Nenda kwa yaliyomo

Wasukuma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kijiji kimojawapo cha Wasukuma mwanzoni mwa karne ya 20 (1906 - 1918).

Wasukuma ni kabila kubwa zaidi nchini Tanzania: linakadiriwa kufikia watu milioni 10, idadi inayowakilisha asilimia 16 ya wakazi wa nchi kwa ujumla.

Jina

Jina "Wasukuma" lina maana ya watu wa Upande wa "Kaskazini", lakini maana hii haiwakilishi maana halisi ambayo watu wengi huitafsiri kwa mfano Wasukuma hutumia alama ya utambulisho (dira) kwa eneo fulani kwa viashirio vya makabila, kwa mfano wa jina kama hili: Kiya. Hili lina maana ya mashariki ambako ni maawio ya jua. Huu ni utambulisho ambao haukufananishwa ama kuitwa kwa jina la kabila fulani. Mfano mwingine ni upande wa "Dakama" ambapo yatambulisha kama eneo la Unyamwezi lakini zaidi ya mpanuko wake ni upande wa "kusini". Zaidi ya hapo neno hili hutumiwa sana na kabila la Wanyamwezi ili kutambulisha eneo la Wasukuma ambapo Wasukuma nao husema "dakama". Upande mwingine ambao unapewa alama ya utambulisho ni "Ushashi" maana yake ni upande wa kabila la Washashi na neno hili Washashi ni mkusanyiko wa makabila ya mkoa wa mara, japo pia neno hili "shahi" linamaanisha kabila la Wakurya ambalo pia mpanuko wake unakomea hapo, ambapo zaidi ya hapo eneo zima la upande huo unamaanisha upande wa kaskazini. Upande wa mwisho kutambulishwa ni "Ngw’eli", neno hili halikupewa kabila na badala yake linawakilisha upande wa magharibi (dira), ambako ni machweo ya jua. "Wasukuma wenyewe hulirejea jina hili kama "Basuguma" kwa wingi na "Nsuguma" kwa umoja.

Vilevile Wasukuma wamegawanyika katika makundi makuu manne ambayo ni Wasukuma wa Bariadi,Maswa na Meatu [Wanyantuzu], Wasukuma wa Mwanza [Bhasuku] au [Wasumau], Wasukuma wa Sengerema na Geita [Bhanang'weli], Wasukuma wa Tabora [Wadakama] na Wasukuma mchanganyiko kutoka Kahama na Tabora (hawa wakienda Tabora wanaambiwa ni Wasukuma, wakienda sehemu za Ntunzu wanaambiwa ni Wanyamwezi. Wako mchanganyiko na Wasumbwa, Wasukuma halisi na Wanyantuzu.

Eneo

Wasukuma huishi eneo la kaskazini magharibi mwa Tanzania, karibu na mwambao wa kusini mwa Ziwa Victoria, na maeneo mbalimbali ya utawala ya wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza, upo pia kusini magharibi mwa mkoa wa Mkoa wa Mara, Mkoa wa Simiyu na Mkoa wa Shinyanga.

Eneo la kaskazini la makazi yao ni katika mbuga maarufu Serengeti. Familia za Wasukuma wengi sana wamehamia maeneo ya kusini kuelekea mkoa wa Rukwa ambao baadae umegawanywa na kuzaa mkoa wa Katavi, wakipita maeneo ya kabila la Wapimbwe na hivyo kufanya makazi katika eneo hili la kijiji cha Wapimbwe.

Eneo hili linakadiriwa kuwa na ukubwa wa mita za mraba 910 hadi 1200.

Mwinuko wake unakadiriwa kuwa inchi 20 hadi 40 ya ujazo wa mvua kutoka Novemba hadi Machi.

Kiwango cha juu cha joto hutegemea angalau ni kutoka wakati kiwango cha chini nyakati za usiku hushuka na kufikia 15°C.

Maeneo yaliyo na madini

Wasukuma wamezungukwa na madini mbalimbali. Yafuatayo ni maeneo yaliyo na madini:

  • 1. Mwadui (Huku kuna madini ya almasi ambayo kwa kiwango kikubwa huipatia serikali pesa za kigeni)
  • 2. Maganzo (Vilevile eneo hili limewekwa kwa ajili ya wachimbaji wadogowadogo wa almasi, eneo hili liko magharibi ya Mwadui)
  • 3. Buzwagi (Kahama)
  • 4. Bulyanhulu (Kahama)
  • 5. Geita
  • 6. Nyangalata (Kahama).

Shughuli za kiuchumi

Shughuli kuu za kiuchumi kwa Wasukuma ni kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara.

Pamba ndio zao kuu la kibiashara kwa wasukuma, ambao pia hulima mazao mengine kama mpunga, tumbaku, mahindi, viazi, dengu na matunda (kisiwani Ukerewe)

Wasukuma pia ni wafanyabiashara na uvuvi, madini mbalimbali kama vile dhahabu, almasi na madini mengineyo ambayo huchimbwa katika maeneo mbalimbali mikoa ya Mwanza na Shinyanga.

Wasukuma pia wanajihusisha sana na kilimo cha mazao ya nafaka na mifugo ya aina mbalimbali. Maeneo ya Shinyanga wanalima mazao ya nafaka kama mahindi na mpunga.

Idadi ya watu inaongezeka kwa kasi na hivyo pia kuongezeka kwa wakulima wa mbogamboga.

Shughuli za sherehe

Wasukuma wengi katika karne ya 20 walitumia utamaduni wao zaidi katika kusherehekea matukio ya nyakati mbalimbali, kwa mfano wakati wa mavuno, unyago, ndoa, misiba n.k.

Sherehe za mavuno maranyingi huitwa Bulabo: hizi ni sherehe zinazofanyika mwezi wa sita mpaka wa saba kwa kila mwaka. Hapa Wasukuma hufurahia burudani za ngoma za kienyeji mfano Mbina za bacheye, bagika, bagalu na wigashe! Hizi zineelezewa vizuri katika Makumbusho ya Wasukuma (Sukuma Museum) pale Bujora Kisesa Mwanza.

Watemi ndio walikuwa viongozi wa kabila la Wasukuma na watu walikaa kiukoo katika eneo moja.

Watu maarufu katika kabila la wasukuma

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wasukuma kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.