Wafiadini wa Aquae Regiae
Mandhari
Wafiadini wa Aquae Regiae (walifariki 459) walikuwa Wakristo wa Kanisa Katoliki ambao waliuawa na Wavandali Waario chini ya mfalme Genseriki kwa ajili ya imani yao wakiwa kanisani kuadhimisha Pasaka katika mji huo (leo Arbal nchini Algeria).
Msomaji wao alichomwa koo kwa mshale wakati wa kuimba Aleluya mimbarini.
Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 5 Aprili[1][2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |