Mason Finley
Mason Finley (alizaliwa Kansas City, Missouri, 7 Oktoba 1990) ni mrusha tufe na mrusha kisahani wa Marekani. Alikuwa kwenye timu ya riadha ya chuo kikuu Kansas kabla ya kuhamia Chuo Kikuu cha Wyoming. Alikuwa na vigezo kurusha kisahani kwenye olimpiki ya majira ya joto mwaka 2020.
Maisha ya ujana
[hariri | hariri chanzo]Finley alisoma shule ya sekondari Buena Vista (ambako alicheza mpira wa kikapu na mpira wa miguu) huko Buena Vista, Colorado baada ya hapo alijiunga na chuo kikuu Kansas kabla ya kuhamia chuo kikuu Wyoming.[1]
Kwa umahiri wake akiwa shule ya sekondari,Finley alitajwa kwenye ESPN RISE kama timu ya riadha kwa shule za sekondari kwa miongo yote miaka ya 2000. Pia alikuwa mwanariadha wa mwaka 2009 kwa shule za sekondari kwenye Track and Field News.[2]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Finley aliweka rekodi ya shule ya sekondari Colorado kwenye kurusha kisahani kwa kurusha kwa futi 236 na inchi 6(mita 72.09) katika High Altitude Challenge huko Alamosa, Colorado.Pia alishinda medali ya dhahabu katika kurusha tufe na kurusha kisahani kwenye michuano ya ya riadha ya vijana Pan Amerika mwaka 2009 iliyofanyika bandari ya Hispania, Trinidad. Kama kijana akiwa Kansas alikuwa mmarekani pekee kwenye kurusha tufe na kisahani. Urushaji wake mzuri ilikuwa mita 60.12(futi 197-3) kwenye kisahani na mita 20.68 (futi 67-10.25) kwenye tufe.
Mwaka 2017 Finley alishinda medali ya shaba kwenye tukio la kurusha kisahani katika michuano ya dunia huko London, akirusha mita 68.03.Hii iliondoa ukame wa miaka 18 wa kutokuwa na mmarekani mwenye medali kwenye kurusha kisahani na ikawa mara ya kwanza mmarekani kushika nafasi kwenye kurusha kisahani kwa wanaume tangu michuano ya dunia huko Sevilla, ambapo Anthony Washington alishinda medali ya dhahabu.[3]
Alifuzu kwa olimpiki ya majira ya joto mwaka 2020 akiwa nwa kwanza kwa vigezo kwa urushaji wa mita 63.07(futi 206.9).[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Letters: August 27, 1821-February 22, 1836", The Hargrave Correspondence, 1821-1843, Champlain Society, ku. 1–230, 2013-01, iliwekwa mnamo 2021-10-04
{{citation}}
: Check date values in:|date=
(help) - ↑ Brügger, Niels; Laursen, Ditte; Nielsen, Janne (2016-06-13). "Methodological reflections about establishing a corpus of the archived web: the case of the Danish web from 2005 to 2015". Researchers, practitioners and their use of the archived web. School of Advanced Study, University of London. doi:10.14296/resaw.0009.
- ↑ Dapena, J. (1998-05). "THE START OF THE FINAL PROPULSION IN THE DISCUS THROW". Medicine & Science in Sports & Exercise. 30 (Supplement): 129. doi:10.1097/00005768-199805001-00737. ISSN 0195-9131.
{{cite journal}}
: Check date values in:|date=
(help) - ↑ Manzenreiter, Wolfram (2020-04-23), "Climbing", Japan Through the Lens of the Tokyo Olympics, Routledge, ku. 25–25, iliwekwa mnamo 2021-10-04