Nenda kwa yaliyomo

Mkuku (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa maana mengine ya jina hili angalia hapa Mkuku

Nyota za kundinyota Mkuku (Carina) katika sehemu yao ya angani

Mkuku (kwa Kilatini na Kiingereza Carina) [1]. ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kusini ya dunia yetu.

Carina (Mkuku) ilianzishwa kama kundinyota la pekee katika karne ya 18 kwa hiyo haikujulikana vile kwa mabaharia Waswahili ambayo hata hivyo waliotumia nyota zake kutafuta njia baharini wakati wa usiku.[2]

Hadi karne 19 kundinyota hili lilitazamiwa kuwa sehemu ya kundinyota kubwa zaidi lililoitwa Argo Navis, mara nyingi pekee "Navis" (yaani merikebu) iliyokuwa moja ya makundinyota 48 yaliyoorodheshwa na Klaudio Ptolemaio. Waarabu waliita Safina au Markab. Lacaille alihesabu ndani yake nyota 180 zilizokuwa nyingi mno kwa kuzitaja kwa majina ya Bayer na hivyo alianza tayari kugawa Argo Navis kwa sehemu tatu za Tanga (Vela), Shetri (Puppis) na Mkuku (Carina). Hii ilithibitishwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia katika orodha ya makundinyota 88 ya kisasa yaliyotolewa mwaka 1930. [3] [4]

“Carina” inataja mkuku ambao ni sehemu ya chini kabisa ya chombo cha majini.

Mahali pake

[hariri | hariri chanzo]

Mkuku - Carina iko katika ukanda wa Njia Nyeupe, karibu na kundinyota la Salibu (Crux), si mbali na ncha ya anga ya kusini.

Inapakana na kundinyota jirani ya Kinyonga (Chamaeleon), Nzi (Musca), Kantarusi (Centaurus), Tanga (Vela), Shetri (Puppis), Mchoraji (Pictor) na Panzimaji (Volans).

Mkuku - Carina ni kundinyota kubwa lenye nyota nyingi. Suheli (Carina) au α Carinae ni nyota angavu sana , ni ya pili kwenye anga ya usiku baada ya Shira (Sirius). Ina mwangaza unaoonekana wa mag -0.72 ikiwa umbali wa miakanuru 310 na Dunia[5][6].

Eta Carinae ni nyota maradufu ya nyota mbili au zaidi iliyowaka ghafla mwaka 1843 ikaonekana angavu kushinda Suheli[7]. Sasa nyota zake zimo ndani ya nebula Homunculus ambayo ni wingu angavu lililobaki baada ya mlipuko wa supanova ile. [8]


Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miakanuru)
Aina ya spektra
α Canopus, Suhail, Suhel -0,62 310 F0 Ib
β Beta Carinae au Miaplacidus 1,67 113 A2 IV
ε Epsilon Carinae au Avior 1,86 632 K3 III + B2 V
ι Iota Carinae au Aspidiske 2,21 700 A9 Ib


  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya "Carina" katika lugha ya Kilatini ni "Carinae" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Carinae, nk.
  2. ling. Knappert 1993
  3. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Oktoba 2017
  4. "The IAU list of the 88 constellations and their abbreviations" ya mwaka 1922, iliangaliwa Mei 2017
  5. Canopus], tovuti ya Constellation Guide, iliangaliwa Oktoba 2017
  6. Canopus (Alpha Carinae), Tovuti ya Prof. Jim Kaler
  7. Star Tales - Carina, tovuti ya Ian Ridpath
  8. Eta Carinae, tovuti ya Constellation Guide

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, “Argo Navis” ukurasa 63 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331