Kifungambuzi
Mandhari
Kifungambuzi | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kishungi cha kifungambuzi
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Kifungambuzi (Eleusine indica) ni spishi ya nyasi katika nusufamilia Chloridoideae. Asili kamili ya nyasi hili haijulikani kwa uhakika lakini yumkini linatoka Afrika au labda Asia. Siku hizi linatokea mahali popote kwa kanda za tropiki na nusutropiki. Spishi hii ni gugu baya shambani na imeanza kupinga viuamimea, kama glyphosate. Wanyama wafugwao hula nyasi hili lakini wakila mingi wanaweza kuugua kwa sababu ya sumu ndani ya majani (glycosides).
Kuna uwezekano mkubwa kama E. indica imezaa E. coracana au mwimbi kwa kuongeza maradufu nambari ya chembeuzi. Kwa hivyo mwimbi ni tetraploidi. Hata punje za kifungambuzi zinaweza kuliwa na hutumika pengine wakati wa uhaba wa chakula.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Taarifa kutoka PROTA Archived 5 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- Taarifa kutoka Feedipedia
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Masuke
-
Visuke
-
Picha ya kisuke iliyofafanuka
-
Masuke yaliyokauka