Usawa wa kijinsia
Usawa wa kijinsia ni lengo la jitihada za kuleta usawa kati ya jinsia zote mbili na kuondokana na dhuluma mbalimbali za jinsia moja dhidi ya nyingine zilizotawala historia ya binadamu.
Usawa wa kijinsia unahusiana na haki za binadamu, hasa haki za wanawake na maendeleo ya kiuchumi. UNICEF inafafanua usawa wa kijinsia kama "kusawazisha uwanja wa kucheza kwa wasichana na wanawake kwa kuhakikisha kwamba watoto wote wana fursa sawa ya kuendeleza vipaji vyao".
Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa (United Nations Population Fund) ulitangaza usawa wa kijinsia "kwanza kabisa kama haki ya binadamu".
Usawa wa kijinsia ni mojawapo kati ya malengo ya "mradi wa Milenia" wa Umoja wa Mataifa unaotarajia kumaliza umaskini ulimwenguni ufikapo mwaka 2015; mradi huo unadai, "Kila lengo linahusiana moja kwa moja na haki za wanawake, na jamii ambamo wanawake hawana haki kama za wanaume kamwe haziwezi kufanikisha maendeleo kwa namna endelevu".
Hivyo, kukuza usawa wa kijinsia kunaonekana kama himizo kwa mafanikio makubwa ya uchumi. Kwa mfano, mataifa ya Kiarabu ambayo yanawanyima wanawake usawa yalionywa katika ripoti iliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2008 kwamba kitendo cha kuwanyima mamlaka wanawake ni kipengele muhimu kinachodhalilisha kurudi kwa mataifa hayo katika nafasi ya kwanza ya uongozi wa dunia katika biashara, elimu na utamaduni.
Tazama pia
Marejeo
Viungo vya nje
- WomenWatch, Mtandao wa Internet wa Umoja wa Mataifa wa Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake
- Uwezeshaji wa Wanawake Archived 9 Oktoba 2009 at the Wayback Machine.Timu ya Kijinsia ya Mpango wa Maendeleo ya Umoja wa Mataifa
- GENDERNET, Jukwaa la kimataifa la wataalamu wa jinsia wanaosaidia usawa. Ushirikiano wa Maendeleo ya Ukurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo
- [1], Shughuli za kijinsia katika kituo cha OECD.
- Usawa wa kijinsia kama Smart Economics Archived 9 Machi 2010 at the Wayback Machine. Benki ya Dunia
- The Local Usawa wa kijinsia katika Uswidi (Mkusanyo wa habari)
- Women Can Do It! Archived 12 Februari 2021 at the Wayback Machine.
- Sexism Discussion Group Archived 29 Novemba 2009 at the Wayback Machine.
- Usawa wa kijinsia na Upendo wa Kiromantic Archived 13 Machi 2013 at the Wayback Machine.
- Usawa wa kijinsia unaofuata Archived 12 Machi 2010 at the Wayback Machine.
- The OneWorld Guide to Gender Equality Archived 13 Mei 2010 at the Wayback Machine.