John Kerry
Mandhari
John Forbes Kerry (amezaliwa 11 Desemba, 1943) ni mwanasiasa wa Marekani akiwa mwanachama wa Chama cha Kidemokrasia. Miaka ya 1983 na 1984 alihudumia kama kaimu gavana wa Massachusetts chini ya Michael Dukakis. Kuanzia 1985 hadi 2013 alikuwa mbunge wa Senati ya Marekani akiwakilisha jimbo la Massachusetts. Mwaka wa 2004 aligombea urais lakini akashindwa na Rais George W. Bush. Kuanzia 2013 hadi 2017 Kerry alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje chini ya Rais Barack Obama.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu John Kerry kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |