Nguu Za Jadi BEST QUIGK GUIDE

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 25

TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

NGUU ZA JADI GUIDE

Jalada, Anwani na Muhtasari

Katika jalada la riwaya ya Nguu za Jadi, kuna vitu anuwai vinavyoonekana, na vinaweza
kuwa na fasiri mbalimbali kwa wasomaji tofautitofauti. Vitu vilivyopo kwenye mchoro wa
jalada hilo ni:

a) Picha ya mwanamume mzee anayemzungumzia mvulana. Kutokana na


wanavyoonekana, ni wazi wamefunikwa kwa kiwango cha haja na giza. Hii
inaweza kuchukuliwa kama ishara ya mtoto wa kiume ambaye ametanzwa na
matatizo, ambaye hajapewa hadhi anayostahili katika jamii, kama inavyoonekana
baadaye kwenye riwaya yenyewe.

b) Mbele ya picha ya mwanamume anayemzungumzia mvulana kuna uwanja


usiokuwa na mimea, pengine kutokana na uharibifu wa mazingira, jambo ambalo
pia linajitokeza ndani ya riwaya.

c) Mbele huko kuna miti ambayo imefunikwa na giza kiasi, ambayo inaweza
kuchukuliwa kuwakilisha matumaini yaliyonyimwa nafasi ya kujitokeza vizuri.

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

d) Nyuma ya miti kuna mlima mkubwa ulio na vilele (nguu) ambavyo vina
mwangaza juu. Hii inaweza kuchukuliwa kuwa ishara ya matatizo (mlima) na
suluhu inayopendekezwa na mwandishi ya kukabiliana na nguu (vikwazo) za tangu
jadi zinazotatiza maendeleo ya jamii.

e) Nyuma ya mlima kuna mwanga hafifu unaojitokeza. Mwanga huu unaweza


kuchukuliwa kuwa kiwakilishi cha matumaini mapya kwamba jamii
iliyokumbwa na matatizo mengi kwa muda mrefu hatimaye inapata mwanga, kama
inavyofanyika kwenye riwaya Lonare anapochaguliwa kuwa mtemi, jambo
linaloipa nchi ya Matuo matumaini mapya ya mabadiliko chanya.

Ufaafu wa Anwani: Nguu za Jadi


Nguu ni vilele vya milima. Katika riwaya hii, neno hili limetumiwa kisitiari, kuwakilisha
vikwazo au matatizo yanayokumba jamii inayozungumziwa. Kwa hivyo, Nguu za Jadi ni
vikwazo ambavyo vimekuwepo kama desturi au kanuni za maisha, na ambavyo
vinadumaza maendeleo ya jamii.
Mifano ya vikwazo hivyo kutoka katika riwaya ni: ✓ Mila ambazo zinawadunisha
wanawake na kuwanyima uhuru wa kujiendeleza. Mifumo ya uongozi mbaya
inayosababisha ufisadi, ukabila, utabaka, ubinafsi, hali ya kutowajibika, ufujaji wa
mali za umma, uharibifu wa mazingira, ukiukaji wa haki za watoto, ukatili na wizi wa
mali ya umma.
✓ Mifumo wa ubabedume uliokolea taasubi ya kiume wenye kudhalilisha wanawake
na watoto wa kike.
✓ Mila zinazomnyima mtoto wa kiume nafasi ya kujiendeleza. Mila hizi
zimemtelekeza mtoto wa kiume kwa kutothamini elimu na maendeleo yake.
✓ Umaskini uliokithiri.
✓ Matumizi na ulanguzi wa dawa za kulevya.
✓ Changamoto za ndoa na ukahaba.

Riwaya ya Nguu za Jadi kwa Muhtasari


Riwaya inapoanza, mhusika mkuu, Mangwasha, yuko na wanawe wawili, Sayore na
Kajewa, katika kanisa fulani, ambapo wanajificha. Nje ya kanisa hilo, wapo watu wengine
wa kabila la Waketwa, waliokimbilia usalama hapo baada ya makao yao katika eneo la
Matango kuchomwa.
Kuna fununu kwamba jamii ya Waketwa inafurushwa kutoka makwao kwa sababu kuna
watu fulani wanaotaka ardhi ya Matango kwa nguvu.
Mtemi Lesulia, kiongozi wa nchi, anachukia kabila la Waketwa kwani yeyeanatoka katika
kabila la Wakule. Waketwa na Wakule Wana uhasarna wa tangu jadi. Lonare, ambaye ni
kiongozi wa Waketwa, ana urnaarufu mkubwa nchini. Katika uchaguzi mkuu uliopita,
alitekwa nyara na kwa namna hiyo, Mtemi Lesulia aliishia kuchaguliwa bila kupingwa.

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

Mangwasha ni mwanamke mwenye bidii, na anafanya kazi ya uhasibu katika afisi ya Chifu
Mshabaha. Chifu huyu ni rafiki mkubwa wa Mtemi Lesulia, naye pia anawachukia
Waketwa. Hivyo, anapanza kuwadhulumu Waketwa, jambo ambalo Mangwasha
analifahamu kutokana na kufanya kazi naye. Chifu Mshabaha pia ni rafikiye Sagilu, mzee
anayetaka kumuoa Mangwasha licha ya kwamba anajua msichana huyu ana mchumba,
Mrima, na wanapanga ndoa. Siku ya harusi ya Mangwasha na Mrima, Sagilu anamtuma
kimada wake, Sihaba, akiwa na bomu lililofungwa kama zawadi kwa maharusi. Kwa bahati
nzuri, watu wanamshuku na maafa aliyokusudia kufanya hayafanyiki. Sagilu
anamnyemelea Mrima na kumzuga kwa kutumia pesa kiasi kwamba Mrima anaisahau
familia yake, huku akimwachia Mangwasha jukumu la kuwalea wana wao wawili.

Nchi ya Matuo inakumbwa na matatizo mengi. Kuna matatizoya kiuchumi


yanayosababishwa na uongozi mbaya na ufisadi uliokithiri. Mtemi Lesulia anaendeleza
ubaguzi dhidi ya Waketwa na vijana wengi walio na elimu hawapati kazi za kujiendeleza
kimaisha. Kwa mfano, uteuzi wa wagombea nafasi za uongozi ukiwa umekaribia, machifu
wanalazimishwa kuwahamisha Waketwa kutoka Matango ili viongozi wanaopendelewa na
mtemi wasipate upinzani, na yeye Mtemi Lesulia asishindwe na mpinzani wake mkuu wa
kisiasa, Lonare. Sihaba anatumwa kwenda kuhakikisha kwamba makazi ya Waketwa
yameteketezwa,

Anawatumia vijana ambao wanatumia petroli kuchoma makazi hap. Lonare na wafuasi
wake wamepeleka kesi mahakamani, na akiwa na wenziwe, kama vile Ngoswe,
wanawashawishi watu kurudi katika mako yao ya zamani kule Matango ambako
wanajenga mahema. Hata hivyo, siku ya tatu, vijikaratasi vinasambazwa kuwataka watu
watoke kwenye ardhi hiyo ambayo, inabainika, imetwaliwa na kupewa Nanzia, mkewe

Mtemi Lesulia, na rafikiye mtemi, Mbwashu. Hawa wanataka kujenga jengo la


kibiashara katika ardhi hiyo ya Matango. Watu wanaokuja kuanza ujenzi wanafukuzwa
na Waketwa walioamua kuitetea ardhi yao kwa vyovyote vile. Baada ya kuona
kwamba mpango wao umetibuka, Mtemi Lesulia anamtumia Sagilu kumpa Mrima
pesa nyingi pamoja na ahadi kwamba atapewa kazi serikalini, ilimradi amfanyie Mtemi
Lesulia kampeni na kuwaendea kinyume Waketwa.
Kipindi kifupi kabla ya uteuzi wa watakaopeperusha bendera za vyama mbalimbali, Sagilu
anatofautiana na mwanawe, Mashauri, baada ya mwanawe kugundua kwamba babake ana
uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake, Cheiya. Mtemi Lesulia naye anakosana na
mwanawe, Ngoswe, wakati anapanga njama ya kuvuruga zoezi la uteuzi ili kuwaharibia
wapinzani wake nafasi za kuteuliwa. Ngoswe anaona kwamba hatua ya babake
inaongozwa na ubinafsi wa kujitakia uongozi na kutojali kwamba baadhi ya watu huenda
wakapoteza maisha yao katika vurugu anazopanga. Sagilu anashindwa katika uteuzi na
inakuwa wazi kwamba Mtemi Lesulia atakuwa na upinzani mkubwa katika uchaguzi mkuu
ujao. Kwa ushawishi wake, Chifu Mshabaha anafutwa kazi na mtemi anaamua
kumwondokea Sagilu ambaye sasa anaandamwa na sheria kwa ufisadi alioendesha nchini.
Awali, tunaona Mangwasha akipoteza kazi yake katika afisi ya Chifu Mshabaha kwa
kujitokeza kama mpinzani wa serikali kwani anamfanyia Lonare kampeni, kando na
kwamba mara zote, hakumkubalia Sagilu ombi la kumtaka awe kimada wake. Sihaba
anatiwa mbaroni kwa kuendesha biashara haramu ya ukahaba inayosababisha wasichana
wengi kuharibika lakini anaachiliwa kutokana na ushawishi aliokuwa nao serikalini.
Mikasa hii inawaathiri wahusika wengi vibaya.

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

Sagilu anapatwa na kichaa na mkewe mtemi, Nanzia, anaugua baada ya jengo lake la
kibiashara la Skyline Mall kutwaliwa. Baada ya kulazwa hospitalini kwa muda, anafariki.
Kwa mara nyingine, Lonare anatekwa nyara kabla ya uchaguzi lakini anafaulu kutoroka na
kupata matibabu. Uchaguzi mkuu unafanyika na Lonare anachaguliwa kuwa mtemi.
Rafikiye Sagilu anashindwa na Mwamba anayechaguliwa kuwa mbunge wa Matango.
Lonare anawahutubia wananchi wa Matuo na kuahidi kuufufua uchumi wa nchi na
kukabiliana na ufisadi serikalini. Anaahidi pia kwamba serikali yake itashughulikia tatizo
la ukosefu wa ajira kwa vijana na kuhakikisha kwamba pana usawa wa kijinsia, akisema
kwamba Matuo imesambaratishwa na ubabedume. Anawaomba wananchi wenzake
kujiepusha na ukabila na kuwahimiza kukataa na kufichua maovu yanapofanyika nchini.
Lonare anachagua kutolipiza kisasi dhidi ya mahasidi wake wa kisiasa.
Sura ya Kwanza

Mangwasha yuko na wanawe katika kanisa fulani ambapo yeye na watu wa kabila lake la
Waketwa wamekimbilia usalama baada ya kuchomewa nyumba zao katika mtaa wa
Matango, jijini Taria. Kuna fununu zinazosema kwamba pana watu fulani waliotaka
kuitwaa ardhi ya Matango kwa nguvu. Inabainika pia kwamba mjini Taria, kuna jamii
mbili ambazo ni mahasimu wa tangu jadi, Wakule na Waketwa. Mtemi Lesulia, kiongozi
wa nchi, anatoka katika jamii ya Wakule na anawachukia Waketwa. Lonare ni kiongozi wa
Waketwa lakini ana umaarufu mkubwa nchini kote kwani katika uchaguzi mkuu uliopita,
alikuwa na sera bora zaidi. Hata hivyo, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi, alitekwa nyara
na Mtemi Lesulia kuchaguliwa bila kupingwa. Mangwasha anafanya kazi ya uhasibu
katika afisi ya Chifu Mshabaha. Anajua kwamba Chifu Mshabaha, ambaye pia
anawachukia Waketwa, anafanya mpango wa kuwadhulumu Waketwa. Kwa sababu hii,
anapanga kumwona kiongozi wake, Lonare, ili kumweleza njama zinazopangwa dhidi ya
watu wake.

Juhudi za Mangwasha, hata hivyo, zinatatizwa na hali kwamba jamii haimthamini


mwanamke, na anashangaa kama atasikilizwa. Anaamua atafanya tu alilokusudia, liwe
liwalo.

Masuala makuu yanayojitokeza katika Sura ya Kwanza

✓ Uhasama wa kikabila na kisiasa unajitokeza kwani Waketwa wanabaguliwa na


kupokwa haki zao za kumiliki ardhi na kuishi kwa amani. Waketwa wanalaumiwa hata
kwa mambo ambayo hayako katika uwezo wa binadamu kudhibiti, kama vile maradhi
sugu yanapowashinda madaktari. Kiongozi wa Waketwa, Lonare ameepuka kifo mara
nyingi, kifo kilichopangwa na Wakule.

✓ Ukabila ulioshamiri Matuo unawafanya Waketwa wengi kuwa katika tabaka la chini,
huku wakiwa na viongozi wachache sana serikalini.
✓ Mfumo wa ubabedume unawanyima wanawake nafasi ya kujiamini kama wahusika
sawa katika jamii. Mwanamke asiyekuwa na cheo au pesa hawezi kusikilizwa (uk. 8).
✓ Ufisadi umeshamiri katika jamii. Ardhi ya Waketwa inapotwaliwa, Chifu Mshabaha
anaangalia kando kwani ameshapokea mlungula (uk. 9).

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

✓ Maudhui ya bidii yanajitokeza kupitia kwa mhusika Mangwasha ambaye msimulizi


anasema alifunzwa kuuambaa uvivu (uk. 12).
Sura ya Pili
Mangwasha ni msichana mwenye bidii kazini, katika afisi ya Chifu Mshabaha. Anakutana
na Mrima, ambaye pia ni mwenye bidii, na kuchumbiana. Wanafanya mazoea ya kwenda
kula chakula katika mkahawa unaomilikiwa na Sagilu, mzee ambaye ni rafikiye Mtemi
Lesulia. Sagilu anamtaka Mangwasha kimapenzi na anapomkataa, anaweka kisasi dhidi
yake. Chifu Mshabaha pia anamchukia Mangwasha kwa kumchumbia mwanamume
asiyekuwa na pesa na kumkataa rafikiye, Sagilu, ambaye ni tajiri.
Siku ya harusi ya Mangwasha na Mrima, Sagilu anamtuma Sihaba, kimada wake, na bomu
ambalo linalipuka na kusababisha watu waliohudhuria sherehe kutawanyika. Baada ya
miaka kadhaa katika ndoa na kuwa na watoto wawili, Mrima anabadilika. Anaitelekeza
familia yake na kuingilia ulevi. Mangwasha anateseka sana na anapoamua kufuatilia
mumewe ili ajue ni nini kilichomfanya abadilike, anagundua kwamba anapewa pesa nyingi
na Sagilu, ambaye ni adui wa ndoa yao.
Masuala makuu yanayojitokeza katika Sura ya Pili ➢ Mangwasha, mhusika mkuu,
anajitokeza kama mwanamke jasiri na aliyejikomboa kiakili. Hathamini tamaduni
zilizopitwa na wakati, kama vile kulazimishiwa ndoa kwa misingi ya mali. Kwa msingi
huu, anamkataa Sagilu ambaye anatumia ushawishi wa hela kumtaka awe mwanamke
wake. Yeye ni mwenye mapenzi ya dhati, haliinayomfanya kumjali mumewe na kufuatilia
ili ajue ana tatizo gani linalomfanya kuingilia ulevi na kuitelekeza familia yake.
➢ Sagilu anasawiriwa kama mtu katili, anayehodhi bidhaa na kuziuza kwa bei za juu
wakati kuna uhaba wa bidhaa hizo. Aliwahi kuagiza maziwa ya watoto ambayo
yalihatarisha maisha yao. Kwa kuwa ana uhusiano wa karibu na Mtemi Lesulia, sheria
hazikumfuatilia katika suala hili, ishara ya ufisadi.
➢ Chifu Mshabaha anajitokeza kama mbaguzi na mpyaro. Anasema kwamba Waketwa
hawana akili (uk. 20).
➢ Ufisadi unajitokeza kwani polisi hawajishughulishi kumtia mbaroni mwanamke
anayekuwa na kilipuzi kwenye harusi ya Mangwasha.

➢ Sagilu ana kisasi na familia ya Mangwasha. Kwa sababu hiyo, anatumia pesa ili
kumtokomeza Mrima na kwa namna hiyo, kumsababishia Mangwasha na wanawe
mateso.
➢ Taasubi ya kiume inajitokeza kupitia mhusika Mrima ambaye anamwambia
Mangwasha kwamba hamzuii kuoa mke mwingine (uk. 41).
Sura ya Tatu
Waketwa ni watu wenye bidii. Hata hivyo, wengi wao wanaishia kufanya kazi duni na
wanabaguliwa kwa kila hali kwani utawala wa Mtemi Lesulia ni fisadi na unaendeleza
ubaguzi dhidi yao. Kuna matatizo ya kiuchumi yanayotokana na uongozi mbaya; vijana
waliosoma hawana ajira na wengi wao hawasomi kutokana na umaskini uliokithiri. Pia,
kuna uharibifu wa mazingira kutokana na mapuuza na kutojali kwa serikali.

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

Uhalifu pia umeongezeka na maadili kuwakimbia watu, hasa vijana. Lonare anamtembelea
Mangwasha. Tunafahamu kwamba machifu wamelazimishwa kuwahamisha Waketwa
kutoka Matango ili Mtemi Lesulia asipate upinzani katika eneo hilo, na Lonare
asichaguliwe, kwani wafuasi wake wengi wanaishi huko. Baadaye, Sagilu anamtembelea
Mangwasha usiku na kutaka kumhonga kwa pesa ili amkubali. Mangwasha anamfukuza na
kukataa Pesa zake. Usiku huo anapolala, anaota kwamba jinyama hatari linamfukuza na
mbele anakokimbilia anakabiliwa na moto mkubwa. Anapoamka, anatanabahi kwamba
Matango inateketezwa kwa moto na watu wanahangaika ovyo.
Masuala makuu

a) Maudhui ya bidii na kutobagua kazi yanasisitizwa katika sura hii. Waketwa


hawakuchagua kazi kama walivyofanya Wakule. Walifanya hata zile zinazofikiriwa
kuwa duni (uk. 43).
b) Ufisadi unajitokeza kwani watu wengi, hasa wa jamii ya Wakule, wanapata kazi
hata bila kuhitimu, jambo ambalo lina madhara makubwa, kama vile vifo
vinavyofanyika hospitalini ambako watu wasiosomea udaktari wanaajiriwa kufanya
upasuaji wa kimatibabu. Viongozi wa kijeshi pia wanatoka katika jamii ya Wakule
(uk. 44).
c) Uchafuzi wa mazingira pia umeangaziwa. Wananchi wanaathirika kiafya kutokana
na uchafuzi wa mazingira (uk. 46).
d) Umaskini unawafanya baadhi ya vijana kutopata elimu ya haja, huku wasichana
wakipata mimba za mapema na kukosa kuendelea na masomo (uk. 48-49).
e) Lonare anajitokeza kama kiongozi bora kwani anapigania elimu ya wasichana na
anataka kuongoza Matuo si kwa sababu ya mshahara tu bali kwa kuwa anawapenda
wananchi wenzake, kuonyesha kwamba yeye pia ni mzalendo.
f) Mwandishi ametumia jazanda ya jinyama na moto. Jinyama linalomkimbiza
Mangwasha ni Sagilu ambaye ni mzee asiyekuwa na maadili, nao moto ni
kiangazambele cha moto unaowachomea Waketwa makazi yao huko Matango.
Sura ya Nne
Sura hii inaanza asubuhi baada ya watu kukesha nje ya kanisa. Hii ni baada ya kufurushwa
kutoka Matango. Mangwasha na Mbungulu wanakutana na wanawake wengine ambao
wanaelezea kwamba usiku walipochomewa nyumba walikutana na vijana. Hawa walikuwa
na mageleni yaliyohanikiza harufu ya mafuta ya petroli. Vijana hao waliingia kwenye gari
jekundu lililoendeshwa na mwanamke fulani ambaye hawakuweza kumtambua.
Mkurugenzi wa ardhi mjini Taria anakuja mahali pale akiandamana na Chifu Mshabaha na
mwanamke aitwaye Mbwashu. Anawaahidi watu chakula, mablanketi na mahema ya
msaada. Watu wanakasirishwa na hatua ya kuwachukulia kama wakimbizi lakini
mkurugenzi huyo anasema kwamba chanzo cha moto uliowachomea makazi yao
hakijulikani kisha anaondoka. Watu wana hasira, hawataki kuishi mahali hapo; wako radhi
kwenda kukita mahema huko Matango.
Siku ya tatu baada ya kurudi Matango, vijikaratasi vinasambazwa kuwataka Waketwa
watoke sehemu hiyo. Watu wanakuja hapo kutaka kujenga ua ili kuzingira ardhi ya
Matango lakini wanafukuzwa na wenyeji, ambapo Sihaba anajeruhiwa. Huyu ndiye
aliyesambaza vijikaratasi vya kuwataka watu wahame eneo la Matango. Sagilu naye
ameshaonywa na Mtemi Lesulia kuhakikisha kwamba jalada halisi la ardhi ya Matango
halipatikani, kwani ardhi hiyo sasa ni mali ya Nanzia, mkewe mtemi, na Mbwashu.

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

Baadaye, Sihaba anamtembelea Chifu Mshabaha. Anamwachia barua zenye taarifa kuhusu
jengo la kibiashara ambalo linanuiwa kujengwa Matango. Kuna barua kutoka kwa Mtemi
Lesulia inayoeleza kwamba kipande hicho cha ardhi ni mali ya Nanzia na Mbwashu.
Mangwasha anazirudufisha barua zote na baadaye zinatumiwa kama ushahidi mahakamani
katika kesi inayohusu ardhi ya Matango. Mwamba, mwanasheria anayewakilisha Waketwa
katika kesi hiyo anashinda kesi kwa ushahidi huo. Mpango wa Mtemi Lesulia, Sagilu na
Chifu Mshabaha wa kuwafurusha Waketwa kutoka kwenye ardhi ya Matango unakosa
kufaulu.
Mtemi Lesulia anapanga njama nyingine. Kupitia kwake Sagilu, wanampa Mrima pesa
nyingi pamoja na ahadi ya kumpa cheo serikalini ikiwa atamfanyia kampeni Mtemi Lesulia
na kuwaendea kinyume Waketwa. Mangwasha anapata pesa hizi pamoja na barua yenye
ahadi alizopewa Mrima na anamtaarifu Lonare, Mwamba, Sauni na Sagura. Wanakutana
na Mrima na kufanikiwa kumweleza ukweli kwamba anatumiwa tu kisiasa, na kwamba
Mtemi Lesulia na Sagilu hawana mpango wowote wakumfaa. Wanakubaliana kurudisha
pesa alizohongwa nazo kwa Sagilu, ambaye wanamkuta akiwa kwenye mkutano pamoja na
wafuasi wake.
Masuala makuu

➢ Mangwasha na Lonare wanajitokeza kama wahusika waadilifu, wanarudisha pesa


zilizotumiwa kama hongo kwa Sagilu kutoka kwa Mrima. Aidha, ni wenye mapenzi
ya dhati kwa nchi na kwa watu wao. Wanamwokoa Mrima kutoka Majaani ambako
amedhoofikia kiafya.
➢ Chifu Mshabaha, Mbwashu, Sagilu, Mafamba na Mtemi Lesulia wanajitokeza kama
wahusika fisadi na katili kwani hawajali athari za vitendo vyao vya kifisadi kwa
wananchi. Mtemi Lesulia analinganishwa na mjusikafiri anayekula chakula cha
mchwa na mchwa wenyewe. Maelezo haya yanajenga jazanda ya utawala dhalimu
unaowaangamiza wananchi wake.
Sura ya Tano
Nchi ya Matuo inakaribia uteuzi wa viongozi. Sagilu, aliyekuwa na matumaini makubwa
ya kupata uteuzi wa kugombea uongozi wa Matango anapata msururu wa mapigo. Ana
uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wa mwanawe, Mashauri, aitwaye Cheiya. Mashauri
anapogundua jambo hili anamchukia babake hata kumkana. Zaidi ya hayo, anajiunga na
kundi linalomuunga mkono Lonare na Mwamba, ambao wanawania kiti cha mtemi na
uongozi wa eneobunge la Matango mtawalia. Mashauri ni rafikiye Ngoswe, mwanawe
Mtemi Lesulia. Ngoswe anafahamika zaidi kama mlanguzi mkubwa wa dawa za kulevya,
kando na kukusanya ushuru kutoka katika mashamba yånayomilikiwa na wazazi wake.
Cheiya anatoka
katika familia ya kimaskini lakini baada ya elimu yake na kukutana na Mashauri,
anakengeuka na kuanza kuhusudu pesa, na hii ndiyo sababu anashawishiwa na Sagilu kwa
urahisi.
Baada ya mtemi Lesulia kujua kwamba mwanawe Sagilu anamuunga mkono Lonare,
anapanga njama ya kuzua vurugu wakati wa uteuzi ili Lonare asipate kuteuliwa akaishia
kushindana naye. Anafanya hivi pia ili Sagilu achukue uongozi wa Matango. Ngoswe
hamuungi babake mkono katika azimio lake. Anashangaa ni kwa nini babake yuko radhi
watu wapoteze maisha yao ili yeye na rafiki yake watwae uongozi. Yeye pia anaasi na
kujiunga na Mashauri katika kumuunga mkono Lonare.

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

Baada ya uteuzi kufanyika, Sagilu anashindwa na mpinzani wake, Mwamba. Jambo hili
linamuudhi Mtemi Lesulia ambaye anaamua kuacha sheria ifuate mkondo wake, kwani
mara zote amekuwa akiwalinda marafiki zake dhidi ya sheria, hasa Sagilu ambaye ni fisadi
mkubwa. Kufuatia hili pia, Chifu Mshabaha anafutwa kazi na waziri anayehusika na
masuala ya utawala.
Mangwasha anafutwa kazi kwa kuwa anamuunga mkono Lonare ambaye ni mpinzani wa
Mtemi Lesulia. Analazimika kujiunga na mumewe katika kuendeleza biashara kwenye
duka lao. Mangwasha anamwonea huruma mtoto wa kiume kwani ameishia kutelekezwa
huku jamii ikimwangazia zaidi mtoto wa kike. Hivyo, kwa msaada wa mashirika
mbalimbali, anafungua afisi mjini Taria ili kuwashughulikia vijana hao, ambao aliona
wanaendelea kuangamia taratibu.
Sihaba, ambaye anaendesha biashara ya ukahaba, anakamatwa na majengo anayoendelezea
biashara hiyo yanafungwa. Miezi minne baada ya kushindwa katika uteuzi, Sagilu
anapatwa na kichaa. Mkewe Mtemi Lesulia, Nanzia, naye anapatwa na msongo wa
mawazo na kulazwa hospitalini, baada ya kupokonywa jengo la kibiashara la Skyline Mall.
Ugonjwa wake unamsababishia kifo. Hata hivyo, kabla hajafa, anamweleza Ngoswe
kwamba yeye ni mtoto wa Sagilu, wala si mwanawe Mtemi Lesulia. Hali ya Sagilu
inaendelea kuwa mbaya hospitalini. Mwishowe anamwomba mwanawe, Mashauri,
msamaha kwa kumwendea kinyume. Mashauri anamsamehe. Mali ya Sagilu inatwaliwa na
serikali kwani aliipata kwa njia ya ufisadi. Wakati huu pia inafahamika kwamba Cheiya
alitumiwa kumtilia Lonare sumu kwenye kinywaji chake. Anakamatwa na kupelekwa
kwenye kituo cha polisi.
Masuala makuu

a) Suala la ukengeushi linaangaziwa katika kisa cha Sagilu na Cheiya. Sagilu kuandamana
na msichana wa umri wa Cheiya ni kuonyesha hali ya kutojiheshimu na kutojali
maadili.
Cheiya, kwa upande mwingine, yuko tayari kujishusha hadhi kwa kuandama pesa.
Ukengeushi pia unajitokeza pale ambapo mmoja wa wasichana wanaofanya ukahaba
kwa Sihaba anasema, za kutununulia chakula, nguo au hata vipodozi?" (uk. 142). Kauli
hii inaashiria kwamba wasichana hawa wamekengeuka kiasi kwamba hawathamini
kazi kama njia halali ya kujitafutia riziki.

b) Suala la malezi mabaya pia linajitokeza katika sura hii kwani Ngoswe ni mwana
kindakindaki aliyeengwaengwa na kudekezwa kupita kiasi (uk. 122). Yeye anaendesha
biashara ya kulangua dawa za kulevya na babake, Mtemi Lesulia, anamlinda kiasi
kwamba hata wakuu serikalini hawawezi kumkamata (uk. 122-123). Sifa ya Sagilu
kama mtu fisadi inajitokeza. Anashirikiana na mwanawe kuifisidi nchi kwa kushiriki
biashara ya vipusa na meno ya ndovu, na Mashauri anaposhtakiwa, kesi zenyewe
zinazimwa kabla ya kuanza (uk. 127).
c) Hatua ya Ngoswe na Mashauri kuungana katika kumpigia kampeni Lonare inaashiria
uwezo wa vijana katika kuchangia mabadiliko chanya katika jamii.
d) Ujasiri wa Mangwasha unaendelea kuonekana katika sura hii. Anapokabiliana na Chifu
Mshabaha baada ya kupoteza kazi yake, anamwambia chifu huyo kwamba yeye na

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

wengine wanaotaka mabadiliko watazibomoa hisia zao za ukabila, ubinafsi na chuki


(uk. 136).
e) Tatizo la umaskini uliokithiri linawafanya watu kufanya mambo kinyume na maadili ya
kijamii. Kwa mfano, baadhi ya wazazi wanawakubalia wana wao wa kike kushiriki
ukahaba kama njia ya kujitafutia riziki (uk. 143).
f) Kufutwa kazi kwa Chifu Mshabaha, kukamatwa kwa Sihaba, Nanzia kupoteza _jengo
la Skyline Mall na hatimaye kufariki, na Mangwasha kuanzisha afisi ya kushughulikia
mtoto wa kiume ni hatua muhimu katika ujenzi wa jamii mpya, jamii inayozingatia
maadili na kuwajali watu.
g) Kupitia mawazo ya Mangwasha, tunapata kuelewa falsafa ya mwandishi kuhusu
maisha: kila mtu ni mhusika mkuu katika kisa cha maisha yake mwenyewe, na jambo
la muhimu ni mhusika huyo kuipa hadhira yake kitu cha kuwatia moyo maishani.
Sura ya Sita
Siku chache kabla ya uchaguzi mkuu, Lonare anaripotiwa kupotea. Hata hivyo, wafuasi
wake wanaamua watampigia kura, awepo au asiwepo. Hii ni licha ya Mtemi Lesulia
kusema kwamba kiti cha mgombea nafasi ya mtemi katika Chama cha Ushirika kifutiliwe
mbali kwani Lonare mwenyewe hayupo.
Asubuhi ya siku ya uchaguzi mkuu, Lonare anapatikana ametupwa nje ya nyumba ya
Mangwasha akiwa katika hali mahututi. Wafuasi wake waliokuwa wameishiwa na
matumaini wanajitokeza kwa wingi kwenda kumpigia kura huku mwenyewe akipelekwa
hospitalini. Akiwa hospitalini, anamshauri Ngoswe kuacha biashara ya mihadarati kwani
kwa kufanya hivyo, atakuwa anaokoa kizazi kizima kutoka katika maangamizi. Lonare
anamshauri pia kuacha biashara nyingine haramu anazofanya na kujitanibu na mitandao
inayoendesh biashara hizo. Lonare anachaguliwa mtemi wa nchi ya Matuo. Baada ya
ushindi huu, anaihutubia nchi. Anaahidi kufufua uchumi wa nchi na kukata mirija ya
ufisadi. Anaahidi pia kwamba serikali yake itashughulikia ukosefu wa ajira kwa vijana.
Isitoshe, anaahidi kwamba atahakikisha kuwa kuna usawa wa kijinsia nchini huku akisema
kwamba Matuo imesambaratishwa na mfumo wa ubabedume. Anawaomba wananchi
wenzake kuepuka ukabila na kufichua maovu yanapofanyika nchini. Anaamua
kuwasamehe maadui wake wa kisiasa.
Masuala makuu

✓ Ujumbe wa kutokata tamaa katika maisha unajitokeza katika sura hii. Licha ya kwamba
Lonare amenyanyaswa sana na utawala wa
✓ Mtemi Lesulia, hakati tamaa. Wafuasi wake pia hawakati tamaa katika azimio lao la
kumchagua kama mtemi. Hii ndiyo sababu wanaamua kumpigia kura tu, awepo au
asiwepo.
✓ Katika hotuba yake Lonare, ni wazi kwamba serikali atakayounda itakuwa serikali bora
kwani ufisadi utamalizwa na umaskini kushughulikiwa, sawa na suala la Vijana na
ajira. Ni dhahiri kwamba mambo haya yakishughulikiwa, Matuo itakuwa nchi thabiti
zaidi.
DHAMIRA
Dhamira ni shabaha au lengo kuu la kazi ya fasihi.

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

1) Katika riwaya ya Nguu za Jadi, mwandishi anakemea ukabila uliosakini katika


jamii na unaodumaza maendeleo ya nchi. Anadhamiria kutuonyesha pia jinsi
ufisadi unavyoweza kubomoa asasi za kijamii na kufukarisha wananchi kiasi cha
kutoweza kujiendeleza kimaisha. Mwandishi anatumia taswira mbalimbali
kutuonyesha jinsi ufisadi unavyoweza kusambaratisha uchumi wa nchi hasa pale
unapochangiwa na uongozi mbaya.
2) Mwandishi anadhamiria kutoa tahadhari dhidi ya kuwapuuza na
kutowashughulikia watoto na vijana ambao hasa ndio dirisha la matumaini ya nchi
katika siku zijazo. Utelekezwaji wa vijana na udunishwaji wa haki zao ni taswira
inayojitokeza na kubainisha dhahiri dhamira ya mwandishi.
3) Ugandamizwaji wa haki za wanawake na umuhimu wa asasi ya ndoa pia ni dhamira
inayojitokeza katika riwaya hii mbali na ukombozi unaochochewa na uzalendo
miongoni mwa wanajamii.
Falsafa ya Mwandishi wa Nguu za Jadi
Falsafa ni msimamo au mawazo yanayomwongoza mtu binafsi (kwa mfano,
mwandishi) katika maisha yake, na ambayo yanaweza kutumiwa pia kama nasaha kwa
wasomaji au wasikilizaji wake, na jamii kwa jumla kupitia usomaji wa kazi fulani.
Yafuatayo ni baadhi ya mawazo ambayo yanaweza kuchukuliwa kuwa falsafa au msimamo
wa mwandishi kuhusu mambo mbalimbali katika maisha.

1) Mwandishi anaamini kwamba wanawake hawafai kufungwa na mila kiasi kwamba


hawawezi kupata haki zao katika maisha. Mangwasha anamwambia Mbungulu
kwamba mila isiyomruhusu mke kumtafuta mumewe kwenye starehe zake ni mila ya
kishenzi (uk. 32). Hiyo ni kumaanisha kwamba wanawake hawafai kukaa na kusubiri tu
mpaka pale mwanamume anapokuwa karibu ili wafanye maamuzi muhimu yanayohusu
maisha yao.
2) Mwandishi anapendekeza kwamba baadhi ya tamaduni za jadi zitupiliwe mbali kwani
zimekwishapitwa na wakati. Miongoni mwa tamaduni hizo ni tamaduni zinazomtweza
mwanamke kuonekana kama mtumwa wa mumewe. Badala yake, mwanamke katika
ndoa anapaswa kuonekana kama mwenza (uk. 42).
3) Mwandishi pia anaamini katika tabia ya kutochagua kazi, na mazoea ya kufanya bidii.
Kwa tabia yao ya kufanya kazi kwa bidii na kutochagua kazi, Waketwa wanapiga hatua
sana kimaendeleo (uk. 43).
4) Mwandishi anashikilia hoja kwamba fahari ya binadamu haitokani na kutoanguka
katika maisha, bali inatokana na kuinuka kila anapoanguka (uk. 48).
5) Mwandishi anaelekea kusema kwamba kwa uthabiti wa jamii, mtoto wa kiume
anahitaji sana uwepo wa mzazi wa kiume pia ili mtoto huyo apate mafunzo muhimu
yatakayomsaidia kukua na kujiendeleza inavyofaa (uk. 139). Mtoto wa kiume
anaangamia kwa kutelekezwa kutokana na makini yote ya jamii kuelekezwa kwa mtoto
wa kike.
6) Kupitia kwa mhusika Mangwasha, mwandishi anaelekea kusema kwamba binadamu
anapokuwa hai, ni muhimu kufanya jambo kwa faida ya jamii, kitu kitakacholeta
matumaini katika maisha yao. Mangwasha anajishughulisha na kuboresha maisha ya
mtoto wa kiume ambaye aliona kwamba mustakabali wake haukuwa na matumaini (uk.
164).

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

MAUDHUI
Maudhui ni ujumbe wa jumla unaojitokeza katika kazi ya fasihi. Aidha, maudhui ni
mafunzo ambayo huweza kupatikana katika kazi ya kisanaa kama vile riwaya, na sehemu
ya maana ambayo aghalabu huingiliana namada. Riwaya ya Nguu za Jadi ina maudhui
mbaljmbali yanayojitokeza na ambayo yanajenga dhamira za mwandishi. Kutokana na hali
kwamba riwaya hii ina maudhui changamano, ni vyema kwa msomaji kubaini maudhui
mengine zaidi mbali na yale yaliyofafanuliwa humu.
Ukabila
Ukabila ni hali ya kupendelea mtu, watu au Jamii fulani kutokana na misingi ya kabila.
Upendeleo huu huweza kuhusisha mambo mengi kama vile ajira, elimu, makazi, vyeo, na
kadhalika. Katika riwaya hii,

1) Wakule ni jamii inayoonyesha ukabila; wao ndio wengi serikalini (uk. 43) kutokana na
hali kwamba Mtemi Lesulia ambaye ndiye kiongozi wa nchi ya Matuo anatoka katika
jamii hii. Wakule wengi hasa walio matajiri wanajibagua na kuishi katika mtaa wa
Majuu ambao ni mtaa linamoishi tabaka tawala.
2) Kazi za madaraka ziliwaendea Wakule ilhali zile za daraja la chini kama vile kazi za
mikono zilifanywa na Waketwa.
3) Ukabila unasababisha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana kutoka katika jamii ya
Waketwa ambao ni wahitimu wa viwango mbalimbali vya elimu na taaluma.
4) Siasa za majina zinatawala (uk. 45) na ukabila unafanya watu wasiohitimu katika
taaluma mbalimbali kuajiriwa na kusababisha maafa nchini. Watu wanaajiriwa
kutokana na uchunguzi wa majina yao. Majina yanakuwa kigezo cha kupimia ajira.
5) Ukabila unamkolea mtemi kiasi cha kukosa imani ya kuajiri wanajeshi kutoka katika
jamii nyingine. Kwa mfano, marubani wanaangusha ndege na manahodha wanapasua
vyombo miambani kwa kukosa ujuzi (uk. 44).
6) Dhuluma za Chifu Mshabaha kwa Mangwasha zinatokana na ukabila. Chifu
anadhihirisha hisia za kikabila anaposema "...Waketwa ni watu wasio na akili hata ya
kuchagua wachumba." (uk. 20).
7) Chifu Mshabaha anamfanyisha Mangwasha kazi nyingi hata zile zinazopaswa
kufanywa na matopasi.
8) Chuki ya Mtemi Lesulia kwa Lonare inatokana na ukabila hasa pale anapohujumu
biashara yake, kumwonea Lonare gere na hata kumpangia mauti (uk. 51-52, 171).
9) Maneno ya Sagilu pia yamebeba hisia za ukabila hasa pale ambapo anawachukua
Waketwa kama watu wasioweza kufanya lolote. Anasema, "Ndege mliolelewa
kizimbani nyie hamwezi kuruka. Mtawezaje kuruka ilhali mnaishi mkifikiria kwamba
kuruka ni ugonjwa?" (uk. 176).
10) Ukabila unafanya wenyeji wa Matango ambao ni Waketwa kuchomewa nyumba zao na
kufurushwa ili wakati wa uchaguzi wa kisiasa wasimpigie mmoja wao kura.
11) Mtemi Lesulia anaendeleza hisia za ukabila anapowaita Waketwa panya (uk. 78).
12) Kufutwa kazi kwa Mangwasha pia kunatokana na ukabila (uk. 135-137) kwani tunaona
anayeajiriwa kuchukua mahali pake ni Mkule.

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

Utabaka
Utabaka ni hali inayosababisha jamii kujibagua katika makundi hasa mawili; matajiri na
maskini au wenye mali na vyeo na wasio navyo.

a) Utabaka unaonekana katika jumuiya inayozungumziwa (uk. 7). Nchi ya Matuo


inazingatia utabaka. Kuna tabaka la juu linalohusisha wakwasi, matajiri na wakuu
wa serikali ambao pia wamejitenga na kuishi katika mtaa wa kifahari uitwao Majuu
(uk. 7 na uk. 51).
b) Wananchi wa kawaida wanaishi katika mitaa ya matabaka ya chini na yale ya kati
kama vile Majengo, Matango na Majaani. Hawa wanahusisha wanaofanya kazi
viwandani, mashambani, makarani, matarishi, matopasi au vibarua wanaofanya
kazi za shokoa.
c) Tunaarifiwa nchi ya Matuo ilishikilia utabaka (uk. 45), "...matajiri wakawa wenye
nchi na wananchi wakasalia kuwa wana wa nchi". Maudhui ya utabaka
yanaonyesha kuwa tabaka la juu ndilo lililomiliki nyenzo za uzalishaji mali na ndilo
lililohujumu dhamana na hawala za serikali. Tabaka hili linahusisha watu kama vile
Mtemi Lesulia, Sagilu, Nanzia, Mbwashu, hata Ngoswe, mwanawe mtemi ambaye
anaishi katika kasri la kifahari.
d) Maudhui ya utabaka pia yanabainika kupitia mhusika Mangwasha anaposhangaa
kumwona Mbwashu akiwasili pale kanisani kwa gari aina ya Land Rover
kumaanisha kwamba hadhi yake haimruhusu kutumia gari kama lile (uk. 68).
Aidha, mke wa Mtemi Lesulia naye anawasili pale kwa gari aina ya Pick Up (uk.
71).
e) Tunamwona Cheiya akitamani maisha ya kifahari kutokana na utabaka uliokuwepo.
Anafanya usuhuba na Mashauri anayeishi mtaa wa Majuu naye akapata kuishi huko
(uk. 118).
f) Maudhui ya utabaka pia yanaendelezwa na mhusika Mashauri anayesimulia kuhusu
kisa cha mfalme wa Ufaransa na malkia wake kwenye karne ya 18. Raia waliishi
katika umaskini huku tabaka la mfalme likiishi maisha ya kitajiri (uk. 148-149).
Uongozi mbaya
Maudhui ya uongozi mbaya yamegawika kuwili; uongozi mbaya serikalini na katika
familia.

1) Uongozi mbaya serikalini unaonekana kupitia kwa Mtemi Lesulia ambaye alitawala
kwa mkono wa chuma na 'kauli alizotoa zilichukuliwa kama sheria za nchi' (uk. 7).
2) Mtemi anaonekana kuogopewa na raia wake na hili linabainika pale Mrima
anapomkanya mkewe asijaribu kukutana na mtemi kumaanisha kwamba si mtu mzuri,
na raia walimwogopa (uk. 8). Mtawala hapaswi kuogopewa na raia wake bali
kuheshimiwa.
3) Uongozi mbaya pia unaonekana kupitia kwa kiongozi huyu ambaye anashirikiana na
raia wake kuwanyanyasa raia wengine kwa kuwachomea makazi yao (Waketwa). Hii ni
ishara

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

ya uongozi mbaya wa kutenga na kubagua raia kwa sababu ya ubinafsi unaotokana na


siasa za ubaguzi na chuki.
4) Uongozi mbaya unaendelezwa pia na Chifu Mshabaha; kumnyanyasa Mangwasha
kazini na kutojali kazi nyingi anazotekeleza katika afisi yake.
5) Uongozi mbaya unaendelezwa pia kupitia kwa uteuzi mbaya wa viongozi katika
serikali ya Mtemi Lesulia; Sagilu anapewa cheo kikubwa lakini kinamfaidi yeye binafsi
ilhali mwanasheria, Mafamba, anayehudumia serikali anahujumu uchumi wa nchi
kupitia kwa kesi zisizozingatia maadili na sheria za nchi.
6) Maudhui ya uongozi mbaya yanaonekana kupitia kwa viongozi wa nchi wanaoruhusu
matendo maovu kama vile ufisadi na uporaji wa rasilimali ya umma ushamiri.
7) Uongozi mbaya unaonekana pale ambapo serikali haina mipango yoyote ya kuimarisha
ajira kwa vijana wanaohitimu katika Shule na vyuo wala kuweka mikakati ya
kuwakinga dhidi ya dhoruba za maisha. Wasichana wadogo wanahangaika mijini huku
wakizalishwa wakiwa na umri mdogo na vijana wa kiume wakihangaika mijini bila
ajira.
8) Ijapokuwa Mtemi Lesulia alikuwa ameshinda kiti cha mtemi wa nchi mara
mbili,hakubadilisha sera za uongozi wala kuweka mikakati ya kushughulikia ukosefu
wa ajira na kuimarisha uchumi au kutokomeza ufisadi nchini.
9) Uongozi mbaya katika serikali unasababisha mafunzo hafifu ya wataalamu katika
mfumo wa elimu. Wataalamu wasiohitimu vyema kama vile marubani na manahodha
wanasababisha maafa safarini kutokana na uongozi usiojali hitimu za watu. Serikali
inawaajiri walimu na madaktari wasiohitimu (uk. 44) huku vijana waliohitimu
wakikosa ajira.
10) Maudhui ya uongozi mbaya pia yanaendelezwa kupitia kwa mtemi wa nchi pale
anaposhirikiana na wezi wa mali ya umma, walafi na wabinafsi kuihasiri nchi. Katika
uk.
78, kwa mfano, Mtemi Lesulia anamwambia Sagilu ahakikishe jalada la ardhi
halipatikani anaposhirikiana naye kuwapoka Waketwa ardhi yao.
11) Tunaarifiwa pia kwamba mtemi hakutafakari ili kujua maana ya uongozi kwa raia
wake. Nyenzo za uongozi wa nchi tunaona zikimilikiwa na matajiri wachache
wanaoshabikia wizi wa mali ya umma. "Uchumi wa nchi ulikuwa ukisambaratika kwa
kasi kutokana na uongozi mbaya wa Mtemi Lesulia." (uk. 51).
12) Maudhui ya uongozi mbaya pia yanaendelezwa kupitia kwa Mtemi Lesulia na familia
yake. Hakuweza kumpa mwanawe, Ngoswe, uongozi aliostahili katika malezi yake. Hii
ndiyo maana Ngoswe anashiriki ulevi, ufuska na kujihusisha na biashara haramu ya
dawa za kulevya. Maudhui ya uongozi mbaya pia tunayaona kupitia kwa familia ya
Mrima. Hakuweza kuwaongoza vyema watoto wake kutokana na ulevi hadi
wakamsahau kama mzazi wao.
Ufisadi
Ufisadi umejitokeza kwa njia mbalimbali kupitia kwa baadhi ya wahusika na unachukua
sehemu kubwa katika riwaya hii.

1) Kutozingatia ujuzi, maarifa au taaluma ya mtu katika ajira kunasababishwa na


ufisadi.Serikali ya Mtemi Lesulia inawaajiri watu wasiokuwa na ujuzi wala maarifa
huku walio na uwezo huo wakiachwa (uk. 44). Tunaambiwa ajira zinatolewa

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

kibubusa na kwa kujuana hasa katika misingi ya ukabila. Hali hii inasababisha
hujuma katika uajiri na kuzorotesha uchumi wa nchi.

2) Ufisadi unasababisha ukiukaji wa maadili ya kifamilia kwani tunaona mauaji ya


kifamilia yakikita mizizi. "Mume anamgeukia mke na kumchinja, naye mke akafanya
vivyo hivyo." (uk. 47).
3) Taasisi na mashirika ya serikali yanamilikiwa na mitandao ya wezi na hivyo kuipoka
nchi hadhi yake (uk. 47). Rasilimali ya nchi inafujwa na watu walioshabikia wizi.
4) Polisi nao wanaendeleza ufisadi pale wanapowatoza madereva wa Lonare faini
zisizoeleweka; pale Lonare anapohangaishwa na polisi kwa makosa madogomadogo;
kupokonywa leseni, na kadhalika.
5) Maudhui ya ufisadi yanajitokeza pale kundi la mabwanyenye linapohujumu dhamana
na hawala za serikali.
6) Upokeaji hongo unaonekana pale watu waliotumwa kumkatizia Lonare maisha
walipomjia na kumwonyesha pesa walizopewa na maadui zake ili kumuua.
7) Kitendo cha Sagilu kujaribu kumhonga Mangwasha kwa pesa ili afaidi penzi lake pia
ni kitendo cha ufisadi (uk. 60).
8) Kauli ya Mtemi Lesulia ya kuamuru jalada la ardhi ya Matango kufichwa
inadhihirisha ufisadi (uk. 78). Alitaka kuwaondoa Waketwa wasimpigie kura Lonare
au Mbaji wakamshinda yeye au Sagilu. Alitaka pia kufyeka uwanja ili
9) Nanzia na Mbwashu wamiliki ardhi hiyo huku wakisema ardhi hiyo ilikuwa
imetengewa ujenzi wa soko. Hivi vyote vinaashiria ufisadi.
10) Ufisadi unaonekana pale Sagilu na Sihaba wanapojaribu kumshawishi Mbaji kwa kila
njia ili asimfanyie Lonare kazi (uk. 98).
11) Maudhui ya ufisadi yanaendelezwa na mtemi na jamaa yake pamoja na marafiki zake
wanapojaribu kuwapoka Waketwa ardhi ya Matango kwa njia zisizo halali. Hongo
inatolewa kwa Chifu Mshabaha, Sagilu na Sihaba katika mchakato huo.
12) Kitendo cha.kuwachomea wenyeji wa Matango nyumba na kuwafurusha kinatokana
na ufisadi kwani kuna vijana waliohongwa kutekeleza uhalifu huo.
13) Sihaba anapotumiwa na Sagilu kusambaza vijikaratasi kuwataka Waketwa wahame
kutoka Matango ni hujuma inayotokana na ufisadi.
14) Maudhui ya ufisadi pia yanaendelezwa na taasisi ya magereza kwani tunaona milango
ya gereza ikifunguliwa ili wahalifu kama vile Sihaba watoke (uk. 85).
15) Ufisadi pia unaendelezwa kupitia wahusika kama vile Mbwashu na Sagilu
wanaotumia njia haramu kuagiza bidhaa ghushi nchini na kukataa kulipa ushuru
mbali na kutoa mlungula bidhaa hizo ziliposhikwa na maafisa wa forodha (uk. 68).
16) Tashbihi inayotolewa ya kumlinganisha Mtemi Lesulia na mjusikafiri juu ya
kichuguu inapiga mwangwi ufisadi uliokuwepo katika serikali yake (uk. 93). Utawala
wake unafisidi pato la nchi linalotokana na jasho la raia wake.
17) Maudhui ya ufisadi yanaendelezwa pia na mwanasheria Mafamba. Huyu anashiriki
ufisadi pale anapoficha siri za watawala kwa kutoa habari za uongo mbele ya korti
kuhusu vyeti ghushi vya ardhi iliyomilikiwa na wenyeji wa Matango. Ufichuzi wa
mwanasheria Mwamba unaweka bayana ufisadi unaohusishwa na ardhi ya Matango
(uk. 95).

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

18) Ulevi wa Mrima unatokana na upotovu wa maadili ambao chanzo chake ni Sagilu.
Kupitia kwa hila za Sagilu, Mrima anatoweka nyumbani kushiriki ulevi kwa kupewa
pesa ili aiharibu ndoa yake na Mangwasha.
19) Mrima anapokea mlungula kutoka kwa Sagilu ili kuhujumu kampeni ya Lonare na
kumuunga mkono Mtemi Lesulia (uk. 105-114).

20) Ufisadi unabainika Lonare anapomwambia Sagilu, "Nimekuja kukukabidhi mlungula


huu uliokuwa umempa Mrima." (uk. 116).
21) Maudhui ya ufisadi yanaendelezwa na mhusika Ngoswe anaposhiriki katika biashara
haramu ya dawa za kulevya ambazo 'zilisambazwa nchini kwa siri' (uk. 123).
Ijapokuwa sheria kali zilipitishwa nchini kuhusu dawa hizo, hazikuzingatiwa
kutokana na ushawishi wa mabwanyenye waliohujumu sheria za nchi kwa manufaa
yao binafsi.
22) Kupitia kwa Mashauri pia, ufisadi unaendelezwa pale anaposhirikiana na Sagilu
kufisidi vipusa na meno ya ndovu (uk. 127).
23) Ufisadi unayawezesha mashtaka yaliyofikishwa kortini kuzimwa hata kabla ya kesi
kuanza.
24) Mtemi na Sagilu wanatumia vishawishi vya pesa kuwahonga vijana ili wazue vurugu
na kuharibu kura za mpinzani wa Sagilu katika eneo la Matango (uk. 128).
Utamaduni
Utamaduni ni ujumla wa maisha ya watu. Aina mbili za maudhui ya utamaduni
zinajitokeza katika riwaya hii.
Kuna utamaduni wa kiasili ambao unazingatia jadi na desturi za kiasili za jamii
zinazozungumziwa, na ule unaokumbatia usasa. Huu ni ule utamaduni unaotokana na
maisha ya kimji na athari zake ambazo zinachukua sehemu kubwa ya maudhuihaya. Kwa
ujumla wake, jumuiya inayozungumziwa ni ile inayozingatia mfumo wa kuumeni. Huu ni
mfumo unaompa mwanamume nguvu na mamlaka zaidi ya mwanamke. Mfumo huu
unajulikana pia kama mfumo wa ubabedume ambao humweka mwanamume katika nafasi
ya juu kijamii akilinganishwa na mwanamke. Mfumo huu pia unagawanya majukumu
tofauti baina ya mwanamume na mwanamke kulingana na jinsia yao. Hali kama hii
tunaiona pale Mangwasha anapotamani kuondoa uhasama wa Wakule na Waketwa lakini
kwa vile yeye ni mwanamke, hangeweza kusikilizwa. Jamii yake pia haimtarajii yeye kuwa
na ujasiri wa kwenda kuongea na wakuu wa nchi na Sio tu kwa sababu ya hali yake ya
kijamii lakini pia kutokana na hali ya kuwa yeye ni mwanamke (uk. 8).
Dhana ya kwamba mwanamke ni chombo tu cha kuchuuzwa na mwanamume inajitokeza
katika uk.10 pale ambapo baadhi ya Waketwa waliochomewa nyumba zao wanatoa hoja
kuwa kuna wale waliowauza wake zao kwa wakuu ili wapate ajira.
Wanawake hawana sauti mbele ya wanaume kama anavyowaza Mangwasha kuwa
"...walipaswa kusikiliza na kutenda bali si kusikilizwa na kutenda." (uk. 11). Maudhui
haya yanaendelezwa pia na mhusika Mangwasha tunapojulishwa kuwa utamaduni
uliomlea ulimfunza kutotumia sifa za kike kustarehesha wanaume ili kujinufaisha
kimaisha.

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

Utamaduni unamfunza mke kujitegemea katika maisha bali si kumtegemea mume kujikimu
katika maisha yake (uk. 12). Udanganyifu ili kufaidi kitu pia hauvumiliki kwa mwanamke
na mila inayozingatiwa na jamii inabainishwa vyema na mhusika Mbungulu anaposema,
"Usimfuate mumeo kwenye makao ya starehe." (uk. 32).
Maudhui ya imani asili ya jamii pia yanakaririwa na Mrima anayeamini kuwa mwanamke
huwa na maneno mengi kama chiriku (uk. 40) na kwamba mke hapaswi kumuuliza
mumewe kule aendako au atokako. Mrima anasema, "...wanawake wa kisasa wanavunja
kila mwiko uliowekwa na wazee." (uk. 40). Mifano anayotoa Mrima ya 'ngamia kumea
pembe' au 'shingo kupita kichwa' ni ishara kamili ya jinsi utamaduni asilia unavyomfunza
mwanamume kuhusu mwanamke kumaanisha daima mwanamke hawezi kumpiku
mwanamume.
Kupitia kwa Mrima pia, maudhui ya jinsi utamaduni asilia unavyosawiriwa katika riwaya
yanaonekana pale anaposema kuwa yeye ni mwanamume na mke hangemzuia kuoa;
kwamba angeweza kuoa wakati wowote na idadi yoyote ya wanawake. Katika jamii nyingi
hasa barani Afrika, wanaume huweza kuoa zaidi ya mara moja na hii ni desturi kongwe
miongoni mwa jamii nyingi.
Utamaduni asilia pia unamtaka mume aweze kuitunza jamaa yake pamoja na kuisimamia.
Hii ndiyo maana Mrima anasisitiza kuwa mila haimruhusu kutunzwa na mkewe. Anasema,
"Siwezi kuvunja mila kwenda kutunzwa kama mtoto." (uk. 101). Haya yanakaririwa na
Sagilu anapomuuliza Mangwasha kwa nini hajamwambia ampe Mrima kazi. Hii
inamaanisha si ada ya mume kutunzwa na mke. Dhana ya uovu wa mwanamke ni dhana
inayoshikiliwa na jamii nyingi pia ulimwenguni. Dhana hii inaendelezwa kupitia kwa
kisasili anachosimulia mhusika Sauni kinachobainisha uovu na kutoaminika kwa
mwanamke (uk. 80-83).
Utamaduni wa kisasa unajitokeza kwa sura mbalimbali. Desturi ya kuhodhi mali na
kujilimbikizia pesa inatokana na ubinafsi unaofungamana na maisha ya kibepari.
Mashindano ya kujinufaisha kifedha na uchu wa kuwa na mali nyingi au vitu ndio
unaowafanya watu kutoweza kuwajali wengine hasa matajiri. Jamii inajigawa katika
makundi mawili; walio navyo na wasio navyo.
Desturi ya mali kumilikiwa na wachache kama vile akina Sagilu, Mbwashu na jamaa ya
Mtemi Lesulia inaendeleza ubeberu na unyanyasaji wa maadui wao. Usasa pia unabainika
kutokana na wingi wa maisha ya raha na starehe. Jamii inazingatia maisha ya ufasiki,
uzinzi na kutowajibika katika ndoa. Tunaambiwa Sagilu anabadilisha magari sawa na
anavyobadilisha wanawake (uk. 18). Ngoswe pia anakumbatia maisha ya anasa na biashara
haramu kama ile ya mihadarati (uk. 123).
Wasichana wanatupilia mbali maadili na kukumbatia starehe na pesa kuliko utu kama vile
Sihaba na Cheiya. Majukumu katika asasi ya ndoa yanabadilika. Pale ambapo
mwanamume anahitaji kuwa kichwa kwa jamaa yake, tunamwona akihepa jukumu hili
linalotwaliwa na mwanamke hasa katika ndoa za kisasa. Hivi ndivyo anavyofanya
Mangwasha (uk. 29). Wanaume nao wanakosa adabu wanapowanyemelea wake za watu.
Tazama jinsi Sagilu anavyomnyemelea Mangwasha au hata kuzaa na mke wa Mtemi
Lesulia (uk. 161).
Mangwasha anaonekana kukashifu mila zilizopitwa na wakati pale anapomwambia
Mbungulu kwamba angeivunja mila ya kutomfuata mumewe katika starehe zake (uk. 32)
na kudharau baadhi ya mila kama hizo.

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

Maisha ya anasa, ulevi na matumizi ya dawa za kulevya


Ufasiki ni tabia ambayo hukiuka maadili ya kijamii. Tabia kama hii huhusishwa na uzinzi
au uzinifu. Tunaonyeshwa jinsi Sagilu anavyoishi maisha ya anasa huku akifanya usuhuba
na wanawake kama Sihaba nje ya ndoa. Anawanyang'anya wanaume wake zao hadi kuitwa
mnyakuzi na dudumizi (uk. 18). Anamhangaisha Mangwasha kutaka kufanya usuhuba
naye, hata kutaka kumhonga kwa kutumia pesa ili akubali (uk. 30, 60).
Ufuska wake unaonekana pia pale Mrima anaposema Sagilu alikuwa na masuria watoshao
kijiji kizima (uk. 18). Mrima anatumbukia katika anasa na kushiriki ulevi kupitia kwa
Sagilu (uk. 30, 37, 39, 42). Anashindwa hata kuitunza jamaa yake. Barua aliyoandikiwa
Mrima na mwanamke na
ambayo inapatikana ndani ya mkoba wa Mangwasha pamoja na yaliyomo katika barua
hiyo ni ishara ya maisha ya uzinzi aliyoishi Mrima (uk. 77).
Ulevi pia unamfanya Mrima kupotelea Majaani, pahali palipokuwa na walevi wa kila aina,
ilhali alikuwa na familia.
Maisha ya anasa yanabainika kupitia kwa uhusiano wa Sagilu na Cheiya, uhusiano
uliojengwa juu ya ufasiki (uk. 119-123). Ngoswe pia anaendeleza maudhui ya anasa, ulevi
na ufasiki pale tunapoambiwa anazifuja pesa kwa anasa mbalimbali. Vijana wengine wa
kitajiri kama yeye pia wanajivinjari katika starehe kutokana na utajiri wa wazazi wao.
Ngoswe ni kielelezo cha wale wanaofanya biashara ya dawa za kulevya (uk. 123) ambapo
mihadarati inaonekana kutumiwa kiholela nchini.
Mandhari ya ulevi katika mtaa wa Ponda Mali yanaendeleza maudhui ya ulevi kwani
pahali hapa palikuwa na walevi wa kila aina na unywaji pombe wa kupindukia (uk. 33).
Unafiki
Ni tabia ya mtu kujifanya rafiki au mwandani wa mtu ilhali sivyo. Tabia kama hii
hudhihirisha uongo au udanganyifu. Sagilu anapomtuma Sihaba kuwapelekea Mrima
na Mangwasha zawadi siku ya arusi yao ni dhihirisho ya unafiki. Hii ni kwa sababu
Sagilu alifahamu kilichokuwa katika kifurushi kilikuwa kilipuzi lakini akajifanya
kuwakirimia zawadi ya arusi (uk. 25).
Unafiki pia unaendelezwa na Sagilu pale ambapo anajifanya kumjali Mangwasha
anapokumbwa na mateso huku akijua ndiye aliyekuwa akisababisha mateso hayo ya
Mangwasha. Kwa mfano, Sagilu anamuuliza Mangwasha, "Mbona umekonda sana siku
hizi?" (uk. 60). Kwa upande wake, Mangwasha anamjua Sagilu kama mnafiki hasa pale
anaposema kwamba Sagilu ni chua ndani ya mchele na kumwita lumbwi. Chua
inapokuwa ndani ya mchele si rahisi kuitambua hadi pale unapoutafuna wali. Kadhalika,
lumbwi au kinyonga ana tabia ya kubadilisha rangi kiasi cha kumfanya mtu kutomtambua
kwa urahisi ili kubaini rangi yake kamili.
Maudhui ya unafiki yanajitokeza kupitia kwa Mtemi Lesulia ambaye alitaka kunyakua
ardhi ya Matango kwa kisingizio kuwa serikali ilitaka kujenga soko (uk. 95).
Chifu Mshabaha pia anaendeleza maudhui ya unafiki pale ambapo anawahujumu Waketwa
na kupokea mlungula kinyume na sheria za nchi aliyoitumikia huku akishirikiana na mtemi
kuwa serikali ilitaka kujenga soko.

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

Nanzia na Mbwashu wanaendeleza unafiki pale wanapowatembelea watu waliochomewa


nyumba zao pale kanisani ili kuwapa misaada ilhali wakijua lengo la kuwachomea watu
hao makazi yao.
Tamaa na ubinafsi
Tamaa ni hali ya kutaka sana kitu, matamanio ya kitu au jambo. Tamaa kama hamu au
utashi mkubwa wa kufaidi kitu huwa mbaya iwapo utafaidi mtu mmoja kutokana na
ubinafsi wake au kundi la watu lenye maslahi yanayofanana. Ubinafsi hubainika pale mtu
anapojipendelea yeye au kujifikiria yeye mwenyewe bila ya kuwajali wengine. Kuna
wahusika kadha wanaoendeleza maudhui ya tamaa na ubinafsi hasa pale mwandishi
anapotaja kuwa mtaa wa Majuu ulikuwa umeshiba ubinafsi na ubaguzi.
Mtemi Lesulia anajawa na tamaa ya uongozi. Yuko tayari kuwadhulumu au hata kuwaua
wapinzani wake kutokana na tamaa ya uongozi wa nchi. Anamteka nyara Lonare asiweze
kuwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu anapohisi kwamba huenda akamshinda na
kuwa mtemi (uk.10, 51, 164-172).
Aidha, akiwa na wakwasi wenzake kama vile Sagilu na Mbwashu wanahujumu pato la
nchi kutokana na tamaa ya kujilimbikizia mali. Ubinafsi wa Mtemi Lesulia unaonekana
pale anapomiliki rasilimali za serikali hasa kupitia kwa unyakuzi unaoendelezwa na mkewe
Nanzia.
Mfano unaotolewa wa mchwa na kichuguu (uk. 93) unaonyesha pia ubinafsi wa mtemi
kutokana na kufaidi jasho la wengine. Nanzia anaonyesha tamaa na ubinafsi pale
anapojaribu kubinafsisha jumba la Skyline Mall ambalo ni mali ya serikali (uk. 147) na
ardhi ya Matango kwa kushirikiana na mafisadi wenzake.
Sagilu anaendeleza maudhui ya tamaa na ubinafsi pale utashi wake wa pesa unampofanya
kuhodhi bidhaa kama vile ngano ili kuiuza kwa bei yajuu (uk. 17). Tamaa hiyo inamfanya
hata kuhatarisha maisha ya watoto nchini Matuo anapoagiza maziwa yenye sumu kutoka
ughaibuni (uk. 17). Ubinafsi wake unamfanya kuwazuia wengine wasimpiku kibiashara.
Tunaambiwa, "Kwa wale waliomshinda kwq werevu, aliwafanyia hila, mizungu na visanga
hata kuwafilisi kabisa kibiashara." (uk. 16). Tamaa ya uongozi na mali inamwingiza katika
urafiki na mtemi ili kutosheleza maslahi ya kibinafsi. Ubinafsi pia unamfanya Sagilu
kumtumia Mrima ili kujinufaisha kisiasa kutokana na tamaa ya uongozi. Sagilu
aliandamwa pia na tamaa za kimwili. Anawabadilisha wanawake hadi kuitwa dudumizi
kutokana na kuvizia na kuwachukua wake wa wengine (uk. 18).
Kupitia kwa Sagilu pia, tunamwona akiendeleza ubinafsi kwa jinsi anavyomtumia Sihaba
Sio tu kama kimada wake bali pia kutosheleza utashi wake wa kumiliki mali na biashara.
Anaendeleza maudhui ya tamaa anapomnyemelea Mangwasha tangu pale alipokuwa
msichana hadi baada ya kuolewa na Mrima ili kutosheleza uchu wake. Tamaa ya Sagilu
inamfanya hata kuzaa na mke wa Mtemi Lesulia kutokana na udhaifu uliodhihiri katika
ndoa yake. Anatumiwa pia na mtemi kama kikaragosi ili kuwanyanyasa watu wa Matango
huku akitumaini kufaidika kibinafsi.
Mrima anaendeleza maudhui ya tamaa na ubinafsi pale ambapo tamaa ya pesa inamtosa
katika tabia potovu. Anadanganywa na Sagilu huku akipewa pesa hadi kuitelekeza jamaa
yake. Ubinafsi wa kuyajali maslahi yake pekee unamfanya kukaidi masharti ya ndoa na
uwajibikaji.

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

Ubinafsi wa Mafamba unamfanya kuhujumu sheria za nchi kwa kuutetea ufisadi serikalini.
Ubinafsi pia unamfanya kudanganya kuwa vyeti vya kumiliki ardhi vya wenyeji wa
Matango vilikuwa ghushi (uk. 94), na kwamba serikali ilitaka kujenga soko katika mtaa wa
Matango.

Tamaa ya pesa inamfanya Sihaba kujiingiza katika biashara ya ulanguzi wa watoto wa


kike (uk. 141-144). Usuhuba wake na Sagilu pia unajengwa juu ya misingi ya tamaa ya
pesa na ubinafsi. Anatumiwa na Sagilu kuhujumu haki za Waketwa mbali na kutumiwa
na Sagilu kuwaangamiza maadui zake kibiashara (uk. 16). Hakujali maslahi ya wengine
ila yake binafsi.
Udanganyifu
Udanganyifu ni vitendo vya kughilibu watu au kufanya jambo ambalo mtu anajua ni
uongo.
Maudhui ya udanganyifu yanajitokeza katika serikali ya Mtemi Lesulia hasa kupitia kwa
mwanasheria Mafamba anayedanganya mahakama kuhusu ujenzi wa soko katika ardhi ya
Matango (uk. 94). Maudhui ya udanganyifu yanabainika kupitia kwa Sagilu
anayeshirikiana na Sihaba kujaribu kuwaangamiza Mrima na Mangwasha siku ya arusi
yao. Zawadi aliyobeba Sihaba haikuwa halisi bali kilipuzi cha kuwaangamiza maarusi hao.
Ukatili
Hii ni tabia inayodhihirisha ukosefu wa huruma. Ukatili unatokana na moyo mgumu kiasi
cha kuweza kutekeleza mauaji au kuleta hasara na mateso kwa wengine.
Maudhui ya ukatili yanaendelezwa kupitia kwa Sagilu ambaye aliweza hata kuwaua
washindani wake katika biashara (uk. 16). Ukatili wake unabainika pia pale anapoagiza
maziwa ya watoto yenye sumu bila kujali maisha Yao.
Sagilu anapovunja ndoa za Wengine anaendeleza ukatili. Anaendeleza maudhui ya ukatili
pale anapomtesa Mangwasha kimawazo huku akihatarisha ndoa yake kwa kutumia pesa
kumlewesha Mrima hadi akawa mlevi na mwishowe kuachishwa kazi.
Sagilu anaendeleza maudhui ya ukatili anapompokonya mwanawe mpenzi wake na hivyo
kuuvunja uchumba wao. Kushiriki kwake katika kupanga njama ya kuwachomea
Waketwa makazi yao ili yeye na jamaa ya mtemi wafaidi kisiasa ni mwendelezo pia wa
maudhui ya ukatili.
Ukatili unaendelezwa na Mtemi Lesulia pale anapowadhulumu raia wake kupitia kwa
vitendo vya kikatili ili kujinufaisha kisiasa. Anampangia Lonare mauti kwa sababu za
kisiasa. Ukatili wa serikali yake unabainika pale yeye na wenzake waliposhindwa kesi ya
ardhi ya Matango. Tunaona hakimu akinyang'anywa leseni ya uanasheria hata kushushwa
madaraka bila kuzingatia haki na ushahidi uliowasilishwa mahakamani. Kauli ya mtemi
kwamba, "Wale panya wamesharudi katika makao Yao..." (uk. 78) inaonyesha ukatili
wake kwa wenyeji wa Matango.
Mwanasheria Mafamba anatumiwa kuendeleza ukatili wa Mtemi Lesulia pale
anapotimuliwa kutoka katika afisi za serikali bila kujali kazi aliyoifanyia serikali hiyo
dhalimu. Maudhui ya ukatili yanaonekana wakati wa uchaguzi wa mchujo tunapomwona

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

mtemi akiwapa vijana pesa na kuwaamuru waharibu zoezi hilo ili mwishowe yeye na
Sagilu wapate kuwashinda wapinzani wao. Hakujali iwapo vijana hao wangeuliwa na
askari walinda usalama wala kujali rai za mwanawe Ngoswe (uk. 129- 130).

Mtemi Lesulia anaendeleza maudhui ya ukatili pale anapohusika katika kutoweka kwa
Lonare siku chache kabla ya uchaguzi mkuu. Anafanya hivyo ili yeye abahatike kushinda
kiti cha mtemi wa Matuo.
Maudhui ya ukatili yanaonekana kupitia kwa Sihaba pale anaposhirikiana na Sagilu
kuwachomea Waketwa nyumba zao. Pia anakubali kusimamia ujenzi wa ua katika makazi
ya Waketwa ilhali anajua kwamba kitendo kile ni cha kikatili.
Maudhui ya ukatili yanaendelezwa na Sihaba pia pale anapowapelekea Mrima na
Mangwasha zawadi ya arusi akiwa na lengo la kuwaangamiza. Anapoanzisha makao ya
Red Beads Lodgings ili kuwachuuza vigoli kwa wanaume ni mwendelezo wa maudhui ya
ukatili. Kujinufaisha kwake kutokana na biashara hiyo haramu ni ukatili anaowatendea
watoto kwani hakujali maisha yao ya baadaye (uk. 140-143).
Mapenzi na asasi ya ndoa
Mapenzi ni hali ya mvuto na upendo alio nao mtu kwa mtu mwingine; hisia ya upendo
aliyo nayo mtu moyoni mwake kuhusu mtu mwingine.
Ndoa ni maafikiano rasmi ya baina ya mwanamume na mwanamke ili waweze kuishi
pamoja kama mke na mume.
Maudhui ya mapenzi na asasi ya ndoa yanaelezwa kupitia kwa wahusika mbalimbali. Asasi
ya ndoa inakumbwa na matatizo kadha yakichangiwa na tamaa za kimwili na pesa. Hata
hivyo, hakuna ndoa inayovunjika hata kama misukosuko inakuwepo.
Ndoa ya Mtemi Lesulia na mkewe Nanzia awali ilikumbwa na tatizo la ukosefu wa watoto
hadi kufikia kiwango cha mtemi kutaka kumtaliki mkewe. Tatizo hili linatoweka pale
mtoto anapozaliwa, hata ingawa baadaye tunafahamishwa kuwa mzazi wake si mtemi.
Ingawa mtemi hafahamu hili, Ngoswe anaachwa na mshtuko mkubwa mama yake
anapomweleza kuwa mzazi wake ni Sagilu.
Ndoa ya Sagilu na mkewe pia inayumba pale Sagilu anapopatwa na kichaa. Mkewe
anamtoroka hadi afueni inapomrejea mumewe, na ndoa hiyo kuimarika tena.
Ndoa kati ya Mrima na mkewe Mangwasha pia ina misukosuko; tokea ulevi wa Mrima na
kutowajibikia ndoa yake hadi vishawishi vya pesa za Sagilu vinavyomfanya kuachishwa
kazi. Uvumilivu wa Mangwasha mwishowe unafaulu kuokoa ndoa yake.
Mapenzi ni sehemu ya maudhui yanayojitokeza pia. Kuna mapenzi baina ya wanandoa na
mapenzi baina ya vijana. Mapenzi baina yavijana hayaonekani kudumu. Mifano ni kama
vile usuhuba wa Mashauri na Cheiya ambao unaonekana kuegemea upande mmoja. Cheiya
anaonekana kumpenda Mashauri lakini mapenzi yake siyo ya dhati ila anavutiwa na
maisha ya anasa na pesa. Hali hii inaonekana pale anapofanya urafiki na mzazi wa
Mashauri ili afaidi pesa zake. Sihaba naye anajifanya kumpenda Sagilu lakini mapenzi

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

yake siyo ya dhati. Anamfuata Sagilu ili kumtimizia mahitaji yake ya maisha. 'Pesa kwake
zilikuwa kigezo cha penzi' (uk.16). Ngoswe haonekani kuwa na mpenzi mmoja bali
anawabadilisha wanawake kutokana na uwezo wa kifedha alio nao. Hathamini mapenzi
kati ya wapendanao kama anavyoeleza
Ukiukaji wa haki za watoto

Haki ni utendaji, ufuataji na utumiaji wa sheria na kanuni katika kutimiza jambo. Maudhui
ya ukiukaji wa haki za watoto yanabainika tunapomwona
Mangwasha pale mwanzoni akihangaika na wanawe peke yake bila baba yao. Mrima
anashiriki ulevi na maisha ya anasa hadi kuachishwa kazi.
Hajishughulishi na malezi ya wanawe kama vile kuwalisha, kuwavisha, kuwasomesha na
kuwapa malezi mema kama mzazi. Anakosa uwajibikaji hadi pale anaposhurutishwa
kuishi na jamaa yake na kuwajibika (uk. 1, 29, 31, 101, 115).
Maudhui ya ukiukaji wa haki za watoto yanaonekana pale wasichana wadogo
wanapozalishwa wakiwa bado hawajatimiza umri wa kujitwika majukumu kama hayo (uk.
137-138). Maudhui haya yanaendelezwa kupitia kwa taswira anayochora mwandishi
kuhusu watoto wenye umri mdogo. Hawa wanaishi katika barabara na vichochoro vya mji
huku
wakinusa gundi na magunia ya taka yakiwa migongoni. Huu ni ukosefu wa malezi mema
unaotokana aghalabu na umaskini wa wazazi wao (uk. 138). Kwa ujumla maudhui haya
yanaendelezwa katika nchi ya Matuo ambayo inahiari kukinyanyasa kizazi hiki kichanga
bila kuwa na mpango mzuri wa maisha yao.
Maudhui ya ukiukaji wa haki za watoto pia tunayaona kupitia kwa vitendo vya Sihaba.
Huyu anapowahusisha wasichana wadogo katika biashara ya ukahaba ili ajinufaishe
kifedha huwa pia anakiuka haki za watoto (uk. 141-143).
Nafasi ya mwanamke katika jamii
Maudhui ya nafasi ya mwanamke yanaendelezwa kupitia kwa taswira mbalimbali za
mwanamke.
Mangwasha ni mwanamke aliyejikomboa kimawazo. Anakaidi mila na desturi potovu za
jamii zilizopitwa na wakati pamoja na zile zinazomdhalilisha mwanamke. Tunamwona
akikataa ushauri wa Chifu Mshabaha aliyetaka kumchagulia mchumba.
Anakataa ushauri wa Mbungulu pia pale anapomwambia mila hairuhusu mke kumfuata
mumewe akiwa katika starehe zake (uk. 32).
Maudhui ya nafasi ya mwanamke yanajitokeza kupitia kwa Mangwasha anayejitambulisha
kama mtetezi na mpiganiaji wa haki za watoto, vijana na wanaodhulumiwa katika jamii.
Mwanamke huyu akishirikiana na wengine kama Mbungulu anafaulu kuwanasua watoto
wa kike waliokuwa wamenaswa katika mtego wa Sihaba aliyetaka kujitajirisha kupitia
kwao.
Tunamwona pia akiwashirikisha vijana na kuwapa usaidizi wa kujiendeleza katika maisha
yao. Tunaarifiwa, "Mangwasha alifungua (uk. 154) afisi mjini ili kushughulikia vijana na

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

watoto wa mitaani..." na kwamba alipata ufadhili kutoka katika mashirika mbalimbali ya


kuwasaidia watoto.
Maudhui ya nafasi ya mwanamke pia yanaendelezwa kupitia kwa Mbungulu anayejitokeza
kama mhafidhina wa utamaduni wa jamii yake na majukumu ya mwanamke katika
utamaduni huu. Anaendeleza uhifadhi wa mila zilizowekwa na jamii yake hasa pale
anapomshauri Mangwasha kuhusu mafunzo aliyofunzwa na jamii yake (uk. 32).

Maudhui haya pia yanajitokeza kupitia kwa Mrima anayezingatia masharti ya jamii yake
iliyosheheni ubabedume unaomdhalilisha mwanamke kiasi cha kutomsikiliza mkewe.
Mangwasha anasimama kidete na kutimiza wajibu wake katika ndoa licha ya kwamba
mumewe anamtupa. Tunamwona jinsi anavyojizatiti kuwatunza wanawe pale mumewe
alipomtoroka kutokana na anasa za ulevi.
Aidha, dhuluma dhidi ya mwanamke inajitokeza kupitia kwa kauli za Mrima hasa pale
anapomtoroka mkewe na wanawe ili kufaidi starehe kupitia pesa alizokuwa akipewa na
Sagilu (uk. 40-41). Maudhui haya pia yanaonyesha kwamba mwanamke hathaminiwi kama
kiumbe sawa na mwanamume chini ya mfumo huu wa ubabedume hasa pale Mrima
anaposema, "Tangu lini mke amuulize mumewe kule aendako au atokako?...Ama kweli,
wanawake wa kisasa wanavunja kila mwiko uliowekwa na wazee." (uk. 40).
Maudhui ya nafasi ya mwanamke kama asiyeheshimiwa yanajitokeza kupitia kwa Sagilu
ambaye anamchukua mwanamke kama pambo tu na anayeweza kushawishiwa kwa urahisi
kwa kutumia pesa. Hali hii inaonekana pale anapotaka kumpa Mangwasha pesa ili akubali
kuwa mpenzi wake (uk. 60).
Kwa upande mwingine, maudhui haya yanabainisha nafasi ya mwanamke kama katili,
mzinzi na mwenye ubinafsi. Kupitia kwa Sihaba, mwanamke anajitokeza kama kielelezo
kibaya kwa jamii hasa anapofananishwa na mabaya yote yanayokumba ulimwengu (taz.
kisasili kinachosimuliwa na Sauni (uk. 81-83).
Taswira mbaya ya mwanamke inaonekana pia kupitia kwa wahusika wa kike kama vile
Mbwashu, Nanzia na Cheiya ambao wanajitokeza kama vitegemezi vya wanaume.
Mbwashu anashirikiana na wanaume kama Mtemi Lesulia kujinufaisha kiuchumi ilhali
Nanzia anaishi chini ya mbawa za mumewe ili kujiimarisha kiuchumi na kimaisha. Cheiya
anaendeleza maudhui hayo ya utegemezi kwani tunaona akiwategemea Mashauri na Sagilu
ili kujinufaisha.
Umaskini
Umaskini ni hali ya kutokuwa na mali; ukata, uchochole.
Maudhui ya umaskini yanaendelezwa kupitia kwa sera mbovu za uongozi katika serikali ya
Mtemi Lesulia. Uongozi unatawaliwa na ubaguzi unaotokana na jamii mbili hasimu;
Wakule wanaofaidi pato la nchi zaidi kutokana na utawala wa Mtemi Lesulia ambaye ni
Mkule, na Waketwa wanaofukarishwa na ubaguzi huo. Utabaka na ufisadi pia unachangia
kuleta umaskini.
Kuna matajiri wenye vyeo na mali kwa upande mmoja na maskini wanaozumbua riziki
kutokana na ajira za mapato ya chini. Maudhui haya pia yanaendelezwa kupitia kwa sera za

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

nchi ambazo ziliwafaidi wachache (uk. 51). Umaskini unasababisha vijana kutumiwa na
matajiri kutekeleza uovu. Katika (uk. 66), tunaona vijana wakitumiwa na matajiri
kuteketeza makazi ya Waketwa. Umaskini unachangiwa na ukosefu wa ajira hasa kwa
vijana waliohitimu shuleni au vyuoni. Umaskini unawafanya hata wazazi kuwachuuza
mabinti zao wachanga ili wapate pesa (uk. 143). Maudhui ya umaskini yanabainishwa
kupitia kwa sera za uchumi zisizozingatia maslahi ya wanyonge. Viongozi wa nchi
wanatajirika ilhali wananchi walio wengi wanafukarishwa zaidi, lengo likiwa
kuwafukarisha ili iwe rahisi kwao kuendelea kuwatawala.

Ukosefu wa matumaini
Matumaini ni hali ya matarajio ya kupata kitu; matarajio, matamanio.
Ukosefu wa matumaini ni hali ya kukataa tamaa; kukosa matarajio, kukosa matamanio,
Maudhui ya ukosefu wa matumaini yanabainika pale idadikubwa ya vijana inaonekana
kuzurura mjini na kupoteza muda wao katika viambaza vya maduka kwa kukosa
matumaini. Mwandishi anaeleza kuwa "Ukosefu wa matumaini ya kuishi ulianza kuhasiri
mifumo ya kijamii." (uk. 47). Ukosefu huu wa matumaini unasababisha maafa katika jamii
pia (uk. 44- 47). Vijana waliomaliza masomo hawana pa kwenda. Ukosefu wa ajira kwa
vijana hao unawafanya kukosa matumaini. Umaskini wa wazazi wao pia unachangia katika
ukosefu wa matumaini. Vibaka wa mji wanakosa matumaini na wanasalia kusubiri ghasia
zizuke mjini ili waweze kuwapora watu mali zao.
Uvumilivu
Uvumilivu ni hali ya kuvumilia mambo magumu; ustahimilivu. Maudhui ya uvumilivu
yanajitokeza kupitia kwa wahusika Mangwasha na Lonare.
Mangwasha anavumilia vitisho na dharau za Chifu Mshabaha ilimradi aweze kuitunza
jamaa yake. Anavumilia kazi nyingi afisini mwa chifu huyo ili aweze kuwakimu wanawe
pale mumewe anapomtoroka. Anavumilia vitimbi vya chifu ilimradi apate mawili matatu
kuhusu njama za serikali na yale wanayopangiwa Waketwa. Anavumilia kauli za chifu za
kumvunja moyo ili aweze kulinda ajira yake. Mangwasha anaendeleza maudhui ya
uvumilivu pia pale anapovumilia lugha ya dharau na ushawishi wa pesa kutoka kwa Sagilu
ili asitiri ndoa yake na Mrima. Aidha, anavumilia dharau, matusi na ulevi wa mumewe ili
kusitiri ndoa yake. Kwa upande wake,
Lonare anaendeleza maudhui haya kupitia uvumilivu dhidi ya vitisho vya uongozi wa
Mtemi Lesulia kutaka kumwangamiza au hata kuangamiza biashara yake (uk. 50).
Maudhui ya uvumilivu pia yanaendelezwa na
Lonare kutokana na jinsi anavyoteswa, kutekwa nyara hadi kuhatarisha maisha yake ili
asaidie kuikomboa nchi yake kutokana na uongozi mbaya wa Mtemi Lesulia.
Usaliti
Usaliti ni hali ya kwenda kinyume na matarajio ya mtu au nchi. Pia ni ile hali ya
kuwafanya watu wakosane kwa kuwachonganisha kupitia matumizi ya uongo.
Maudhui ya usaliti yanajitokeza kupitia kwa Chifu Mshabaha, Mrima, Sagilu, Mtemi
Lesulia, Nanzia, Mbwashu na Cheiya.

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

chifu Mshabaha anaisaliti jamii ya Waketwa kwa kushiriki katika njama ya kuwaondoa
kutoka katika makao yao (uk. 55). Chifu anamsaliti
Mangwasha anapompa Mrima bahasha ya pesa kama hongo ya kuendesha kampeni za
Mtemi Lesulia (uk. 110), kinyume na matakwa ya jamii yake. Aidha, usaliti unaendelezwa
na chifu pale anapomsaliti Mangwasha kwa kumleta msichana mwingine kazini kwake ili
kumfuta yeye kazi (uk. 135).

Maudhui ya usaliti yanajitokeza kupitia kwa Mtemi Lesulia pale anapousaliti uaminifu wa
Ngoswe kwa kuwaambia waende kuvuruga amani wakati wa uteuzi wa viongozi ili
kuhakikisha ushindi unamwendea Sagilu bila kujali iwapo wangeuliwa na askari (uk. 129).
Mtemi anaisaliti nchi pamoja na wananchi wa Matuo kwa kuzorotesha uchumi kupitia kwa
sera mbovu za uongozi na ufisadi uliokithiri. Isitoshe, anaisaliti jamii ya Waketwa kwa
kuibagua katika ajira, biashara, hata katika makazi yao.
Maudhui ya usaliti yanajitokeza kupitia kwa Mtemi Lesulia pia kwani licha ya
mwanasheria Mafamba kuifanyia serikali yake kazi na kumfichia uovu wake katika kesi za
ufisadi, anamnyang'anya cheti cha uanasheria na kumtowesha kutoka mjini Taria. Pia
anamnyang'anya hakimu cheti chake cha uanasheria na kumfuta kazi licha ya kwamba
alikuwa akitekeleza majukumu yake kulingana na sheria.
Maudhui ya usaliti yanaendelezwa na Sagilu anapoisaliti jamii ya Waketwa walioishi
Matango kwa kushiriki katika kuchoma makazi yao licha ya kwamba yeye mwenyewe
alitaka achaguliwe kuwa mbunge wao. Anamsaliti Mrima kwa kumhonga pesa ashiriki
katika anasa huku akijua alimtaka mkewe kimapenzi.
Tunamwona akimsaliti Mangwasha kwa kumtembelea na kujifanya anayajali maslahi yake
ilhali ndiye anayemfadhili Mrima kushiriki ulevi na anasa hadi kufutwa kazi.
Sagilu anamsaliti mwanawe Mashauri kwa kumnyang'anya mchumba wake Cheiya bila
kujali heshima yake.
Pia anamsaliti Mtemi Lesulia kwa kumhakikishia kuwa kila kitu kiko shwari wakati wa
uchaguzi mkuu huku akijua kwamba katu Lesulia hangeshinda katika uchaguzi huo (uk.
174).
Kupitia kwa Mrima, maudhui ya usaliti yanabainika anapoisaliti jamaa Yake kwa
kushirikiana na Sagilu huku mkewe na wanawe wakiteseka.
Mrima pia anamsaliti mkewe kwa kufanya usuhuba na wanawake nje ya ndoa hasa kupitia
kwa barua anayoipata Mangwasha (uk. 77), huku mkewe akijitahidi kuitunza familia bila
usaidizi kutoka kwake.
Usaliti pia unajitokeza pale Mrima anapoisaliti jamii yake hasa Lonare na wengine
waliomwokoa kutoka katika maisha ya ulevi, pale anapochukua hongo ili amfanyie mtemi
kampeni ilhali akijua huyu alikuwa adui wa Waketwa.
Maudhui haya pia yanaendelezwa na Cheiya anayemsaliti Mashauri anapokubali kufanya
usuhuba na Sagilu bila kujali kuwa huyu alikuwa mzazi wa Mashauri. Nanzia anamsaliti

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181


TOPLIGHT PUBLISHERS KENYA PANEL NGUU ZA JADI GUIDE BOOK

mumewe Mtemi Lesulia pale anapofanya usuhuba na Mhindi pamoja na Sagilu na kuzaa
watoto nje ya ndoa.
Usaliti wa Mbwashu unatokea pale anapotorokea Ulaya baada ya Mtemi Lesulia
kushindwa katika uchaguzi mkuu. Anamtoroka baada ya kutajirika kutokana na utawala
wake huku akimwacha na fedheha ambayo hakutaka kushiriki wala kujihusisha na uovu
waliofanya pamoja wakati wa utawala wake.
Ulipizaji kisasi

Kisasi ni tendo la kulipiza ubaya aliofanyiwa mtu.


Kulipa kisasi ni kulipiza maovu aliyotendewa mtu.
Maudhui ya kulipiza kisasi tunayaona kupitia kwa Sagilu ambaye analipiza kisasi tangu pale
penzi lake lilipokataliwa na Mangwasha. Anamtumia Mrima kulipiza kisasi pale anapofaulu
kumteka akili, kumpumbaza kwa pesa na anasa za ulevi ilimradi Mangwasha
ateseke katika ndoa yake. Sagilu anahiari hata kujaribu kutoa uhai wa Mangwasha na
mumewe siku ya arusi yao kwa kumtumia Sihaba ili awaangamize kwa kilipuzi.
Ukombozi

KWA MWONGOZO MZIMA PIGA SIMU 0729125181

KWA MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA NA MAPAMBAZUKO PIGA SIMU KWA 0729125181

You might also like