Nenda kwa yaliyomo

Usayaria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Usayaria mjini Dhaka, Bangla Desh
Ndani ya usayaria mjini Belgrad, wakati projekta inatupisha anga la usiku
Usayaria mdogo wa kubeba, ndani ya hema

Usayaria (kwa Kiing. planetarium) ni jengo au chumba chenye kusudi la kuonyesha picha kamili ya anga la usiku na nyota zake. Usayaria ni tofauti na paoneaanga ambako nyota halisi zinatazamwa[1][2].

Ukumbi au chumba cha usayaria huwa na umbo la kuba, kama nusu-tufe.

Picha zinarushwa hapo kwa njia ya projekta.

Projekta za kisasa zinaweza kuonyesha anga la usiku jinsi linavyoonekana mahali popote duniani na pia wakati wowote ama wakati uliopita au wakati ujao.

Projekta za usayaria za kwanza zilitengenezwa na kampuni ya Zeiss huko Ujerumani baada ya Vita Kuu ya Kwanza. [3]

Sayaria zinapatikana karibu kote duniani; usayaria kubwa zaidi uko Sankt Peterburg (Urusi) wenye ukumbi ulio na kipenyo cha mita 37. Ziko pia sayaria ndogo za plastiki zinazofunguliwa kwa kujaza hewa ndani yake. Usayaria mdogo vile hutumiwa kufundisha shuleni ukiweza kuhamishwa kirahisi.

  1. King, Henry C. "Geared to the Stars; the evolution of planetariums, orreries, and astronomical clocks" University of Toronto Press, 1978
  2. Directory of Planetariums, 2005, International Planetarium Society
  3. A Fifty Year Anniversary of a Two Thousand Year Dream (PDF). Juz. la 2. International Society of Planetarium Educators. 1973-09-21. ku. 95 ff.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]