Mitume Petro na Paulo
Mwaka wa liturujia |
---|
Magharibi |
Mashariki |
Sherehe ya Mitume Petro na Paulo ni sikukuu ya fahari kwa heshima ya kifodini cha watakatifu hao kilichotokea mjini Roma katika miaka ya 60 BK kutokana na dhuluma dhidi ya Wakristo ambayo ilianzishwa na Kaisari Nero mwaka 64 na kuendelea hadi alipojiua mwaka 68.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Tangu zamani sana sikukuu hiyo inaadhimishwa kila tarehe 29 Juni, ikiwaunganisha ingawa hawakuuawa pamoja[1][2].
Kadiri ya mapokeo, mtume Petro alitangulia kuuawa kwa kusulubiwa kichwa chini miguu juu katika mtaa wa Vatikano, ambapo sasa limesimama basilika lake ambalo ni kanisa kubwa kuliko yote duniani.
Mtume Paulo aliuawa baadaye kwa kukatwa kichwa nje kidogo ya ngome ya mji. Sehemu hiyo kwa heshima yake lipo basilika lingine kubwa lililojengwa juu ya kaburi lake.
Adhimisho
[hariri | hariri chanzo]Kwa Wakatoliki ni sikukuu ya amri, yaani inayodai kila mwamini ashiriki Misa, ingawa Baraza la Maaskofu linaweza kusamehe amri hiyo kwa wakazi wa eneo lake kama kalenda ya serikali haiadhimishi kama sikukuu ya taifa.[3]
Katika Ukristo wa mashariki ndio mwisho wa mfungo wa Mitume.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ The Catholic Encyclopedia, Volume XI (Robert Appleton Company, New York, 1911), s.v. "St. Paul", accessed 2007-06-04.
- ↑ Codex Iuris Canonici (1983), canon 1246.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- The Holy Glorious and All-Praised Leader of the Apostles, Peter & Paul Icon and Synaxarion of the Feast (Orthodox)
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mitume Petro na Paulo kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |