Paulo I wa Konstantinopoli
Mandhari
Paulo I wa Konstantinopoli (mzaliwa wa Thesalonike, Ugiriki, alifariki mwaka 350 hivi) alikuwa askofu mkuu wa sita wa Konstantinopoli kuanzia mwaka 337.
Paulo alijihusisha na mabishano kuhusu Uario yaliyoshughulikiwa na ndugu Makaisari Constans I (Dola la Roma Magharibi) na Constantius II (Dola la Roma Mashariki).
Basi Paulo alitawazwa na kuondolewa mara tatu kati ya miaka 337 na 351.
Hatimaye Constans I alimpeleka uhamishoni huko Cucusus, kijiji cha mkoa wa Kapadokia (leo nchini Uturuki) alipokabwa kikatili na Waario hadi kufa [1].
Anaheshimiwa tangu kale kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Juni au tarehe 6 Novemba[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Socrates Scholasticus, H. E. ii. 6, etc.
- Sozomenus, H. E. iii. 3, etc.
- Atanasi wa Aleksandria, Hist. Arian. ad Monach. 275;
- Giovanni Domenico Mansi, Concil. i. 1275.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |