Kifimbo (samaki)
Kifimbo | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kifimbo wa kawaida (Albula vulpes)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 11 zilizopo:
|
Vifimbo, chache, minyimbi, manyimbi, manyimbwi, mkizi waume au panya ni samaki wa baharini katika jenasi Albula ya familia Albulidae.
Tabia
[hariri | hariri chanzo]Kifimbo wa pwani za Afrika ya Mashariki ni mkubwa kuliko spishi zote nyingine na ana uzito wa kipeo wa kg 10.0 na urefu wa sm 104. Spishi nyingine ni sm 25-50 kwa kipeo. Rangi yao ni ya fedha kwenye mbavu na kijivu hadi kijani-zaituni mgongoni. Kijivu kwenye magamba huunda mistari myanana myembamba mara nyingi ambayo hunyumbuka urefu wa mbavu kutoka kwa matamvua mpaka mkia. Vitako vya mapezi mbavuni pengine ni njano.
Mwenendo
[hariri | hariri chanzo]Spishi hizi huishi maji ya kitropiki karibu na pwani na huenda kwenye pwa-tope ili kujilisha wakati wa maji maundifu. Samaki wazima na wachanga wanaweza kuwa pamoja katika makundi, na wanaweza kupatikana kwa peke yao au kwa jozi.
Vifimbo hula nyungunyungu-bahari, samaki wachanga, gegereka na moluska. Miamba, magenge na vitalu safi vya nyasi-bahari ina mawindo madogo tele kama vile kaa na uduvi. Wanaweza kufuata shepwa ili kukamata wanyama wadogo wanaowafukuza kutoka kwenye mchanga wa sakafu.
Vifimbo na binadamu
[hariri | hariri chanzo]Uvuvi wa vifimbo kwa kutumia chambo cha nzi bandia ni mchezo maarufu katika Bahamas na kusini mwa Florida. Zamani uvuvi huu ulikuwa maarufu kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki pia lakini siku hizi vifimbo wamekuwa nadra. Kwa sababu vifimbo huishi katika maji kame ya pwani, uvuvi unaweza kufanywa kwa kutembea kwenye maji au kutoka mashua yasiyoingia maji sana. Uvuvi huu unafanyika kwa ajili ya michezo kwa kawaida, kwa hivyo samaki huachwa, lakini wanaweza kuliwa pia. Mapishi ya mfano ni samaki aliyegawanyika na kukolewa na mchuzi wa pilipili na chumvi halafu kuokwa.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Albula glossodonta, Kifimbo Pua-fupi (Shortjaw bonefish)
- Albula goreensis, Kifimbo Magharibi (West African bonefish)
- Albula oligolepis, Kifimbo Magamba-madogo (Smallscale bonefish)
- Albula vulpes, Kifimbo wa Kawaida (Bonefish)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Albula argentea (Silver sharpjaw bonefish)
- Albula esuncula (Eastern Pacific bonefish)
- Albula gilberti (Cortez bonefish)
- Albula koreana (Korean bonefish)
- Albula nemoptera (Threadfin bonefish)
- Albula pacifica (Pacific shafted bonefish)
- Albula virgata (Hawaian or longjaw bonefish)
Spishi za kabla ya historia
[hariri | hariri chanzo]- Albula bartonensis
- Albula bashiana
- Albula campaniana
- Albula dunklei
- Albula eppsi
- Albula oweni
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kifimbo magamba-madogo
-
Pacific shafted bonefish
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
- Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.