Kampuni ya Viatu ya Brown
Kampuni ya Viatu ya Brown | |
---|---|
Jina la kampuni | Kampuni ya Viatu ya Brown |
Mwanzilishi | George Warren Brown Alvin Bryan |
Huduma zinazowasilishwa | Utengenezaji |
Makao Makuu ya kampuni | Clayton,Missouri |
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii | Viatu |
Nchi | Marekani |
Tovuti | http://www.brownshoe.com/ |
Kampuni ya Viatu ya Brown [1] ni kampuni ya viatu ambayo inamiliki aina mbalimbali ya viatu nchini Marekani na Kanada. Makao yake makuu yanapatikana Clayton, Missouri ,kitongoji kidogo kilichokuwa karibu na St. Louis, Missouri.
Asili ya kampuni
[hariri | hariri chanzo]Kampuni hii ilianzishwa katika eneo la St. Louis na hapo awali iliitwa Bryan, Brown & Company kwa makumbusho ya waanzilishi George Warren Brown na Alvin Bryan. Jina lilibadilishwa kuwa Kampuni ya Viatu ya Brown katika mwaka wa 1893. Shule ya George Warren Brown ya Kazi kwa Jamii ilianzishwa katika Chuo Kikuu cha Washington huko St. Louis katika mwaka wa 1925 na mjane wake GW Brown.
Uendeshaji wa biashara.
[hariri | hariri chanzo]Kampuni ya Viatu ya Brown, ni kampuni ya thamani ya $ bilioni 2.4 ikiwa na operesheni zake kote duniani. Kampuni hii inaendesha mnyororo wa maduka 1100 ya Famous Footwear. Inaendesha ,pia, maduka 300 maalum ya rejareja nchini Marekani, Uchina na Kanada chini ya majina kama Brown Shoe Closet, FX LaSalle , Franco Sarto na ,pia, Shoes.com (tovuti rasmi ya kibiashara ya kampuni). Sehemu za kampuni hii za kuuza bidhaa kwa wingi na ,pia, zenye viatu maarufu ni kama Naturalizer, LifeStride, Via Spiga, Nickels Soft, Connie na Buster Brown. Kampuni hii ina leseni ,pia, ya uuzaji wa viatu vinavyojulikana sana vya watu wazima kama Franco Sarto, Etienne Aigner, Dr. Scholl's, Carlos ya Carlos Santana na Fergie. Vilevile, inauza viatu vya watoto vya Barbie na Nickelodeon.
Katuni za kuwakilisha kampuni
[hariri | hariri chanzo]Tangu mwaka wa 1904, katuni za kuwakilisha kampuni zimekuwa Buster Brown na mbwa wake, Tige(angalia picha kule juu). Wote wawili huonekana kwenye matangazo ya televisheni ya kampuni. Katika miaka ya 1940 na 1950, kampuni iliingia ,kwa muda mfupi, katika uchapishaji wa magazeti yenye michoro ya katuni. Magazeti haya yalihusisha katuni maarufu Buster Brown kwenye ukurasa wa kwanza ingawa hekaya zingine pia zilichorwa katika machapisho haya, kama zile za Robin Hood.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ^ "Clayton city, Missouri." Archived 6 Septemba 2009 at the Wayback Machine. U.S. Census Bureau.
- ^ "We're Brown Shoe." Brown Shoe Company.