Jack Ma
'
Jack Ma Yun | |
---|---|
Jack Ma mnamo mwaka 2018 | |
Amezaliwa | 10 Septemba 1964 |
Majina mengine | Ma Yun |
Kazi yake | Mfanyabiashara |
Jack Ma Yun (alizaliwa 10 Septemba 1964) ni mfanyabiashara na mwekezaji wa nchini China. Ni mwanzilishi na mwenyekiti wa zamani wa Alibaba Group, kampuni kubwa ya kimataifa ya masuala ya teknolojia. Pia alikuwa mwanzilishi mwenza wa Yunfeng Capital, kampuni binafsi ya hisa nchini China.
Kulingana na Bloomberg Billionaires Index,[1] mnamo Januari 2023, inakadiliwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 34.1, hivyo na kuwa mtu wa tano kwa utajiri nchini China (baada ya Zhong Shanshan, Zhang Yiming, Ma Huateng na Robin Zeng), na pia mtu wa 34 kwa utajiri duniani.
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Jack Ma alizaliwa kwa jina la Ma Yun huko Hangzhou, Zhejiang mnamo Septemba 10, 1964.[2] Alianza kupenda Kiingereza tangu akiwa kijana mdogo na akaanza kufanya mazoezi na wazungumzaji wa Kiingereza katika hoteli ya Hangzhou International. Babu yake alifanya kazi kama mlinzi wakati wa vita vya pili vya China na Japan. Akiwa na umri wa miaka 12,alinunua redio ndogo na akaanza kusikiliza vituo vya redio vya Kiingereza kila siku. Kwa miaka tisa, alikuwa akiendesha baiskeli katika ziara za watalii katika eneo hilo na kufanya mazoezi ya Kiingereza. Akawa rafiki wa mmoja wa watalii hao, ambaye alimwita "Jack" kwa sababu aliona ni vigumu kutamka jina lake la Kichina.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Bloomberg Billionaires Index: Jack Ma", Bloomberg.
- ↑ cite encyclopedia|title=Jack Ma|encyclopedia=Encyclopedia Britannica|url=https://www.britannica.com/biography/Jack-Ma%7Cdate=September 6, 2022|access-date=September 9, 2022}}
- ↑ Mookherji, Kalyani (2008). [[[:Kigezo:Google books]] Brief biography of Jack Ma]. Prabhat Prakashan.
{{cite book}}
: Check|url=
value (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jack Ma kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |