Nenda kwa yaliyomo

Polokwane

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Polokwane


Jiji la Polokwane
Jiji la Polokwane is located in Afrika Kusini
Jiji la Polokwane
Jiji la Polokwane

Mahali pa mji wa Polokwane katika Afrika Kusini

Majiranukta: 23°53′24″S 29°27′0″E / 23.89000°S 29.45000°E / -23.89000; 29.45000
Nchi Afrika Kusini
Majimbo Limpopo
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 123,749
Tovuti:  www.polokwane.org.za

Polokwane (kwa Kiafrikaans: Pietersburg) ni manisipaa ya Afrika Kusini na mji mkuu wa Jimbo la Limpopo. Mji una wakazi nusu milioni.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mji ulianzishwa mwaka 1886 na makaburu wa Voortrekker ukapewa jina la Pietersburgh kwa heshima ya jenerali ya makaburu Petrus Jacobus "Piet" Joubert. Wakati wa Vita ya pili ya Waingereza dhidi ya Makaburu Pietersburgh ikawa mji mkuu wa jamhuri ya Transvaal ikavamiwa na Waingereza mwaka 1901.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Polokwane iko katika nyanda za juu kwa kimo cha mita 1,312. Hali ya hewa ni ya wastani yenye sentigredi 27°C wakati wa joto na 20°C wakati wa baridi.

Kuna migodi ya almasi na kiwanda cha kuchimbia mchanga safi sana unaofaa matumizi ya vioo. Pamoja na migodi kuna pia viwanda mbalimbali.

Polokwane iliona michezo ya mpira wakati wa kombe la dunia la 2010. Polokwane pia ni jina la timu ya mpira wa miguu, na ndiyo makao makuu ya timu hiyo ijulikanayo kama "Polokwane Football Club"

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Polokwane kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.