Parthenon
Parthenone (Kigiriki: Παρθενών) ni hekalu kwenye Akropoli mjini Athens iliyojengwa wakati wa Ugiriki ya Kale. Ni kati ya majengo mashuhuri duniani na kielelezo wa sanaa na usanifu wa Ugiriki ya Kale.
Ilikuwa hekalu ya mungu wa kike Pallas Athena aliyeabudiwa kama mungu mlinzi kwa mji wa Athens ya kale.
Hekalu ilijengwa katika karne ya 5 KK baada ya ushindi wa Wagiriki juu ya Waajemi. Wagiriki waliamini ya kwamba mungu Pallas Athena aliwaokoa. Baadaye serikali ya Athens ilitumia kama jengo la kutunza hazina ya dola.
Baada ya uenezaji wa Ukristo hekalu iligeuzwa kuwa kanisa katika karne ya 6 KK. Baada ya Waosmani kutawala Ugiriki waliitumia kama ghala ya baruti kwa jeshi lao. Katika vita kati ya jamhuri ya Venesia na Milki ya Osmani hekalu ilipigwa na bunduki na mlipuko ulitokea uliovunja sehemu ya jengo.
Sehemu za mapambo ya nje ambayo ni uchongaji wa mawe zilipelekwa Uingereza mwaka 1807 na zinaonyeshwa katika makumbusho ya Britania mjini London. Serikali ya Ugiriki inadai kurudishwa kwa sehmu hizi.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ugiriki bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Parthenon kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Parthenon kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |