Kali
Kali (kalium; potassium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Kali (kalium; potassium) |
Alama | K |
Namba atomia | 19 |
Mfululizo safu | Metali alikali |
Uzani atomia | 39.098 |
Densiti | 0.89 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 336.53 K (63.38 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 1032 K (759 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 2.4 % |
Hali maada | imara |
Kali (pia: potasiamu, ing. potassium) ni elementi na metali alikali yenye namba atomia 19 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 39.098. Alama yake ni K.
Kali - potasiamu
[hariri | hariri chanzo]Jina Kali latokana na neno la Kiarabu "qalia" kwa majivu lakini jina la potasiamu ni kawaida vilevile kutokana na neno "potassium" kwa sababu kampaundi zake zimo kwa wingi ndani ya majivu ya ubao yaliyosafishwa kwa kuchemsha katika sufuria (Kiing.: "ash" na "pot").
Tabia
[hariri | hariri chanzo]Kali (potasiamu) ni metali laini sana inayochemka kwa sentigredi 83 tayari. Rangi yake ni nyeupe-fedha. Haipatikana kiasili kama metali tupu kwa sababu humenyuka haraka na kuoksidika hewani. Inamenyuka vikali sana na maji hivyo kali metali hutunzwa chini ya mafuta.
Matumizi
[hariri | hariri chanzo]Aloi ya kali na natiri hutumiwa kama kiowevu cha kupoza mitambo ya nyuklia.
Chumvi za kali hutumiwa sana kama mbolea wa kilimo.
Kali (Potasiamu) ni muhimu hasa katika chembe za mimea na wanyama. Lazima kuwepo katika chakula chetu lakini si mno kwa sababu ikizidi inaleta hasara.
-
Kali ina rangi ya kifedha-nyeupe lakini hubadilika rangi hewani mara moja
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |