Papa Adeodato I
Papa Adeodato I (pia Adeodatus, Deodatus, Deusdedit) alikuwa Papa kuanzia tarehe 19 Oktoba 615 hadi kifo chake tarehe 8 Novemba 618[1]. Alitokea Roma, Italia[2]. Jina la baba yake lilikuwa Stephanus, ambaye alikuwa shemasi mdogo.
Alimfuata Papa Bonifasi IV akafuatwa na Papa Bonifasi V.
Kabla ya kuchaguliwa, alitoa huduma ya kipadri kwa miaka 40[3]. Alikuwa padri wa kwanza kuchaguliwa kuwa Papa tangu Yohane II mwaka 533. Baadaye alikuza idadi ya mapadri na kuwapa nafasi zilizokuwa zimeshikwa na wamonaki kadiri ya sera ya Papa Gregori I na Papa Bonifasi IV[4][3].
Kweli alijulikana kwa kupenda wakleri na waumini wake pamoja na unyofu na hekima yake [5].
Matumizi ya kwanza ya mihuri ya risasi au bullae kwenye nyaraka za Kipapa yanahusishwa naye.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[6].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[7].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Mapapa
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ 3.0 3.1 Attwater, Aubrey (1939). A Dictionary of Popes: From Peter to Pius XII. uk. 66. ISBN 0199295816.
- ↑ Jeffrey Richards, The Popes and the Papacy in the Early Middle Ages (London: Routledge and Kegan Paul, 1979), p. 262
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/76800
- ↑ Philips, Fr Andrew. "The Holy Orthodox Popes of Rome". orthodoxengland.org.uk. Iliwekwa mnamo 2018-03-17.
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Adeodato I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |