate afueni,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
Dunia una lawama, za uongo si yakini,
Dunia wanokusema, ni manjunju si razini,
Dunia huna hasama, waja ndio kisirani,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Dunia kuharibika, hayo amezusha nani?


Dunia watu humaka, hao wanokuhini,
Dunia umejazika, kila tunu ya thamani,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Dunia unatukisha, bwerere bila undani,


Dunia unatukosha, maji tele baharini,
Dunia unaotehsa, mimea tosha shambani,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Dunia hujageuka, tangu umbwe na manani


Dunia watu ndo, nyoka, mahaini na wahuni
Dunia una baraka, mwenye pupa hazioni
Dunia huna ubaya, wabaya ni insani.

Maswali:

(a) Shairi hili ni la bahari gani? Toa sababu yako. (alama 3)


(b) (i) Kichwa cha shairi hili kinaoanaje na maudhui ya shairi?. (alama 2)
(ii) Andika methali moja inayoeleza maudhui ya shairi hili. (alama 3)
(c)Eleza sifa tatu za wanadamu kama anavyoeleza mshairi.(alama 3)
Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
(d)Kwa kutoa mifano kutokana na shairi hili, eleza mbinu tatu za lugha
alizotumiamshairi. (alama 6)
(e) Eleza maana ya vifungu vifuatavyo vya maneno kama vilivyotumika katika
shairi.
(i) bwerere bila undani
(ii) hao watu mafatani
(iii) afueni
(iv) insani (alama 4)

USHAIRI WA 9
1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Jama, Jama, Jamani
Mbona twabebeshwa mateso hivi
Mizigo mikubwa ya dhiki kama
Kwamba hatuna haki ya kusema
Kukataa ndoa za lazima
Kukataa kuozwa wazee
Kukataa kukatishwa masomo
Kukataa tohara ya lazima

Jama, Jama Jamani


Iweje tuteswe mateso haya
Na watu wasio kuwa hata na haya kama
Kwamba hatuna haki ya kulalamika
Kulalamikia kutumikishwa kama mayaya
Kulalamikia kudhalilishwa kiunyama
Kulalamikia kutolindwa na sheria
Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Jama, Jama, Jamani


Sasa hii ni awamu nyingine
Na macho tumeyafungua kabisa
Tumekataa kudhalilishwa kabisa
Tumekataa kuteswa kama watumwa
Tumekataa tohara ya lazima
Tumekataa kuozwa....... Tumekataa! Tumekataa
Hii awamu ya ’Haki ya mtoto wa kike’

Maswali
a) Taja mambo matatu muhimu yaliyozungumzwa na mshairi kisha ueleze
kila moja. (Alama 6)
b) Eleza muundo wa shairi hili (Alama 4)
c) Taja mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi kisha ueleze kila
moja(Alama 4)
d) Kwa nini mshairi huyu anasema hii ni ’awamu’ nyingine?
(Alama 3)
e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa na mshairi
(alama 3)
(i) awamu
(ii) kudhalilishwa
(iii) Dhiki

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 10
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo
1. Mkata ni mkatika, harithi hatoridhiwa
Sina ninalolishika, wala ninalochukuwa
Mlimwengu kanipoka, hata tone la muruwa!
Mrithi nini wanangu?

2. Sina ngo’mbe sina mbuzi, sina konde sina buwa


Sina hata makaazi, mupasayo kuyajuwa
Sina mazuri makuzi, jinsi nilivyoachwa
Mrithi nini wanangu?

3. Sina kazi sina bazi, ila wingi wa shakawa


Sina chembe ya majazi, mno nikukamuliwa
Nakwa’cheni upagazi, ngumu kwenu ku’tuwa
Mrithi nini wanangu?

4. Sina sikuachi jina, mkata hatasifiwa


Hata nifanye la mana, mno mi kulaumiwa
Poleni wangu sana, sana kwenu cha kutowa
Mrithi nini wanangu?

5. Sina leo sina jana, sina kesho kutwaliwa


Sina zizi sina shina, wala tawi kuchipuwa
Sina wanangu mi sina , sana la kuacha kuraduwa
Mrithi nini wanangu?

6. Sina utu sina haki, mila yangu meuliwa


Nyuma yangu ili dhiki, na mbele imekaliwa
N’nawana na miliki, hadi nitakapofukiwa
Mrithi nini wanangu?

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
7. Sina ila kesho kwenu, wenyewe kuiongowa
Muwane kwa nyinyi mbinu, mwende pasi kupumuwa
Leo siyo kesho yenu, kama mutajikamuwa
Mrithi nini wananngu?

(a)Taja mambo yoyote mawili ambayo mtunzi angewarithisha


wanawe. (alama 2)
(b) Eleza sababu ya mtunzi kutoweza kuwarithisha wanawe.
(alama 3)
(c) Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 4)
(d) Dondoa mifano miwili miwili ya : (alama 2)
(i) Inkisari
(ii) Tabdila
(e)Chambua shairi hili kwa upande wa :
(i) Dhamira (alama 2)
(ii) Muundo (alama 4)

(f) Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kama vilivyotumiwa katika


shairi. (alama 3)
(i) Mlimwengu kanipoka
(ii) Sina konde sina buwa.
(iii) Wingi wa shakawa.

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 11
Soma shairi hili kisha ujibu maswali.

Jicho, tavumiliaje, kwa hayo uyaonayo?


Kicho, utasubirije, maonevu yapitayo
Kwacho, lijalo na lije, nimechoka vumiliyo
Naandika!

Moyo, unao timbuko, maudhi tuyasikiayo


Nayo, visa na mauko, wanyonge wayakutayo
Kwayo, sina zuiliko, natoa niyahisiyo
Naandika!

Hawa, wanotulimiya, dhiki wavumiliayo


Hawa, mamiya mamiya, na mali wazalishayo
Hawa, ndo wanaoumiya, na maafa wakutayo
Naandika!

Hawa, sioni wengine, kwao liko angamiyo


Hawa, uwapa unene, watukufu wenye nayo
Hawa, bado ni wavune, kwa shida waikutayo
Naandika!

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
Bado, wawapo mabwana, wenye pupa na kamiyo
Bado, tafauti sana, kwa pato na mengineyo
Bado, tuling’owe shina, ulaji pia na choyo
Naandika!

Maswali
(a)Shairi hili laweza kuwekwa katika bahari zipi? (alama 4)
Thibitisha kila jibu lako.
(b) Eleza dhamira ya mshairi. (alama 2)
(c)Onyesha mifano miwili ya uhuru wa kishairi jinsi ulivyotumika katika
shairi. (alama 2)
(d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)
(e)Tambulisha kwa mifano mbinu zozote mbili za sanaa katika shairi.
(alama2)
(f) Fafanua sifa za kiarudhi zilizotumika katika ubeti wa tano. (alama 3)
(g) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi.
(alama 3)
(i) Zuiliko
(ii) Wavune
(iii) Wenye pupa na Kamiyo.

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

SHAIRI LA 12
Soma shairi hili kisha ujibu mawali yanayofuata.
SABUNI YA ROHO
Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
Ndiwe suluhu la zama, waja wakukimbilia,
Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,


Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Matajiri wakujua, wema wako wameonja,


Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
Sura Zao ‘mefufua, Wanazuru kila nyanja,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Ndiwe mvunja mlima, onana na masikini


Watazame mayatima, kwao kumekua wa duni
Wabebe waliokwama, wainue walio chini,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Ndiwe mvunja mlima,wapi kapata uwezo?


Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
Ndiwe chanzo cha zahama, umewaitia vikwazo,
Ndiwe sabuni ya roho, Ndiwe mvunja mlima.

Umevunja usuhuba, familia zazozana,


Walokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
Niondoe jehanamu, ya ufukara wa sumu,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika


Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

(a) Mshairi anaongea na nani katika shairi hili? [alama 1]


(b) Taja majina mengine matatu aliyopewa huyu anayesemeshwa.
[alama 3]
(c) Anayezungumziwa katika shairi hili amesababisha balaa gani?
[alama 2]
(d) Mshairi anatoa mwito gani kwa mwenziwe? [alama 4]
(e) Fafanua maudhui ya ubeti wa sita. [alama 2]

(f) Mbinu kadha za uandishi zimetumiwa na msanii kuwasilisha


ujumbe wake. Taja mbinu zozote tatu na uzitolee mifano
katika shairi. [alama 3]

(g) Fafanua maana ya:


Sura zao “mefufua, wanazuru kila nyanja. [alama 1]
(h) Andika ubeti wa saba katika lugha nathari. [ alama 4]

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 13
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
1. Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

2. Dunia ingetatana, na kizazi katikati,


Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,
Vipi tungeliona, na kuzaa hatuwati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

3. Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,


Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,
Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

4. Walakini subuhana, kapanga sisi na miti,


Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti,
Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
5. Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,
Kwa uwezewe Rabana, kaipanga madhubuti,
Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

6. Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati ,


Sote tungeambatana, pa kulima hatupati,
Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

7. Peleleza utaona, hayataki utafiti,


Kama tungelikongana , ingelikuwa ni bahati,
Vipi tungelisukumana, katika hiyo hayati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

8. Mbele sitakwenda tena, hapa mwisho nasukuti,


Yaeleni waungwana, shauri yake jabaruti,
Yote tuloelezana, katenda bila senti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
MASWALI
a) Shairi hili ni la bahari gani? (alama 2)

b) kwa kutoa mifano mwafaka onyesha jinsi mtunzi wa shairi hili


alivyotumia uhuru wa utunzi (alama 2)
c) Eleza muundo wa shairi hili (alama 4)
c) Andika ubeti wa tano katika lugha nathari. (alama 4)
d) Tambulisha mbinu zozote mbili za lugha zilizotumiwa na mshairi(alm4)
e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi
i)katiti
ii) yakuti
iii) Hatuwati
iv) Nasukuti (alama 4)

USHAIRI WA 14
KIFO
1. ‘likuwa tisini moja 2. ‘lituachia vioja
‘lipojikunja pamoja Raha hatujaionja
Kutuaga mara moja Tumezidi na kungoja
Safari moja kwa moja Matumaini ya waja.

3. Kifo hatuna faraja 4. Maisha ‘mekosa haja


Baba livuka daraja Na mama amejikunja
‘likuwa wetu kiranja katwa auma viganja
Majonzi ‘lituachia Nyumba sasa inavuja
Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

5. Vitamu nani taonja 6. Kifo kwetu sisi waja


Mali sasa imefuja Tumaini hutuvunja
Mifupa tutaivunja Ingawa ndio daraja
Mifugo katu uwanja Haituweki pamoja

MASWALI
1. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
2. Mshairi ana ujumbe gani ? (alama 2)
3. Taja mbinu zozote tatu za lugha alizotumia mshairi na uzitolee mifano
kutoka shairi.(alama 6)
4. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4)
5. Eleza maana ya mistari hii kama ilivyotumika katika shairi. (alama 2)
i) Baba livuka daraja
ii) Kutwa auma viganja
6. i) Mshairi ametumia mbinu gani katika maneno haya . (alama 1)
‘likuwa
‘lituachia
‘lipojikunja
ii) Kwa nini akatumia mbinu hiyo? (alama 1)

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 15
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yote.

KIPIMO NI KIPI?
Nitampa nani, sauti yangu ya dhati
Kwa kipimo gani, ingawa kiwe katiti
Amefanya nini, La kutetea umati
Kipimo ni kipi?

Yupi wa maani, asosita katikati


Alo na maoni, yasojua gatigati
Atazame chini, kwa kile ule wakati
Kipimo ni kipi?

Alo mzalendo, atambuaye shuruti


Asiye mafundo, asojua mangiriti
Anoshika pendo, hata katika mauti
Kipimo ni kipi?

Kipimo ni kipi, changu mimi kudhibiti


Utu uko wapi, ni wapi unapoketi
Nije kwa mkwapi, au ndani kwa buheti
Kipimo ni kipi?

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]
(a)Eleza umbo la shairi hili Alama 4
(b) Taja tamadhaliza usemi na kisha utoe mifano Alama 3
(c)Taja na ueleze namna mshairi alivyotumia uhuru wa ushairi? Alama 2
(d) Eleza maudhui ya shairi hili? Alama 3
(e)Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari Alama 4
(f) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa Alama 4
(i) Katiti
(ii) Gatigati
(iii) Shuruti
(iv) Mangiriti

USHAIRI WA 16

Vita vya ndimi

Huyo! Amshike huyo! Yu imara mmoja wao.


Hakuna bunduki wala kifaru Akirusha kombora la neno zito!
Bomu na risasi hata hawazijui! Limtingishe adui wake
Lakini mno wanashambuliana. Na kumgusa hisia kwa pigo kuu.
Kwa ndimi zilizonolewa kwa Pigo linalopenya moyoni kama
makali kichomi
Vipande vya matusi silaha zao. Kuchipuza joto la hasira na kisasi
Katika mapigano yaso na kikomo.
Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Filimbi ya suluhu inapulizwa


kuwaamua!
Ni nani anayekubali suluhu?
Roho zinakataa katakata
Huku ukaidi ukinyemelea na
kutawala kote
Mapandikizi ya watu yakipigana
Vitu shadidi visivyo ukomo
Vita vya ndimi!

Magharibi sasa
Jua linapungia mkono machweo
Nalo giza likinyemelea kwa kiburi
na kasi
Sisikii tena sauti za misonyo
Mate ya watesi yamekauka

Makanwa yao yamelemewa na


uchovu
Sasa wameshikana mikono
Nyuso zao zikitabasamu
Ishara ya suluhu!

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

(a) Hili ni shairi la aina gani? (alama 1)


(b) Eleza sifa za utunzi alizotumia mshairi. (alama 4)
(c) Taja kwa kutolea mifano tamathali za usemi zozote tatu zilizotumiwa
katika shairi hili.(alama 3)
(d) Fafanua mishororo hii:
(i) Akirusha kombora la neno zito!
(ii) Makanwa yao yamelemewa na uchovu (alama 4)
(e) Zungumzia mgogoro katika shairi na namna unavyomalizika.
(alama 6)
(f) Toa maana ya msamiati huu
(i) Kichomi
(ii) Misonyo
(alama2)

USHAIRI WA 17
Soma mashairi ya A na B kisha ujibu maswali.
A
Mtu ni afya yake, ndio uzima wa mtu
Mtu ni kuwa na chake, hakuwi ela kwa kitu
Mtu ni bahati yake, kupendekeza kwa watu
Mtu si fakhari kwako, kuitwa nyama ya mwitu

Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Mtu ni ulimi wake, kunena vyema na watu


Mtu ni kijungu chake, kuweka mawe matatu
Mtu ni mwenda kwa lake., mtoshawa na kula kitu
Mtu si uzuri kwake, kuitwa nyama wa mwitu

Mtu ni mwenye nadhari, apimaye kula kitu


Mtu ni moyo hariri, mwenye imani na watu
Mtu ni alo na ari, shika sana mwana kwetu
Mtu si yake fakhari, kuitwa nyama wa mwitu

Mtu ni mkono wazi, mtasadaku na watu


Mtu ni mwenye maozi, kuoneya kula kitu
Mtu ni alo tulizo, asopenda utukutu
Mtu si jambo pendezi, kuitwa nyama wa mwitu

Mtu ni mwenye ahadi, ndio u’ngwana na utu


Mtu ni alo baridi, mbembeleza wa watu
Mtu ni moyo asadi, asoonewa na mtu
Mtu si yake ifadi, kuitwa nyama wa mwitu

Mtu niliyoyanena, pima sana ewe mtu


Mtu sikuja tukan, kukirihi nyoyo watu
Mtu nakupa maana, wende nyendo za kiutu
Mtu si uzuri sana, kuitwa nyama wa mwitu
Mtu ni mtenda njema, atwiiye Mola wetu
Mtu ni mbele na nyuma, pima sana mwana kwetu
Mtu natiye khatima, fafanua kula kitu
Mtu si yake hisima, kuitwa nyama wa mwitu.

Page | 35
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

B
MTU HACHAGUI KAZI
Naamba kazi ni kazi, vyovyote vile iwavyo
Madamu si ubazazi, kwa mwanaadamu ndivyo
Kushona na upagazi, pia vile vyenginevyo
Kazi ni kitu azizi, wala vyenginevyo sivyo
Mtu hachagui kazi.

Mtu hadharau kazi, ile ahisiyo duni


Ayuzuie machozi, walilia jambo gani
Ukulima na ukwezi, na uvuvi baharini
Hizi nazo njema kazi, yafaa uzibaini
Mtu hachagui kazi

Si laiki kubughudhi, hakuna iliyo duni


Hayo makubwa maradhi, na tena uhayawani
Kazi zote zina hadhi, hivyo tusibagueni
Inafaa tuziridhi, tuzitende kwa yakini
Mtu hachagui kazi.

Ni wajibu kuipenda, na kuikiri moyoni


Na kwa dhati kuitenda, kwa juhudi na makini
Matatizo huyashinda, na uvivu kuuhuni
Hapo mtu atashinda, na magumu kumhuni
Mtu hachagui kazi

Page | 36
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

MASWALI
(a)Lipe shairi la A kichwa mwafaka. (alama 1)
(b) Kwa mifano mwafaka fafanua bahari katika shairi la A na B.
(alama 4)
(c)Toa sababu za mwandishi kuchagua “Mtu hachagua kazi” kama
kichwa cha shairi la B. (alama 1)
(d) Mtunzi alikuwa na ujumbe gani katika mashairi haya? (alama 4)
(e)Andika ubeti wa pili wa shairi A katika lugha nathari. (alama 4)
(f) Eleza muundo wa shairi la B. (alama 4)
(g) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika
mashairi haya. (alama 2)
(i) Nadhari
(ii) Ubazazi
USHAIRI WA 18
Soma shairi lifuatalo kisha uiibu maswali

Duniani husifiki; Walifanya makubeli.


Wala hupati thamani, Wakaapa hadharani,
Yalisemwa hukumbuki? La uongo huwa kweli,
Na wazee wa zamani, " Kubishika kitaani,
"Mkono haurambiki, Na tangu kukosa mali,
Bila kitu kiganjani" Wakawa kama nyani!

Wangapi watu azizi, Walifanya mahashumu.


Fulani bin Fulani, Kuwaliko masultani,
Waliokichinja mbuzi, Ushekhe na Ualimu,
Kukirimu mitaani, Kufasiri vitabuni,
Sasa kama wapuuzi, Na leo wana wazimu,
Kwa hali kuwa ta'bani Kama si wanachuoni.

Page | 37
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Maswali
(a) Kwa maneno yako mwenyewe eleza ujumbe wa shairi hili.
(Alama 3)
(b) Eleza jinsi mshairi anavyosisitiza huo ujumbe katika shairi lote.
(Alama 4)
(c) Eleza kwa tafsili umbo la shairi hili. (Alama 5)
(d) Andika ubeti wa kwanza katika lugha nathari. (Alama 3)
(e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyo tumika katika shairi;
(i) Kiganjani.
(ii) Kukirimu.
(iii) Makubeli.
(iv) Mahashumu.
(v) Wanachuoni (Alama 5)

USHAIR1:
Soma shairi lifuatalo kisfea ujibu saaswali vanavofuata:
1.
Niliusiwa zamani, babu aliniusia,
N 3. Mtima ndio sukani,
ili bado utotoni, hapo waongoza'kila ndia,
aliponambia, Weka mkazo moyoni, kila
Babu yaweke kitwani, yasije unalofwatia,
yakapotea, Moyoni mwako amini, kuwa
Penye nia ipo njia, usikate utalifikia,
tumaini. Penye nia ipo njia, usikate
tumaini.
2. Wewe bado ni mgeni, katika
hii dunia, 4. Kama uko safarini ,
Mimi ndiye wa zamani, waongoza kila ndia,
mengi nimejionea, Bahari kuu kinani, mawimbi
Sasa niko uzeeni, uzee yakuchachia,
umewadia, Usikate tumaini. hapo ndipo
penye nia ipo njia, usikate penye ndia,
tumaini.
Page |
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Penye nia ipo njia, usikate


tumaini.

5. Hapo hapo mawimbini, wewe


hapo pigania,
Hapo ndipo milangoni,
mawimbi yakuzuia,
Mtima utie kani, bandarini
utangia,
Penye nia ipo njia, usikate
tumaini.

6. Na iwapo ni shuleni, masomo


yakutatia,
Usiasi masomoni, kusoma
ukakimbia,
Kidogodogo bongoni, elimu
itakungia,
Penye nia ipo njia, usikate
tumaini.

7. Kama wenda uchumini,


biashara waania.
Usihofu asilani, hasara
ikitukia,
Leo ukipata duni, na kesbo
litazidia,
Penye nia ipo njia, usikate
tumaini.

Page | 39
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

(a)Andika methaii ambayo ingetumiwa kujumuisha ujumbe katika


ubeti wa pili. (Alama 1)
(b) Kutokana na shairi hili, ni katika nyanja zipi za maisha
tunapopaswa kujikakamua? Tujikakamue vipi?
(alama 6)
(c)Taja arudhi ambazo zimetumiwa kuusarifu ubeti wa kwanza.
(Alama 4)
(d) Huku ukitoa mfano mmoja bainisha uhuru wa kishairi
ambao umetumiwa katika ubeti wa 3.(alama 1)
(e)Andika ubeti pili kwa lugha ya nathari. (Alama 4)
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika
shairi.
(i) Aliniusia.
(ii) Mtima.
(iii) Sukani
(iv) Waania. (Alama 4)

USHAIRI WA 19
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata
Kaka: Kusoma nilikosoma, kambiwa sipati kazi,
Yapata mwaka mzima, nategemea shangazi,
Wasiojuwa husema, ‘ sababu sina ujuzi,’
Huno uhaba wa kazi, mesababishwa ni wake.
Page | 40
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Dada: Mbona watuingilia, kaka acha ubaguzi,


Likukeralo twambia, tulijuwe waziwazi,
Au unalochukia ni wake kufanya kazi?
Mambo ya siku hizi,watu ni bega kwa bega.

Kaka: Siwangilie kwa nini, nanyi mwatukopa kazi


Kwani tokea zamani, hazikuwa shida hizi,
Mtu kitoka shuleni, kibaruwa si tatizi,
Leo hatupati kazi, kisa nyinyi wanawake

Dada: Hapo kaka hujasema, kuwa wake ndiyo chanzi,


Chanzo cha hii nakama, waume kukosa kazi,
Bure mwatupa lawama, wenyewe mna ajizi,
Mtindo wa siku hizi, watu ni bega kwa bega.

Kaka: Hayo unayotamka, yote niya upuuzi,


Mumetoroka kupika, kazi yenu toka enzi,
Bilashi mwahangaika, kushabihi vijakazi,
Sasa hatupati kazi, kisa nyinyi wanawake.

Dada; Mbona wafanya ukali, ishakuwa ni chukizi?


Hata na yangu kauli, umekuwa husikizi,
Nisemaye ni halali,ukweli uliowazi,
Mtindo wa siku hizi, watu ni bega kwa bega.

Page | 41
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Kaka: Yana uhalali gani, mbona basi huelezi?


Kipita maofisini, mumejaa kama inzi,
Mwataka tuwe mekoni, wala halitupendezi,
Na nje hakuna kazi, kisa nyinyi wanawake.

Dada: kakangu una matata, kuyaelewa siwezi,


Wasema unamopita, wambiwa hakuna kazi?
Na sisi wake twapata, haraka pasi ajizi,
Sababu siku hizi, watu ni bega kwa bega.

Kaka: Sisi kazi hatupati, wengi wetu ni mijizi,


Elanyi muna bahati, mabosi hawawaizi,
Hampotezi wakati, ni kidogo pingamizi,
Nasi hatupati kazi, kisa nyingi wanawake..

Dada: kakangu wanichekesha, hadi sina kizuizi,


Vipi lakukasirisha, sisi tukifanya kazi?
Hujui ndivyo maisha, yaendavyo siku hizi?
Mtindo wa siku hizi, watu ni bega kwa bega.

Kaka: Huna haja ya kucheka, nisemayo si upuzi,


Kazi inayojulika, yenu ni kukuna nazi,
Kisha mwenda zianika, mukaziuze takizi,
Leo hatupati kazi, kisa nyinyi wanawake.

Page | 42
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Dada: Yalikuwa ni ya kale, kuuza chicha za nazi,


Ela leo twenda mbele, na nyuma hatujibanzi,
Hakuna aliyelele, kushiriki usingizi,
Kwani mambo siku hizi, watu ni bega kwa bega.

Kaka: kulla kitu mwakitaka, kiwe chenu siku hizi,


Ishakuwa na miaka, pia mwataka ihozi,
Nasikia mwatamka, mwaka huno wa ledizi,
Mwisho mutataka myezi, iwe yenu wanawake.

Hai mana kubishana, nikashabihi mkizi,


Mengi niliyoyanena, yafanyie uchunguzi,
Iwapo tutafanana, yupi taleya vizazi?
Sisi hatupati kazi, hadi murudi mekoni.

Dada: Baba mbele mama nyuma, yamekuwa simulizi,


Muradi sote twasoma, soteni tuwe walezi,
Wake haturudi nyuma, tunataka mapinduzi,
Maisha ya siku hizi, watu ni bega kwa bega.

Page | 43
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

MASWALI
a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (Alama 2)
b)Dada anatoa sababu gani ya wanawake kuajiriwa maofisini?
(Alama2)
c) Kaka anataja sababu zipi za wanaume kukosa kuajiriwa kazi?
(Alama2)
d) Eleza umbo la shairi hili (Alama3)
e)Dondoa na ueleze mifano miwili tofauti ya uhuru wa kishairi katika
shairi(Alama4)
f) Kwa mujibu wa shairi hili, kazi za wanawake ni zipi?
(Alama2)
g) Eleza ubeti wa mwisho kwa maneno yako mwenyewe (Alama2)
h) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi.
(Alama3)
(i) Kulla
(ii) Nakama
(iii) Ajizi
USHAIRI WA 20
Soma shairi hili kasha ujibu maswali.
1. Pasi kuhofu lawama, imenibidi kunena,

Nina mengi ya kusema, ambayo ni ya maana


Kwetu sote ni lazima, viumbe kuambizana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.

Page | 44
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

2. Sahau I akilini, yataka kukumbushana,


Madamu tu duniani, la kosa huelezana,
Ili tuwe hadharini, tujilinde na fitina,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema

3. Uchochezi ukitiwa, uwongo unapofana,


Lolote laweza kuwa, hata watu kupigana,
Fitina yaweza ua, binadamu wengi sana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.

4. Fatani anapojua, jamii yasikizana,


Aweza leta adawa, ya fitina kugombana,
Hata akawa baguwa, ndugu wakafarikana,
Yashinda kifo fitina, fatani si ntu mwema.

5. Nahakikisha wenzangu, fitina ina laana,


Fitina kwa Bwana Mungu, katu hataki iona,
Yasaliti walimwengu, mume mke kuachana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.

Page | 45
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

6. Fitina si kitu safi, nazidi toa bayana,


Fitina ina makofi, muda ukijulikana,
Fitina ni ukorofi, mfano wake hapana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.

7. Fitina yashinda tusi, uovu wa kutukana,


Fitina ina maasi, madhambi ya kujazana,
Fitina ina utesi, tena usowezekana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema

8. Fitina si masihara, yashinda hata khiana,


Fitina ina madhara, nchi zaweza gongana,
Fitina aina izara, na aibu nyingi sana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.

9. Fitina haina shaka, ni mbovu nasema tena,


Fitina mali hakika, ya ghibu nawe waona,
Fitina ina mashaka, na dhiki kila namna,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.

10. fitina kitu haramu, tamati zaidi sina,


Fitina na binadamu, wawe wakichukiana,
Fitina ni mbaya sumu, ya au sifa na jina,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu, mwema.

Page | 46
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Maswali:
(a) Bainisha athari tano za fitina kulingana na mshairi (alama 5)
(b) Ubeti wa sita umechukua mikondo na bahari tofauti tofauti.
Zitaje na utoe mifano (alama 4)
(c) Andika ubeti wa nne kwa lugha ya nathari (kawaida) (alama 3)
(d) Mshairi ametumia mbinu zipi kufanya jumbe zake zieleweke
kwa bayana zaidi. (alama 4)
(e) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika
shairi.
(i) Adawa
(ii) Fatana
(iii) Wakafarikana
(iv) Tusi (alama 4)

Soma shairi hili kisha ujibi maswali yanayofuata.

1. Tusitake kusimama, bila kwanza kusimama,


Au dede kuwa hima, kabla hatujakaa,
Tutakapo kuchutama, kuinama inafaa,
Tujihimu kujinyima, makubwa kutoyavaa.

Page | 47
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

2. Tusitake kuenenda, guu lisipokomaa,


Tujizonge na mikanda, inapochagiza njaa,
Na mazuri tukipenda, ni lazima kuyandaa,
Tujiase kujipinda, kujepusha na balaa.

3. Tusitake uvulana, au sifa kuzagaa,


Tushikaye nyonga sana, tunuiyapo kupaa,
Kama uweza hapana, tutoelee dagaa,
Tujiase hicho kina, maji yajapokujaa.

4. Tusitake vya wenzetu, walochuma kwa hadaa,


Wanaofyatua vitu, na kasha vikasambaa,
Uwezo hatuna katu, umaskini fazaa,
Tujihimu kula vyetu, siendekeze tamaa.

5. Mtaka kuiga watu, kufata kubwa rubaa,


Vyao vijaile kwetu, vifaa vingi vifaa,
Tunamezwa na machatu, tusibakishwe dhiraa,
Tujihimu kilo chetu, hata kama twapagaa.

(a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 1)


(b) Eleza madhumuni ya shairi hili (alama 2)

Page | 48
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

(c) shairi hili ni bahari gani? Toa sababu. (alama 4)


(d) Bainisha umbo katika ubeti wa kwanza na wa mwisho
ukizingatia vina na mizani. (alama 4)
(e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nathari. (alama 4)
(f) Taja mbinu moja ya kisanii inayoibuka katika ubeti wa nne.
Kwa nini imetumiwa? (alama 2)
(g) Eleza msamiati ufuatao kama unavyotokea katika shairi.
(alama 3)
(i) Kuiga
(ii) Dede
(iii) Tujizonge.

USHAIRI WA 21
Alipokwenda kwao, mamaye alimwambia

Nipa fedha au nguo, nataka kwenda tumia!

Nikosapo hivi leo, nipa kisu tajitia !

Huzunguka akilia kwa maana ya uketo.

Ndipo mamaye kawaza, pamwe na kuzingatia,

Fedha zako umesoza, na leo zimekwisha,

Kisu sikukukataza, twaa upate jitia!

Mbele zangu n’ondokea! Wende na ukiwa wako!

Page | 49
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Ulipogeuka nondo, nguo ukazingilia,

Kakaka kwa vishindo, usisaze hata moya,

Leo wanuka uvundo, wambeja wakukimbia!

Mbele zangu n’ondokea! Wende na ukiwa wako.

Ukijigeuza nyama, kama Simba ukilia,

Watumwa ukawaegema, ukawala wote pia,

Pasi kuona huruma, kutoa wahurumia,

Mbona hukuzingatia? Wende na ukiwa wako!

Si mimi naliokupa, ukata huo sikia !

Kwamba utakuja hapa, nipate kuondolea,

Naapa thama, naapa, sina la kukutendea!

Mbele zangu n’ondokea ! Wende na ukiwa wako !

Tamati nalikomile, ni hayo nalokwambia,

Hapahitaji kelele na kujirisha mabaya

Na kwamba yakutukie, sema yapate n’elea !

Zidi radhi kuniwea ! wende na ukiwa wako !

Page | 50
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Maswali

(a) Lipe shairi hili anwani mwafaka. (alama 2)

(b) Ni maudui gani yanayojitokeza katika shairi hili.(alama 4)

(c) Taja na ueleze tabia za mnenewa katika shairi hili.(alama 4)

(d) Mshairi ametumia uhuru wa utunzi. Taja sehemu mbili


alikotumia uhuru huo. (alama 4)

(e) Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)

(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa


katika shairi :- (alama 2)

(i) Uketo

(ii) Ukata

USHAIRI WA 22
Vile walalama, kwa yale ulotendwa,
Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachwa,
Ulipotenda unyama, uliona ndio sawa
Mtenda akitendwa, hulalama kaonewa.

Ulizusha uhasma, leo wewe wapagawa,


Walia bila kukoma, tungedhani umefiwa,
Sasa huna usalama, huwezi kujiopowa!
Mtenda akitendwa, hulalama kaonewa.

Page | 51
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Tenda mambo kwa kupima, usiinuke huna bwawa,


Una macho kutazama, na akili umepewa,
Matendo hurudi nyuma, atendaye hurudiwa,
Mtenda akitendwa, hulalama kaonewa.

Dunia haishi njama, sijione umepewa,


Ukadhani u salama, binadamu kupagawa,
Ukahisi ni wanyama, waso hali kama ngawa,
Mtenda alitendwa, hulalama kaonewa.

Unapotenda zahama, siku yako ikakuwa,


Ambapo utaungwama, useme umechachiwa,
Na uanze kutetema, ulie umeonewa,
Mtenda akitendwa, hulalama kaonewa.
Maswali

(a) Lipe kichwa shairi hili. (alama 2)

(b) Hili ni shairi la aina gani. (alama 2)

(c ) Eleza muundo wa ubeti wa pili. (alama 4)

(d) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nathari. (alama 4)

(e) Toa mifano miwili ya inkisari na uindeleze inavyofaa. (alama 4)

(f) Ni kaida zipi zilizotumiwa na mwandishi wa shairi hili. (alama 2)

(g) Eleza maana ya (alama 2)

Page | 52
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

(i) Uhasama

(ii) Umepowa

USHAIRI WA 23
Soma shairi lifuatalo kwa makini,halafu ujibu maswali yanayofuatia.

Hakika yamekithiri, ni nani asoyajua?


Wazazi wayahubiri,na hivyo kutubagua
Hayana komwe fahari,ila kweli yatua.
Uhuru wa kuoana,ni lini tutaupata?

Mwanamke siyo huyo? baba mtu anasema


Mwanamke kwani huyo? anateta naye mama,
Sababu waitoayo, haina nguvu wima,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutampata?

Kabila letu nihili,sharuti uoe huko,


Unazomewa ukali,kuoa nje ni mwiko
Hivyo twafanywa dhalili,viumbe tuso mashiko
Uhuru wa kuoana ,ni lini tutaupata.

Wanachunguza tabaka,ndipo wazushe wahaka


Wauliza kwa haraka,wajue lake tabaka,
Wasioridhika wafika,arudi alikotoka,
Uhuru wa kuona, ni lini tutaupata?

Page | 53
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Waichuja yake dini,ndo ndoa ibarikiwe


Lazima yake imani,iwe sawa na yakuwe
Huu kweli ni uhuru,wataka uondolewe,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Japo mwanipa elimu,uhuru ninautaka,


Na mie muniheshimu,nipate nilomtaka
Kuoa kitu adhimu, so mchezo kwa hakika
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Nawashauri wazazi,twahitaji kupumua,


Wawili ndo waamuzi , hata Mungu anajua,
Wasifu pasi ajizi, kwa yao njema hatua,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Ndoa ikivunjikana,wawili wajisakeni,


Isije kusemekana,wazazi ndio kiini,
Ndiposa hata Rabana,situtie lawamani,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Aliye na masikio,mesikia kwa makini,


Tusitamani kilio,mithili tulo vitani,
Wakioa sema ndio. Mola asikulaani
Uhuru wa kuoana ni lini tataupata?

Page | 54
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Maswali.
a) Lipe shiari hili anwani mwafaka. (ala.1)
b) Shairi hili laweza kuwekwa katika bahari mbili.Zitaje huku ukitoa
sababu ( ala.4)
c) Mtunzi alikuwa na lengo gani alipolitunga shairi hili?
d) Ni masharti gani kijana nafaa kuyatimiza kabla ya and oa na
ambazo mshairi analalamikia Taja manne. (ala.4)
e) Vijana wanafaa kuchaguliwa mke/mume wa kuoa? Toa maoni
yako. (ala.2)
f) Ukizingatia shairi ulilopewa eleza jinsi mtunzi alivyotumia uhuru
wake. (ala.4)
g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika shairi.
(ala. 3)
(i) Wahaka
(ii) Yamekithiri
(iii) Dhalili.

USHAIRI WA 24
Soma shairi ulilopewa kwa makini kisha ujibu maswali

Ah! siambile ovyo, sambi ah! Kupuuzwa


Ah! hii niambavyo, si kwamba nimependezwa
Ah! moyo wamba hivyo, kwayo niliyofanyizwa
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.

Page | 55
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Ah! si mimi nilivyo, mawazo yametatizwa


Ah! tata za magovyo, fikira zimeshangazwa
Ah! naviwe viwavyo, sioni pa kutulizwa
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.

Ah! sililii yavyo, kwa kutaka kunyamazwa


Ah! sipendezwi navyo, sipendezewi kebezwa
Ah! ni hivi ambavyo, mkata heshi kutezwa?
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.

Ah! kukicha ya vivyo, na uchao yajalizwa


Ah! havishi viishavyo, na matayo kuambizwa
Ah! sivyo hivi sivyo, vyakanywa na kukatazwa
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.

Ah! lau hata ndivyo, basi hata kulekezwa


Ah! wayatenda kwayo, kwamba ndiko kutukuzwa
Ah! tenda utendavyo, ni kuwa watendekezwa
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.

Ah! ni vile wambwavyo, togo upate tangazwa


Ah! kila upendwavyo, mwisho ‘we utatukizwa
Ah! pendo lianzwavyo, sivyo vya kuishilizwa
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.

Page | 56
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Ah! kila lenye govyo, halikawii kuvizwa


Ah! nalende lendavyo, ukomo litagotezwa
Ah! ni vipi kulivyo, kukadumu kutulizwa?
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.

Ah! dunia ni kyovyo,kizamacho chaibuzwa


Ah! ni mangapi ja’vyo, hayako metokomezwa
Ah! jaa lijaavyo, mwishilio lapunguzwa
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.

Ah! kaa ukaavyo, hatimayo yasogezwa


Ah! nauwe uwavyo, atendae hulipizwa
Ah! hakuna lilivyo, gumu lisilolegezwa
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.

Maswali
(a) Taja mambo matatu ambayo mshairi analalamikia (ala.3)
(b) Kwa nini anayezungumziwa anatenda ayatendayo. (ala..3)
(c) Taja na kueleza tamathali zozote tatu zilizotumiwa na
mshairi. (ala.6)
(d) Huku ukitoa mifano kutoka shairi, eleza matumizi yoyote
mawili ya uhuru wa ushairi. (ala.2)
(e) Andika ubeti wa kwanza katika lugha ya nadharia. (ala.4)

Page | 57
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa


kwenye shairi. (ala. 2)
(i)watendekezwa
(ii) togo

USHAIRI WA 25
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.

DUNIANI husifiki
Wala hupati
Yalisemwa hukumbiki?
Na wazee wa zamani
“Mkono haurambiki
Bila kitu kiganjani.

Wangapi watu azizi,


Fulani bin Fulani,
Waliokichinja mbuzi,
Kukirimu mitaani,
Sasa kama wapuuzi
Kwa hali kuwa ta’bani

Page | 58
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Walifanya makubeli,
Wakaapo hadharani
La uongo huwa kweli,
Kubishika kitaani,
Na tangu kukosa mali,
Wamekuwa kama nyani!

Walifanya mahashumu,
Kuwaliko masultani,
Ushehe na ualimu,
Kufasiri vitabuni
Na leo wana wazimu,
Kama si wanachuoni.

MASWALI
(i) Eleza ujumbe wa mshairi (Alama 1)
(ii) Onyesha jinsi mshairi alivyousisitiza ujumbe katika shairi.
(Alama 3)
(iii) Eleza kwa tafsili umbo la shairi. (Alama 4)
(iv) Andika ubeti wa kwanza katika lugha ya nathari. (Alama 3)
(v) Onyesha idhini ya kishairi ilivyotumika katika shairi kwa
kutolea mifano. (Alama 4)
(v) Toa mifano ya mbinu za lugha zilizotumiwa katika shairi.
(Alama 2)

Page | 59
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

(vi) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika


katika shairi.
(a) Kukirimu
(b) Makubeli
(c) Mahashumu (Alama 3)

USHAIRI WA 26

Soma shairi ulilopewa kwa makini kisha ujibu maswali


Pindi ilipomjia,khabari za binti kazaliwa,
uso ulimsawijika kwa soni akachanganyikiwa.
“Hii ni nukhusi?
Aka, ni nakama!
La, ni beluwa?”
Bali si beluwa?”
Wapi uso aufiche?
Au mchangani auzike?
Izara hii asiipate1
Ya kuzaliwa ‘mke.
Nitawatolea kis…
Nawatangulizia sasa,
Kisa kilichoanza,
Kinachoendelea hasa,

Page | 60
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Hakijawahi kukoma,
Baharini wa bara,
Kote kimeenea
Namna wanavyomtesa,
Kiumbe dhahili wamenanys,
Lini atathaminiwa?
Kisa chenyewe kitendawili,
Mwenye busara atoe taawili,
Ya haya mambo mwawili,
Maisha bila ‘mke ni awali,
Kisa kingeendelea?
Lulu iliyohifadhiwa ni la pili
Kisa kingeendelea?

Maswali
a) (i) Lipe anwani shairi hili. (ala.1)
(ii) Mshairi ana ujumbe gani katika shairi hili? (ala. 3)
b) (i) Balagha ni nini? ( ala.1)
(ii) Kwa nini mshairi ametumia sana m,binu hii ya balagha
katika shairi hili? ( ala.2)
c) Hili ni sahiri la aina gani? ( ala. 2)
d) Fafanua umbo la shairi hili ukizingatyia. (ala. 8)
i) Ubeti
ii) Mishororo
iii) Mizani

Page | 61
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

iv) Vina
e) Eleza maana ya maneno haya kama ya livyotumiwa aktika shairi.
(ala. 3)
i) Kisa
ii) Baharini wala bara
iii) Atahta miniwa.

USHAIRI WA 27

Soma shairi kisha ujibu maswali;


Vile walalama, kwa yale ulotendwa,
Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachwa,
Ulipotenda unyama, uliona ndio sawa
Mtenda akitendwa, hulalama kaonewa.

Ulizusha uhasma, leo wewe wapagawa,


Walia bila kukoma, tungedhani umefiwa,
Sasa huna usalama, huwezi kujiopowa!
Mtenda akitendwa, hulalama kaonewa.

Tenda mambo kwa kupima, usiinuke huna bwawa,


Una macho kutazama, na akili umepewa,
Matendo hurudi nyuma, atendaye hurudiwa,
Mtenda akitendwa, hulalama kaonewa.

Page | 62
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Dunia haishi njama, sijione umepewa,


Ukadhani u salama, binadamu kupagawa,
Ukahisi ni wanyama, waso hali kama ngawa,
Mtenda alitendwa, hulalama kaonewa.

Unapotenda zahama, siku yako ikakuwa,


Ambapo utaungwama, useme umechachiwa,
Na uanze kutetema, ulie umeonewa,
Mtenda akitendwa, hulalama kaonewa.

Maswali.
(a) Lipe kichwa shairi hili. ( alama 2 )
(b) Hili ni shairi la aina gani. ( alama 2 )
(c ) Eleza muundo wa ubeti wa pili. ( alama 4 )
(d) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nathari. ( alama 4 )
(e) Toa mifano miwili ya inkisari na uindeleze inavyofaa.
( alama 4 )
(f) Ni kaida zipi zilizotumiwa na mwandishi wa shairi hili. ( alama 2 )
(g) Eleza maana ya (alama 2 )
(i) Uhasama

(ii) Umepowa

Page | 63
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 28
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
1. Sina ni kukosekana, si kuwa ni ubahili,
Watu hutarajiana, kupana zao fadhili,
Kiwapo chapatikana, chenye kuzidi shughuli,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.

2. Iwapo mwenzio hana, cha ziada kukujali,


Ndipo anenapo sina, kukuafu yako hali,
Usidhani ni hiyana, chake kuwa hakubali,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.

3. Yapasa kukumbukana, tuishipo mbali mbali,


Kila mtu jambo yuna, limtialo thakili,
Akawa ni mwenye dhana,la kesho kulikabili,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.

4. Na pindi anapoona, tarehe mno i mbali,


Na katika muawana, punje ya rasilimali,
Nyumbani kiwa hakuna, kukupa mtu muhali,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.

Page | 64
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

5. Kutaka ungekazana, nasaha na tafadhali,


Endapo hana namna, mwenzio lile na hili,
Bora ni kuombeana, Mungu awape sahali,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.

6. Wajua watu hupana, kiasi cha kuhimili,


Mioyo kukunjuana, imani kuwa kamili,
Akwambaye leo sina, kesho kweli takujali,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.

7. Hasa munaopendana, pendo lisotamthili,


Kichache na zaidana, furahani na madhili
Daima mwaambatana, leo ni gani ajili,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.

Maswali
1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 2)
2. Taja na ueleze bahari mbili zinazojitokeza katika shairi hili.
(alama 4)
3. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
4. Andika ubeti wa 6 kwa lugha nathari (ya kawaida). (alama 4)
5. Taja mifano mitatu ya maneno ambayo yameandikwa kishairi
na kisha uyaandike kisanifu. (alama 3)

Page | 65
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

6. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika


shairi:
a) bahili (alama 1)
b) fadhili (alama 1)
c) thakili (alama 1)

USHAIRI WA 29
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.

Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani, kweli mja


hapendeki

Kwa kweli haaminiki, hila ameficha ndani, la wazi ni unafiki

Ukweliwe haafiki, njama zake zi moyoni, usimwone ni rafiki,

Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

Wenginea watakuua, wakiona una pesa, hata zikiwa kidogo

Hizo kwao ni maua, hupupiwa zikatesa, wakizifuata nyago

Hadi kwenye wako au, pasipo hata kupesa, walakukupa kisogo

Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

Page | 66
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Pindi kinunua kitu, hafurahi shaitani, bali tajawa chukizo

Mtu kiwa mtukutu, tanuna mtimani, kwato ako tekelezo

Tamko lake ‘subutu’, kuondoa tumaini, na kukuliza wazo

Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

Aliye na taraghani, taabu kuishi naye, kazi yake kujidai

Takusema faraghani, asosema kiwa naye, kupendeza maadui

Hana faida nyumbani, ni mtu akichimbaye, mradi usitumai

Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

Kwa hakika ni baka, kumkirimu mchawi, aliyejaa uchoyo

Bahati ina hadaa, kukupa alo sodawi, aibarili rowoyo

Mipangayo kwake jaa, na nia ya ustawi, huwiza kuvunja kaniyo

Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

Ninacho changu kilio, ninalia sanasana, kinyesi nimetupiwa

Ningetoa azinio, lakini uwezo sina, kwa mazito kuambiwa

Ama nitimue mbio, fuadinininanena, akilini nazuiwa

Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

Page | 67
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Maswali

a) Toa kichwa cha shairi hili (Alama 1)

b) Eleza sababu za mtungaji kulalamika katika shairi hili (Alama


3)

c) Eleza umbo la shairi hili (Alama 4)

d) Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari (Alama 4)

e) Taja na utoe mifano ya aina mbili za tamathali za usemi


zilizotumika katika shairi hili (Alama 4)

f) Toa mifano miwili tofauti ya uhuru wa kishairi katika shairi hili


(Alama 2)

g) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyo tumika katika


shairi

i) Zani

ii) Faraghani (Alama 2)

Page | 68
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 30
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata

Kila nikaapo hushika tama


Na kuiwazia hali inayonizunguka

Huyawazia madhila
Huziwazia shida
Huiwazia dhiki

Dhiki ya ulezi
Shida ya kudhalilishwa kazini
Madhila ya kufanyiwa dharau
Kwa sababu ya jinsia yangu ya kike

Hukaa na kujidadisi
Hujidadisi kujua kwa nini
Jamii haisikii kilio changu
Wenzangu hawanishiki mikono
Bali wanidharau kwa kuukosoa utamaduni

Hukaa na kujiuliza
I wapi afua yangu dunia hii?
I wapi raha yangu ulimwengu huu?
I wapi jamaa nzima ya wanawake?

Page | 69
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

a) Pendekeza kichwa mwafaka kwa shairi hili {alama 1}


b) Ni nini dhamira ya mshairi? {alama 2)
c) Eleza maudhui yanayojitokeza katika shairi hili {alama 4}
(d)Taja mifano ya tamathali zilizotumika katika shairi hili {alama4}
(e) Dhibitisha kwamba hili ni shairi huru {alama 3}
(f) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari {alama 4}
(g) Eleza msamiati ufuatao ulivyotumiwa katika shairi hili {alama 2}
(i) afua
(ii) hawanishiki mikono

USHAIRI WA 31

Soma shairi hili kasha ujibu maswali yanayofuata


Bahari
1. Bahari uzuri, wake tawambia,
Sifa tabashiri, kuwahadithia,
Ambazo ni nzuri, na faida pia

2. Na faida pia, na kwamba ujue,


Nakukuelea, nawe utambue
Na sasa sikia, uzifafanue.

Page | 70
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

3 Uzifafanue, bahari za pambo


Lenye uzuriwe, pia na urembo
Ni siri ujue, na pia ni tambo

4 Na pia ni tambo, ni siri yakini,


Aidha ni fumbo haiwezekani,
Ina mengi mambo, yenye na thamani

5 Yenye na thamani, kwa watu wa pwani,


Nawapa yakini, nanyi sikizani,
Humo baharini, kwanza pulikani.

6 Kwanza pulikani, lulu twaipata,


Samaki yakini, faida huleta,
Aidha wendani, pia huokota

7 Pia huokota, ambari zinduna,


Munyu na mafuta, vinapatikana,
Faida yaleta, pulikiza sana.

8 Pulikiza sana, tia sikioni,


Tija ya maana, ilo baharini,
Inapatikana, kwa kila ya fani.

Page | 71
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

9 Kwa kila ya fani, samaki twauza,


Mapezi yakini, ya papa sikiza,
Huleta thamani, yenye muangaza.

10 Yenye muangaza, pia na forodha,


Pato huongeza, la kuleta fedha,
Pia yaangaza, bahari kwa adha.

11 Bahari kwa adha, adhaye upepo,


Hapana orodha na ichafukapo,
Huondoka ladha, tena hapo ndipo.

12 Tena hapo ndipo, chombo hutotoma,


Nyote muliopo, hapana msema,
Ndipo muliyapo, “Mama, yoo mama!”,

Maswali
a) Shairi hili ni la bahari gani? Eleza sababu yako {alama 3}
b) Taja faida mbili na hasara mbili za bahari kama
anavyoeleza mshairi {alama 4}
c) Kwa kuzingatia beti mbili za mwisho eleza umbo la shairi
hili {alama 4}
d) Kwa kutoa mifano, eleza idhini ya kishairi alizotumia
mtunzi. {alama 4}

Page | 72
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

e) Andika ubeti wa nane katika lugha nathari. {alama 3}


f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika
katika shairi {alama2}
(i) pulikani
(ii) adhaye

USHAIRI WA 32
. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
Hayawani nondokeya, nondokeya nenda mbali
melaniwa huna haya, leo haja kukabili.
Kimbiya nenda waya, up indo wako usuli?
Umbakaji haini.

Watoto waulizani, changudoa mekushinda?


Umezua vya uhuni, kuyachafua makinda
Pinga kama si punguani, adilifu mekushinda
Umbakaji haini

Wahanyahanya yayaya, mitaani patupatu


Matendoyo kubwayaya , umewasinya wenetu
Nairobi na siaya, kote kote lithubutu
Umbakaji haini.

Page | 73
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Jogoo kuparagia, kifaranga ni halali?


Ukimwi wawapatia, huna akili kamili
Nakutungia sheria, takufunga ukubali
Umbakaji haini.

Maswali
(a) Lipe shairi hili anwani mwafaka (Alama1)
(b) Shairi hili ni la bahari gani? Thibitisha (Alama2)
(c) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa pili (Alama2)
(d) Taja na ueleze tamathali mbili za lugha alizotumia mtunzi
(Alama2)
(e) Andika ubeti wa nne kwa lugha ya nathari. (Alama4)
(f) Taja matendo yoyote matatu mabaya ya anayesemwa.
(Alama3)
(g) Eleza jinsi mshairi alivyotumia uhuru wake wa utunzi.
(Alama4)
(h) Eleza maana ya maneno yafuatayo
(i) Hayawani (Alama1)
(ii) Umewasinya (Alama1)

Page | 74
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 33
. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
UTII
Raia Mwema ni yule, aliyejaa utii,
Si ubishi na kelele, akanywalo hasikii,
Ni mwasi huyo jinale, achunguzwe kwa bidii,
Raia asiyetii, ni fisadi wa nchiye

Uonapo uhalifu, usambe huuzuii,


Ndio huo uvunjifu, kamawe huzingatii
Mwananchi mwadilifu,hilo halikadirii
Raia asiyetii, ni fisadi wa nchiye

Utii kama haupo,sheria haziagii


Imani huwa haipo, na mema hayatujii
Usalama hufa papo, mara nchi ikadhii
Raia asiyetii, ni fisadi wa nchiye
Nia za watu watano, ambazo hazififii
Uchao ni tangamano, si chusa hawachukii
Hushinda kumi na tano, ambao hawatulii
Raia asiyetii, ni fasidi wa nchiye.

Kila raia nchini, ni ile au ni hii


Ana hisa wastani,ingawa haitumii
Hazuiliwi hanani,kusema hatumbukii
Raia asiyetii, ni fisadi wa nchiye.
Page | 75
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Maswali.
(a)Taja sifa mbili za raia Mtiifa. (ala. 2)
(b) Ni mambo gani ambayo hutokea wananchi wanapokosa utii?
( ala.2)
(c) Eleza ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari ( ala 4)
(d) Onyesha mbinu mbili zilizotumiwa ili kuonyesha uhuru wa
mtunzi,kwa kutolea mifano.( ala.2)
(e) Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu. ( ala.2)
(f) Eleza muundo wa shairi. (alam 4)
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa
katika shairi. (ala.4)
(i) Mwasi
(ii) haziagii
(iii) Tangamano
(v) hisa
USHAIRI WA 34
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
Wana –haramu

Hebu nikuulize mama Afrika


Kwa nini………………
Mimba changa ukajichukulia
Ya haramu sana ilotepetea
Ukazaa wana walo jahilia
Wasiojijua, wala yao njia ?

Page | 76
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Kuzurura ukamalizikia
Bila muruwa, heba kukupotea
Ukawa ganda la kupita njia
Usije maoni ya kuonelea?

Kwa nini……………..
Ukazaa kizazi kilo kiwete
Kilihasirika kwa wakati wote
Kilichopagawa kwa kingi kite
Hata utu wake ukakipotea?

Ah moyo waumia!
Hupigwa na mshangao
Niwafikiriapo
Wale barobaro wanao
Wasaliti wanati walo na vyeo
Walomdhidi mama mzazi wao
Kwa muradi wao.

Lakini sijali
Sijali kwani najua
Siku moja itawadia
Wanaharamu watajihalalia
Kila cha haramu kukuondolea
Na kukurakasa…..
Mama wasikia?
Hiyo siku ya siku itakapofika
Kila la dhuluma litajikatika
Na kila mahali utadhihirika
Mwisho wa salata na uharamia…….
Mama wasikia?

Page | 77
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Maswali
(a) mwandihsi analalamikia mambo yapi katika shairi hili?
( ala.5)
(b) Mwandishi ametumia mbinu gani katika kutumia maneno. “
Mama Afriaka?” Neno hili limetumika kumaanisha nini?( ala. 4)
(c) Andika ubeti wa nne katika lugha ya nathari. ( ala.4)
(d) Eleza maana ya maneno yafuatatyo: ( ala 5)
(i) jahilia (ii) Muruwa
(iii) Kilohasirika (iv) kite
(v) Barobaro.
(e) Mtunzi anamaanisha nini anaposema, ‘ukazaa kizazi kilo kiwete?’
( ala. 2)

USHAIRI WA 35
Shairi A:
1. Jaribu kuwa mpole, kwa wenzio darasani,
Jihadhari na kelele, na utusi mdomoni,
Wala siwe kama wale, wanafunzi maluuni,
Waso akili vichwani, katu usiwaingilie.

2. Ujipanyapo ja vile, watoto wale wahuni,


Juwa jatakwenda mbele, utashindwa mtihani,
Na toka dakika ile, utaingia mashakani,
Jaribu uwe twaani, mwanafunzi zingatile.

Page | 78
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

3. Mtoto kiwa mpole, nakueleza yakini,


Huwa ni mfahamile, wa elimu akilini,
Ni shida kuangukile, kushindwa na mtihani,
Yataka utamakani, mwanafunzi siliwale.

4. Mwanafunzi nakukanya, kwa yale mawi mwandani,


Sizowee kusengenya, sengenyo madarasani,
Kama hilo ukifanya, utakuwa mashakani,
Ni hayo nilowaonya, kwa hiyo nawaageni.

Shairi B:
Aliniusia babu, zamani za utotoni
Kanambia jitanibu, na mambo ya nukaani
Na wala usijaribu, kwa mbali wala jirani
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

Liche jambo la aibu, lipalo mtu huzuni


Liuvunjao wajibu, m’bora akawa duni
Lau chamba utatubu, kulipwa hukosekani
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

Page | 79
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Usipolipwa karibu, lakutoka fahamuni


Lazima lije jawabu, ingawa pindi mwakani
Japo kuwa ughaibu, au mwisho uzeeni
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

Kila neno lina jibu, usitafute kwa nini


Mambo yenda taratibu, pupa jingi lafaani
Akopeshae zabibu, atalipwa zaituni
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

Ahimilie taabu, hupata mema mwishoni


La raha au sulubu, malifi ni duniani
Mambo bahati nasibu, viumbe tahadharini
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.
Maswali:
a) i) Linganisha shairi A na B kwa kuzingatia maudhui. (Alama 6)
ii) Linganisha na kutofautisha mashairi A na B ukizingatia sifa
za arudhi. (Alama 6)
b) Toa mifano miwili yoyote ya inkisari kutoka kwa mashairi haya.
(Alama 2)
c) Fafanua maana ya mishororo ifuatayo kama ilivyotumiwa katika
mashairi haya. (Alama 2)
i) Kanambia jitanibu, na mambo ya nuksani.
ii) Mwanafunzi nakukanya, kwa yale mawi mwandani.

Page | 80
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

d) Eleza maana ya msamiati ufuatao (Alama 4)


i) Nuksani
ii) Sulubu
iii) Malifi
iii) Katu

USHAIRI WA 36
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.

Ameumbuwa mwanadamu,kwa lililo zuri umbo,


Basi si wote fahamu, waliyo na sawa mambo,
Wako waliyotimamu, na wengineyo wa kombo
Na mtu kuwa na tumbo, si kwamba mekamilika.

Kuna walo mafidhuli, lugha yao ni matango,


Na kuna wenye kauli, zisokuwa na ushingo,
Kuna wake kwa wavuli, vipofu na wenye tongo,
Na mtu kuwa na shingo, si kwamba mekamilika.

Kuna walo na fikira, na wenye vibovu vitwa,


Kuna walo na subira,husubiri kucha kutwa,
Wengine tabiya ya bora, hino huwanayo katwa,
Na mtu kuwa na kitwa , si kwamba mekamilika.

Page | 81
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Kukamilika kwa Mja, ni mbali na kwa moliwa,


Kwa Mja nitakutaja, ili upate kwelewa,
Ni kufikiya daraja, ile aliyoumbiwa,
Hapo ndipo huambiwa, Mja amekamilika.

Aiyelewe duniya, kwa marefu na mapana,


Azipite zile ndiya, za miba mitungu sana,
Avuke bahari piya, zito na virefu vina,
Hiyo ni yangu maana ya mja kukamilika.

Akishafikwa na hayo, si kwamba ndiyo akhiri,


Lazima awe na moyo, wa kuweza kusubiri,
Kuyasubiri ambayo, yote yatayomjiri,
Kama huyo tamkiri, ni mja mekamilika.
Maswali.
(a)Kulingana na shairi hili ni yapi humfanya mtu kuwa na utu.
Taja matano (ala. 5)
(b) Fafanua namna mshairi alivyofaulu kutumia uhuru wake
( ala.4)
(c) Eleza maana ya vifungu hivi kama vilivyotumiwa katika
shairi ( ala 3)
(i) Vibovu vitwa.
(ii) Tabiya Bora
(iii) Mtu kuwa na kitwa
(d) Msanii anakiri nini kuhusu Mja? ( ala.2)

Page | 82
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

(e) Andika ubeti wa tano kwa lugha nathari ( ala.4)


(f) Eleza Umbo la shairi hili kwa kuzingatia mizani na vina
(ala.2)

USHAIRI WA 37
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Nina jambo muhimu, nyi wakubwa kwa wadogo,


Kuwa tabia alimu, usiubwage gogo,
Mtu kukosa nidhamu, ja mtu akili ndogo,
Tabia njema ni utu.

Walezi nawaambia, wafunze tabia wana,


Ili wanapokua, wenye heshima maana,
Mtu kukosa tabia, ni kama mti bila shina,
Tabia njema ni utu.

Hutuzidisha hisia, kufurahisha roho,


Gumu tuepushia, linalotumiza roho,
Mtu kukosa twabia, nikiumbe bila roho,
Tabia njema ni utu.

Wanafunzi nao pia, shuleni sizushe bala,


Ili masomo kubia, bila mambo ya kifala,
Mtu kukosa twabia, dareva toroli bila,
Tabia njema ni utu.

Mahabani walioa, sio urembo mwingi,


Bali hasa ni tabia, utu mapenzi mengi,
Mtu kukosa tabia, kama nyumba bila msingi,
Tabia njema ni utu.

Page | 83
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Shuleni vijijinia, amani dumu kujali,


Sababu kuwa tabia, lizingatiwa aali,
Mtu kukosa tabia, ni kisu bila makali,
Tabia njema ni utu.

Rafiki kukupendea, sio kwa uzuri eti,


Bali ni hasa tabia, ndani yako wima uti,
Mtu kukosa tabia, ni kiumbe bila uti,
Tabia njema ni utu.

Tamati kuachia, kwamba jambo aali,


Mengi ningewambia, lakini metoshekali,
Mtu kukosa tabia, ni kiatu bila soli,
Tabia njema ni utu.

MASWALI
1. Pendekeza kichwa mwafaka la shairi ulilosoma. (alama 1)
2. Shairi hili linaweza kuwekwa katika bahari tatu tofauti. Taja
ukitolea sababu. (alama 3)
3. Fafanua muundo wa shairi hili. (alama 4)
4. Huku ukidhibitisha, onyesha jinsi mshairi alivyotumia idhini
yake ya kishairi. (alama 4)
5. Taja na uonyeshe mbinu za lugha zilizotumika katika shairi
hili. (alama 2)
6. Andika ubeti wa sita katika lugha tutumbi. (alama 4)
7. Eleza maana ya maneno haya kwa mujibu wa shairi.(alama 2)
a. Shina
b. Wima

Page | 84
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 38
Soma shairi ulilopewa kwa makini kisha ujibu maswali (ala. 20)

Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani ,kweli mja hapendeki,


Kwa kweli haaminiki,hila ameficha ndani,la wazi ni unafiki,
Ukweliwe haafiki, njama zake zi moyoni,usimwone ni rafiki,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake,ni hatari kama nyoka.

Wengine watakuua,wakiona una pesa,hata zikiwa kidogo,


Hizo kwao ni maua,hupupiwa zikatesa,wakizifuata nyago,
Hadi kwenye wako ua, pasipo hata kupesa, wala kukupa kisogo,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

Pindi kinunua kitu, hafurahi shaitani, bali tajawa chukizo,


Mtu akiwa mtukutu, tanuna mtimani,kwalo lako tekelezo,
Tamko lake “Subutu”, kuondoa tumaini, na kukuulia wazo
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

Aliye na talaghani, taabu kuishi naye,kazi yake kujidai,


Takusema faraghani, asosema kiwa naye, kupendeza maadui,
Hana faida nyumbani, ni mtu akuchimbaye, mradi asitamai.
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

Page | 85
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Kwa hakika ni balaa, kumkirimu mchawi, aliyejaa uchoyo,


Bahati ina hadaa, kukupa alo sodawi,aibatili rohoni,
Mipangoyo kwake jaa, na nia ya ustawi, huwiza kuvunja kaniyo,
Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake,ni hatari kama nyoka.

Ninacho changu kilio, ninalia sana sana, kinyesi nimetupiwa,


Ningetoa azimio, lakini uwezo sina, kwa mazito kuambiwa,
Ama nitumue mbio, fuadini ninanena, akilini nazuiwa,
Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

Maswali
(a) Toa kichwa cha shairi hili. (ala. 1)
(b) Eleza sababu za mtunzi kulalamika katika shairi hili. ( ala. 3)
(c) Eleza muundo wa shairi hili. (ala.4)
(d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari ( ala.4
(e) Taja na utoe mifano ya aina mbili za tamathali za usemi
zilizotumiwa katika shairi hili. (ala.4)
(f) Toa mifano miwili tofauti ya uhuru wa kishairi katika shairi hili.(al2)
(g) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi.
(ala.2)
(i) Zani
(ii) Taraghani

Page | 86
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 39
Soma shairi hili kasha ujibu maswali yafuatayo
Unganambia ni mui, katu siuwati wema,
Wewe ndiwe wangu, bui, nalousiwa na mama,
Leo kwamba siujui, ni kupotosha heshima
Siati kutenda wema, kanandama uadui

Wema anambiwa ni ndia, hadi bandari salama


Hayo inliyasiklia, nao wahenga wa zama
Penye wema nitajitia, ipate taadhima
Siati kutenda wema, japo mungainunia

Na iwe kupawa mali, ya kuhadaa mtima,


Niandame ufidhuli, itengane nao wewa
Hilo sitokubali, japo waja wangasema
Siati kutanda wema, ujapokuwa ni ghali

Sotomcha kabaila, nganitenza nache wema


Munganitia na jela, kisa imefanza hruma
Haragwe lenu talila, pamoja na yenu sima,
Siati kutanda wema, japo tagoni talala
Haufi mungaufihsa, auhamipo karima’
Mola atauhuisha, welekeapo kuzama
Mimi kutanda wema, nganitia mshawasha

Page | 87
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Wema uNgawa mchungu, tajaribu kutotema,


Tautenda nende zangu, niache wanaosema
Malipo yangu kwa Mungu, hayo ynu si lazima
Siati kutenda wema, kigharimu roho yangu

Maswali

a) Ukizingatia beti nne za mwisho, taja mambo ambayo hata


mshairi akifanyiwa hawezi kuacha kutenda mema (ala4)
b) Elza jinsi matumizi wa shairi hili alivyotumia uhuru wake
(ala4)
c) Mhairi alipata wapi ari ya kuzingatia wema (ala1)
d) Eleza muundo wa ubeti wa pili ukizingatia mizani na vina
(ala2)
e) Eleza maudhui ya shairi hili (ala2)
f) andika ubeti wa mwisho katika lugha ya nathari (ala4)
g) Eleza maana ya maneno jafuatayo kama yalivyotumika katika
shairi(ala3)
i) Mtima
ii) Kutotema
iii) Kigharimu roho wangu

Page | 88
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 40
soma mashairi yafuatayo kasha ujibu maswali

Ngoma Ya Vilini

1. Huo, huo, mpwitopwito wa ngoma,


Unachemsha damu yangu,
Na matamanio yaliyo ladha
2. Damy iliyopozwa na kubembelezwa,
Na vilini nyororo, vailini inayonita,
Kwa huzuni yenye furaha
3. Sasa nacheka na kupwitapwita,
Sasa nafurahi na kuburudika
Mdundo wa maisha
Wapi niende?

4. Lazima niswali-niabudu
Nimuabudu Allah,
Lakini atasikia sauti yenye panda,
Sauti yenye panda,
Sauti inayotaokana na mwenye kuvaa,
Kanzu na msalaba?

Page | 89
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

B
Kisu Mkononi: Euphrase Kesilahabi
1. Wakati miaka inaibwea mmoja mmoja
Kurudi nyuma, kusimama kupunguza mwendo,
Siwezi, kama gurudumu nitajivingirisha,
Mteremko mkali huu
Lini na wapi mwisho sijui
2. Mbele chui mweusi, nyuma mwanga,
Nionako kwa huzuni, vifurushi maelfu vya dhambi,
Kisu, maisha kafiri haya,
Kama kutazama nyuma au mbele
Ni kufa moyo mzima:
3. Sasa kama samba-mtu shauri nimekata,
Ya nyuma sana siyajui, ya mbele sasa nayakubali,
Kwa ujasiri na uangalifu nitazunguka,
Nikifuata kama ng’ombe aliyefungwa,
Kila mpigo wa moyo wangu,
Huu prigo muziki wa maisha.

a) Pendekeza mada moja kuu inayoafiki ujumbe wa mahsairi yote mawili


(ala1)
b)Dhana ya ‘maisha’ imesawiriwa vipi katika mashairi A na B (ala4)
c) Taja tamathali moja ya usemi iliyotumika katika mashairi yote na
uonyeshe mifano miwili ya jinsi ilivyotumika (ala3)

Page | 90
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

d)Linganisha mashariri A na B upande wa umbo (ala6)


e) “Wahsairi wanafanya maamuzi mawili muhimu.” Dondoa mfano mmoja
kutoka kila shairi kushadidia kauli hii (ala2)
f) Ukitumia mifano, dhihirisha hsia mbili zinazoibuka katika mashairi haya
(ala2)
g)Mishororo ifuatayo in maana gani shairini (ala2)
(i) Kwa huzuni yenye furaha
(ii) Mbele chui mweusi, nyuma mwanga

USHAIRI WA 41
Soma shairi lifuatalo halafu ujibu maswalli yanayofuata

1. Upasi: HassanM Mbega

Upasi ukija, usipokukoma, hukupa teo,

Hupata faraja, utakapochuma, chumo lijapo

Hufunga kharija, kutokuandama. ‘kwa hazipo,

Watu hukutaja, kusifiwa wema, hujatendapo,

Kukifika haja, ukawa u wima, kwa yaliyopo.

Page | 91
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

2. Upasi ukija, ukiwa u mwema, kwa upatapo

Maovu huchuja, yakabaki thama, mema malipo

Pasingie hoja, isije lawama, popote ziwapo,

Ukapata tija, zilizoegemea, kwa kisichopo

Usiwe kufuja, japo ukatuma, na utawapo.

3. Upasi ukija, hujia salama, tata zisipo,


Ukapata moja, nyingine zi nyuma, pale ulipo,
Hutokea waja, kukupa hishima, waso’ kujapo
Sione vioja, ndizoze alama, pao lilipo,
Subiri kungoja, na nyingi rehema, zisoshukapo.

4. Upasi ukija, mpaka khatima, ukiwa upo,


Hukuvika koja, lilosakama, losovukapo,
Pasiwe pamoja, utakaposema, llisitimupo,
Ukawa mmoja, katika azima, usikosepo,
Ukafuzu hijia, kishapo kiyama, wapata pepo.

5. Upasi ukija, sizivute chama. Wala viapo


Zache tafrija, zipazo lawama, zisofanywapo,
Usiwe washaja, usiku mzima, kutolalapo,
Kufanya miuja, , na majitapo,
Mwisho utakanama, utakuja, uwe kulalama, usitakapo.
Page | 92
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

6. Hilo, ‘melitaja, hakwambia thuma, usoshikapo


Majuto hupija, kondo’ye kinyuma, pale wishapo,
Wenda kuleja, mangi ukasema, yashokwishapo,
Huondoka daraja, zilizosimama, kula kuchapo,
Zibaki huja, macho yakamana, likesha tapo

a) Taja mawazo yoyote manne yanayoendelezwa na msanii katika


shairi hili (ala5)
b) Eleza mbinu mbili za kumuundo zinazojitokeza katika ubeti wa
mwisho (ala2)
c) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari (ala4)
d) Fafanua sifa za kiarudhi katika ubeti wa pili (ala4)
e) Onyesha madhumuni ya msanii katika shairi hili (ala2)
f) Tambua mbinu mbili za kisauti zilizotumiwa kujenga wazani
katika shairi (ala2)
g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika
shairi(ala2)
I) Tepo
II) Yakamana

Page | 93
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 42
Soma shairi hili kasha ujibu maswali yanayofuata

Ulimwengu jifa, na kusimangana


Kingiacho ufa, hakiungi tena
Kizima kikafa, hakidumu sana
Walipwao sifa, kabisa hakuna

Ulimwengu ghafi, thamani hauna


Bakia ulafi, na kipokonyana
Ukipigwa kofi, na kusukumana
Wapendao, safi huwezi waona

Ulimwengu gofu, la kuzoeana


Una udhaifu, wa kutizana
Huzidi machafu, hisabu hayana
Na waaminifu, kwa kukosekana

Ulimwengu kiza cha kutoonana


Una miujiza, isosemekana
Mara hutatiza, ukose namna
Wa kimmuliza , utabaki huna

Page | 94
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Ulimwengu zuz, wa kuzuzuwana


Unga vile tanzu, isoshikamana
Japovaa kanzu, mikono mipana
Bado hujafuzu, muombe Rabbana

Ulimwengu guzo, mambo’ye vitimbi


Uwelee chanzo, kutendea dhambi
Hawishi mizozo, na kilimbilimbi
Mbali matatizo, panapo ukumbi

(a) Lipe shairi hili anwani mwafaka


(b) Shairi hili ni la bahari gain? Thibitisha.
(c) Nini tasnifu ya mtunzi juu ya swala analoangazia
(d) Mtunzi ametumia uhuru wa kishairi katika utungo huu. Toa
mifano miwili.
(e) Eleza sifa za kiarudhi ambazo zimetumika katika shairi hili.
(f) Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari
(g) Fafanua maana ya msamiati huu kwa mujibu wa shairi
(i) ghafi
(ii) Tanzu
(iii) Uwelee

Page | 95
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 43
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
NDWELE
Kumeota kuu ndwele, kubwa yeye kutuhini
Kila mja kama mwele, hakuna wa kuauni
Kwa vijana na wavyele, wote wako taabani.

Ndwele hii inasomba, watu wote kama mto


Mahali kote yapamba, wenda fuata mivuto
Watumia kama pamba, bila kujali majuto

Jama kweli kubwa janga, sichukulie utani


Kila mja hangahanga, haijui mvumini
Ndwele hii ni mzinga, yadondosha visirani
Kumezuka ndwele kuu, twahitaji mganguzi

Waungwana kwa watwana, huyabugia sawia


Wenye vyeo vya kufana, kwa juhudi huvamia
Pasi wao muawana, matindi huyabugia
Kumezuka ndwele kuu, twahitaji mganguzi

Katika wao ulevi, ngwenje pyuu zaishia


Pia huletana wivi, za hama zenye balaa
Wamekuwa ja kipofu, wasalis na kelele
Kumezuka ndwele kuu, twahitaji mganguzi

Page | 96
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

(a) Eleza madhara ya ndwele hii yalivyodokezwa na mshairi. (Alama 4)


(b) Toa mifano miwili miwili ya taswira na tashbihi alizozitumia
mshairi. (Alama 4)
(c) Eleza ubeti wa tano katika lugha ya nathari. (Alama 4)
(d) Taja mfano mmoja wa mazida aliotumia mshairi. (Alama 2)
(e) Eleza umbo la ubeti wa nne. (Alama 4)
Katika shairi. (Alama 2)
(i) Ndwele
(ii) hangahanga
(iii) Inasomba
(iv) Waumbua

USHAIRI WA 44
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
Mbele ya safari
Ilipoanza safari, ilianza kwa dhiki
Tulipatikana kwa ari, kwenda safari ya haki
Tukawa ma majabari, nyoyo zisitaharuki
Tukajizatiti
Njaa ikawa dhabiti, na kiu kutamalaki
Nasi tulitia dhati, tusijali kuhiliki
Ingawa mbele manti, dhila na mingi mikiki
Tulijizatiti

Page | 97
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Huu mwisho wa safari, tukaambiwa ni haki


Shangwe kwetu na fahari, utumwa hatuutaki
Kuwa mbele ya safari, juhudi iliyobaki
Tulijizatiti
Ile ilikuwa ndoto, mwisho wake mafataki
Nguvu zimechomwa moto, sahali ‘mekuwa dhiki
Wagombania kipato, utashi haukatiki
Twataka hazina
Tukiwa migongo wazi, tukainama kwa haki
Tukawa ‘chia ukwezi’, kileleni wadiriki
Wakapandwa bila kazi, kuteremsha miliki
Wakaitapia
Wakafikia makazi, ya pumbao na ashiki
Huko wakajibarizi, kwenye raha lakilaki
Wakaisahau ngazi, ya umma ulomiliki
Mbele ya safari.
Na lazima yetu sote, kuishusha hawataki
Wamo wanatema wote, kwa umati halaiki
Imezimia nia yote, kiza hakitakasiki
Mbele ya safari.
(a) Eleza mambo anayeleza mshairi katika utungo wake. (Alama 3)
(b) Je, mshairi ana furaha ama huzuni? Eleza. (Alama 3)
(c) Dondoa wahusika na utoe sifa moja kwa kila wahusika. (Alama 3)
(d) Eleza umbo la shairi hili. (Alama 4)

Page | 98
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

(e) Andika ubeti wa nne kwa lugha ya nadhari. (Alama 4)


(f) Fafanua maana ya:
(i) Sahali ‘mekuwa dhiki
(ii) Tukawa ‘chia ukwezi’, kialeni washiriki

USHAIRI WA 45
Soma mashairi haya kisha ujibu maswali yanayofuata.

SHAIRI A

TABASAMU ZAO: Timothy Arege


Nitafakaripo kwa tuo
Moyo hunitweta na mtetemo kunivaa
Wanijiapo na tabasamu
Ambazo hulinyonga tumaini langu
Ninahuzunika.

Wanisalimiapo kwa mikono miwili


Na chini kuniinamia
Wakiyakoleza yao matamshi
‘Mzee…ndugu…Salama ! Salama !’

Page | 99
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Nachukia zao nyendo.


Wanadai kwa mihemko
‘Lazima tungo kutetea wanyonge’
Lakini nitazamapo, wenyewe hawasiti
Mnyonge mkononi kumtia
Na kwa maguvu kumfikicha
Haki yake kumhini
Mtetezi kumhini
Mtetezi kufaidi.

Wote hawa sioni yao tofauti.


Wote hawa, sawa
Na mwanasiasa mwehu
Ni mtoto wa jicho.
Wanapotabasamu nachelea kuridhia.
Hutabasamu wadhamiriapo vingine.
Tabasamu zao ni ishara ya maangamizi
Wanipangiayo kimoyomoyo, kimyakimya
Wafurahie kutakarika kwangu
Kwenye tanuri hii ya maisha.

Page | 100
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

SHAIRI B

MUWEREVU HAJINYOWI: Abdilatif Abdalla

Mwenye nacho wajishasha, wajiona kama ndovu


Kitu kimekulewesha, huutambuwi uovu
Ngoma yako itakesha, au ni nguvu za povu?
Tangu lini muwerevu, akajinyowa mwenyewe?

Tangu ukite kwa kitu, ‘megeuka mpumbavu


Katu kuthamini mtu, ambaye kwamba mtovu
Wafikiri kisu gutu, hakikati nyama pevu?
Tangu lini muwerevu, akajinyowa mwenyewe?

Kupata kusighuri, ukidhani muwerevu


Na hicho chako kiburi, ujuwe ni maangavu
Iko siku tajiri, ujikute mwenye wavu
Tangu lini muwerevu, akajinyowa mwenyewe?

Kila mwenye kukuonya, uiwate ndiya mbovu


Huchelewi kumminya, kumvunda zake mbavu
Fanya ambayo wafanya, bada ya mbiti ni mbivu
Ungajidai muwerevu, hutajinyowa mwenyewe.

Page | 101
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Maswali
1. (a)Mashairi haya ni ya aina gani? Toa sababu zako. (alama 2)

(b)Linganua mashairi haya kiarudhi. (alama 4)


(c) Eleza jinsi mtunzi wa shairi B alivyofaulu kutumia uhuru wake.
(alama 3)
(d) Fafanua maudhui ya mashairi haya. (alama 2)
(e) Eleza falsafa ya mtunzi wa shairi A. (alama 1)
(g) Taja na ufafanue mbinu za kisanaa zilizotumika katika mashairi
haya. (alama 3)
(h) Andika ubeti wa nne wa shairi B kwa lugha tutumbi. (alama 4)
(i) Eleza maana ya kifungu kifuatacho. (alama 1)
Wafikiri kisu gutu

USHAIRI WA 46
Shairi A:
1. Jaribu kuwa mpole, kwa wenzio darasani,
Jihadhari na kelele, na utusi mdomoni,
Wala siwe kama wale, wanafunzi maluuni,
Waso akili vichwani, katu usiwaingilie.

2. Ujipanyapo ja vile, watoto wale wahuni,


Juwa jatakwenda mbele, utashindwa mtihani,
Na toka dakika ile, utaingia mashakani,
Jaribu uwe twaani, mwanafunzi zingatile.

Page | 102
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

3. Mtoto kiwa mpole, nakueleza yakini,


Huwa ni mfahamile, wa elimu akilini,
Ni shida kuangukile, kushindwa na mtihani,
Yataka utamakani, mwanafunzi siliwale.

4. Mwanafunzi nakukanya, kwa yale mawi mwandani,


Sizowee kusengenya, sengenyo madarasani,
Kama hilo ukifanya, utakuwa mashakani,
Ni hayo nilowaonya, kwa hiyo nawaageni.

Shairi B:

Aliniusia babu, zamani za utotoni


Kanambia jitanibu, na mambo ya nukaani
Na wala usijaribu, kwa mbali wala jirani
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

Liche jambo la aibu, lipalo mtu huzuni


Liuvunjao wajibu, m’bora akawa duni
Lau chamba utatubu, kulipwa hukosekani
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

Usipolipwa karibu, lakutoka fahamuni


Lazima lije jawabu, ingawa pindi mwakani
Japo kuwa ughaibu, au mwisho uzeeni
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

Kila neno lina jibu, usitafute kwa nini


Mambo yenda taratibu, pupa jingi lafaani
Akopeshae zabibu, atalipwa zaituni
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

Ahimilie taabu, hupata mema mwishoni


La raha au sulubu, malifi ni duniani
Mambo bahati nasibu, viumbe tahadharini
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.

Page | 103
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Maswali:
b) i) Linganisha shairi A na B kwa kuzingatia maudhui. (Alama 6)
ii) Linganisha na kutofautisha mashairi A na B ukizingatia sifa
za arudhi. (Alama 6)
b) Toa mifano miwili yoyote ya inkisari kutoka kwa mashairi haya.
(Alama 2)
c) Fafanua maana ya mishororo ifuatayo kama ilivyotumiwa katika
mashairi haya. (Alama 2)
i) Kanambia jitanibu, na mambo ya nuksani.
ii) Mwanafunzi nakukanya, kwa yale mawi mwandani.

d) Eleza maana ya msamiati ufuatao (Alama 4)


i) Nuksani
ii) Sulubu
iii) Malifi
iv) Katu

USHAIRI WA 47
Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali:

Jama, yasikilizeni, nisemayo mbaini


Jama, sitie kapuni, kwamba hayana maoni
Jama, yanayo uzani, mkubwa uso kifani
Walemavu tuthamini, wanayo kubwa thamani.

Page | 104
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Jama, tusiwatengeni, kuwaondoa kundini.


Jama, mbele wapisheni, pasi haya usoni,
Jama, dosari mwilini, haifanyi mja duni,
Walemavu tuthamini, wanayo kubwa thamani

Jama, waenda shuleni, hata pia na kazini,


Jama, wawapo njiani, tusiseme ondokeni,
Jama, siwasukumeni, tusiwatusi katani,
Walemavu tuthamini, wanayo kubwa thamani.

Jama, na mahakamani, haki yao ilindeni,


Jama, sheria mbungeni, iwe nawathamini,
Jama, japo hawaoni, chao sitwae mwengini,
Walemavu tuthamini, wanayo kubwa thamani.

Jama, kule viwanjani, wasitengwe asilani,


Jama, wawe michezoni, hata washinde nishani,
Jama, pia burudani, wana haki kumbukeni,
Walemavu tuthamini, wanayo kubwa thamani.

Jama, leo sikizeni, msiuze wasemani,


Jama, japo hawaneni, ishara zao jueni,
Jama, mwapuza acheni, ni watu si hayawani,
Walemavu tuthamini, wanayo kubwa thamani.

Page | 105
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

(a) Taja na ufafanue bahari zozote mbili za shairi hili. (alama 2)


(b) Eleza jinsi kanuni za utunzi zilivyotumiwa kusarifu ubeti wa pili
wa shairi hili. (alama 4)
(c) Toa mfano mmoja mmoja wa neno lililotumiwa kwa
maksudi ya:
(i) Ulinganifu wa vina.
(ii) Kusawazisha mizani. (alama 2)
(d) Toa mfano mmoja mmoja wa tamathali zozote mbili
zilizotumiwa kwenye shairi hili. (alama 2)
(e) Eleza dhamira ya mshairi wa shairi hili. (alama 2)
(f) Ni mlemavu yupi anayerejelewa katika:
Ubeti wa 4
Ubeti wa 6 (alama 2)
(g) Andika ubeti wa tano kwa lugha ya nathari. (alama 4)
(h) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa
kwenye shairi.
(i) Katani
(ii) Hayawani. (alama 2)

Page | 106
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 48
USHAIRI

Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.


Hakika siku ya leo, ni siku ya majivuno
Basi pasiwe na choyo, na usonono
Tulekezane yaliyo, unawiri Muungano.

Tuzisafisheni nyoyo, pasiwe na miguguno


Yaongoke tutakayo, kusiwe na mabishano
Mbegu hii tupandayo, ilete mema mavuno.

Tufungulie upeo, Mola usiye mfano


Pa kitasa na komeo, tupite bila kinzano
Tupitishe njia hiyo, pasina masongamano

Twakuomba uumbao, mkono vyanda vitano


Tushikane hii leo, tuwe moja tangamano
Tupendane kwa pumbao, hali na maridhiano

Aliye ana machukiyo, adui wa Muungano


Naazibe masikiyo, asisikie maneno
Kisha awe kibogoyo, asiwe na moja jino.

Page | 107
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Ya Ilahi ujalie, huu wetu Muungano


Nuru yake izagae, na nguvu za mapigano
Hasidi mpe hakie, mateso yaso mfano.

Watamati komeleo, kuimba kwangu hukuno


Nataka maendeleo, yasiyo na malumbano
Daima tuwe ni ngao, palipo msagurano.

(a) Toa kichwa cha shairi hili. (alama 2)


(b)Shairi hili ni la bahari gani? Taja mbili. (alama 2)
(c) Taja sifa tano za aina hii ya ushairi. (alama 5)
(d)Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari. (alama 3)
(e) Eleza maana ya mshororo ufuatao: Pa kitasa na komeo, tupite bila
kinzano. (alama 3)
(f) Huku ukitoa mifano mitatu eleza uhuru wa ushairi katika shairi
hili. (alama 3)
(g)Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika
shairi. (alama 3)
(i) Usonono :
(ii) Vyanda:
(iii) Msagurano:

Page | 108
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 49
Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali. Utendewapo uovu, wa kupituka
Utendewapo uovu, wa kupituka kiwango
Moyo siutue chevu, ukautapisha nyongo
Na kujipa maumivu, ya fikira na maungo
Kipitacho kipe chogo, kitendo hakina kovu

Lingawa Ia maonevu, simbulizi na matangondo


Au la kutenzwa nguvu, hizaya na masimango
Usingie ulemavu, moyo kuupa kisongo
Kipitacho kipe chongo, kitendo hakina kovu,

Kitendo hakina kovu, sijitie songo songo


Mcha mungu si mtovu, kwalo sijie pengo
Changa hugeuka pevu, tizama embe na tango
Kipitacho kipe chongo, kitendo hakina kovu.

Ungaliona ni kavu, lakuumiza mgongo


Lifanye jepe ja povu, lifukie na udongo
Moto mwishowe ni jivu, hakuna liso kiungo
Kipitacho kipe chongo, kitendo hakina kovu

Mangapi yalo matevu, kwa matao na maringo


Yatia kichevuchevu, ukachafuka ubongo
Yakeshia uptevu, ja pepe ndani ya ungo
Kipitacho kipe chongo, kitendo hakina kovu
Page | 109
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Twaa mfano wa ndevu, zimeazo hata shigo


Zikazunguka mashavu, kusongana mviringo
Hazilemei kidevu, hazikutii kibyongo
Kipitacho kipe chongo, kitendo hakina kovu.

Vyambiwa mvumilivu, msubiri japo bungo


Hupata lililo bivu, bivu lisili na chongo
Bora kuwa mtulivu, mwaka huanza miongo
Kipitacho kipe chongo, kitendo hakina kovu

Maswali

a) Eleza maushui ya mshariri huyu. (ala4)


b) Kwa kurejelea vina, eleza bahari ys ushairi inayokita katika
utunzi (ala4)
c) Kwa jinsi mshairi ametumia uhuru wa ushairi katika utunzi huu
(ala4)
d) Andika ubeti wa-nne ka lugha ya nathari (ala4)
e) Eleza sifa za kiarudhi zinazopatikana katika utunzi huu (ala4)
f) Eleza maana ya msamiati huu kwa mujibu wa shairi (ala2)
i) Chongo
ii) Maonevu (ala20)

Page | 110
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

USHAIRI WA 50
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yatakayofuata.
Hayano yametokea, tangu zama hadi sasa,

Janibu zilipotea, kwa mambo yenye kunasa?

Zile ziliondolea, zilishinda kunyanyasa,

Siweke kati anasa, unapounga tawala

Walipokutana chungu, kolokolo na matime,

Kutaka vunja ufungu, ukabila ndo wahame,

Pakatokea vurugu, zikatusiana tume,

Kita nguzo uzipime, ujengapo utawala

Nao mchwa na siafu, pamoja walibarizi,

Mkutano kusafiri, kuunda jambo azizi,

Hakuna lililosadifu, kwa kuparamia enzi?

Kwa tamaa viongozi , walishindwa utawala

Wakaja na wale nzi, kereng’ende nao nyuki,

Wakawasili na panzi, na chafuo mnafiki,

Pakazuka uushenzi, hakuna alo diriki,

Hakuna waloafiki, kuujenga utawala


Page | 111
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Wadudu kila aina, kuungana walitaka,

Huku walikopatana, ikawa kutawanyika,

Ya kwamba wangeungana, hakuyataka Rabuka,

Umoja kwao mashaka, hawawezi utawala

Hulka hino kwa mja, ‘mepambiwa na Manani,

Waungane kwa umoja, na kusambaza amani,

Na upendo kupambaja, huyapata ya peponi,

Wanati tuunganeni, tuujenge utawala

Maswali

a) Pendekeza kichwa mwafaka kwa shairi hili. (alama 2)


b) Taja na ueleze mbinu kuu ya uandishi iliyotumika katika shairi
hili. (alama 2)
c) Andika ubeti wa tano kwa lugha ya kawaida. (alama 4)
d) Chambua umbo la shairi hili (alama 4)
e) Fafanua bahari mbalimbali za ushairi zinazopatikana katika
shairi hili (alama 3)
f) Eleza idhini ya kishairi ilivyotumika katika shairi hili (alama 3)
g) Eleza maana ya msamiati huu. (alama 2)
i) Pakazuka
ii) Na upendo kupambaja

Page | 112
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes
[email protected]

Page | 113
Prefer Calling Sir Obiero Amos @ 0706 851 439 for Marking Schemes

You might also like