Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro |
|
Mahali pa Mkoa wa Morogoro katika Tanzania | |
Majiranukta: 8°0′S 37°0′E / 8.000°S 37.000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Wilaya | 8 |
Mji mkuu | Morogoro |
Serikali | |
- Mkuu wa Mkoa | |
Eneo | |
- Jumla | 73,039 km² |
Idadi ya wakazi (2022) | |
- Wakazi kwa ujumla | 3,197,104 |
Tovuti: http://www.morogoro.go.tz/ |
Morogoro ni jina la mto, mji, wilaya na mkoa wa Tanzania.
Mkoa wa Morogoro ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 67000.
Umepakana na mikoa ya Tanga, Pwani, Lindi, Ruvuma, Iringa, Dodoma na Manyara.
Eneo lake ni km² 72 939, ambapo kuna wakazi 3,197,104 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 [1] (kutoka 2,218,492 wa mwaka 2012). Hivyo Morogoro ni kati ya mikoa mikubwa na yenye wakazi wengi zaidi ya Tanzania.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Eneo la Mkoa wa Morogoro liko katikati ya mikoa ya pwani ya Bahari Hindi na Nyanda za Juu za Kusini Tanzania.
Kuna tambarare za chini kama vile Ifakara / Kilombero, pia milima ya juu kama Uluguru yenye mlima wa Kimhandu wenye mita 2646 juu ya UB.
Mito mikubwa ni Wami na Ruvu inayoanza kwenye milima ya Uluguru. Ruvu ndio mto wa kutoa maji kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Karibu nusu ya eneo la Mkoa wa Morogoro ni hifadhi za taifa za Mikumi na sehemu ya eneo la Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na la ile ya Udzungwa.
Utawala
[hariri | hariri chanzo]Mkoa una wilaya tisa ambazo ndizo (katika mabano idadi ya wakazi mwaka 2022): Gairo (268,205), Kilosa (617,032), Malinyi (225,126), Mlimba (292,536), Morogoro Vijijini (387,736), Morogoro Mjini (471,409), Mvomero (421,741), Ulanga (232,895).
Wakazi walio wengi hukalia wilaya za kaskazini. Zaidi ya robo huishi katika miji ya mkoa.
Ramani | Wilaya au manisipaa | Wakazi (2002) | Tarafa | Kata | Kijiji | Eneo km² |
---|---|---|---|---|---|---|
Wilaya ya Kilombero | 321,611 | 5 | 19 | 81 | 14,918 | |
Wilaya ya Kilosa | 489,513 | 9 | 37 | 164 | 14,245 | |
Wilaya ya Morogoro Vijijini | 263,920 | 6 | 25 | 132 | 11,925 | |
Wilaya ya Morogoro Mjini | 227,921 | 1 | 19 | - | 531 | |
Wilaya ya Mvomero | 260,525 | 4 | 17 | 101 | 7,325 | |
Wilaya ya Ulanga | 193,280 | 5 | 24 | 65 | 24,560 | |
Jumla | 1,759,809 | 30 | 141 | 543 | 73,039 | |
Makisio ya idadi ya watu kwa mwaka 2008 ni watu 2,021,714 kutokana na kiwango cha ongezeko la watu la asilimia 2.6 kwa mwaka. | ||||||
Marejeo: Mkoa wa Morogoro |
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Kabila kubwa ni la Waluguru waliotoa jina kwa mji wa Morogoro pamoja na milima ya Uluguru.
Makabila mengine makubwa zaidi ni Wangulu, Wakagulu, Wasagala, Wapogolo, Wandamba, Wabena, Wambungu, Wakutu na Wavidunda.
Upande wa dini, karibu nusu ni Waislamu na nusu ni Wakristo.
Mawasiliano
[hariri | hariri chanzo]Barabara Kuu za lami za Dar es Salaam - Morogoro - Mbeya - Zambia/Malawi na Dar es Salaam - Morogoro - Dodoma hupita eneo la mkoa pamoja na reli ya kati Dar es Salaam - Morogoro - Dodoma - Kigoma / Mwanza. Reli ya TAZARA hupita wilaya ya Kilombero.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Ardhi ya Morogoro ina takribani rutuba ya kufaa kwa mazao mengi. Lakini kilimo kinategemea hali ya mvua.
Karibu nusu ya eneo la mashamba yote hulimwa mahindi.
Mazao ya sokoni hulimwa milimani.
Mkoa wa Morogoro ni eneo lililojaliwa na Mungu kwa uzalishaji wa sukari kwa wingi. Hasa Wilaya ya Kilombero ina mashamba makubwa ya miwa.
Majimbo ya bunge
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Gairo : mbunge ni Ahmed Shabiby (CCM)
- Kilombero : mbunge ni Peter Lijualikali (Chadema)
- Kilosa : mbunge ni Baraka Bawazir (CCM)
- Mikumi : mbunge ni Joseph Haule (Chadema)
- Mlimba : mbunge ni Suzan Kiwanga (Chadema)
- Morogoro Kusini : mbunge ni Prosper Joseph Mbena (CCM)
- Morogoro Kusini Mashariki : mbunge ni Omar Tibweta Mgumba (CCM)
- Morogoro Mjini : mbunge ni Abood Mohamed Abdul Aziz (CCM)
- Mvomero : mbunge ni Ahmed Sadiq Murad (CCM)
- Ulanga Magharibi/ Malinyi : mbunge ni Dk. Hadji Mponda (CCM)
- Ulanga Mashariki : mbunge ni Goodluck Mlinga (CCM)
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Morogoro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |