Djemila
Mandhari
Djemila (kar.: جميلة "mzuri, unaopendeza") ni kijiji katika Algeria ya kaskazini penye maghofu ya Curculum (pia: Cuicul) uliokuwa mji wa Roma ya Kale katika jimbo la Numidia. Maghofu yamepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia tangu 1982.
Curculum iliundwa mnamo mwaka 97 BK kama koloni ya Kiroma wakati wa Kaisari Nerva. Mji ulistawi vizuri hadi kuvamiwa na Wavandali 431. Baadaye ilitekwa na jeshi la Bizanti lakini iliendelea kupungua. Iliachwa tayari kabla ya kufika kwa Waarabu katika karne ya 7.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti ya UNESCO
- Habari na picha za ziada Archived 11 Februari 2006 at the Wayback Machine. (kifaransa)
- Tovuti ya makumbusho ya Djemila Archived 11 Septemba 2007 at the Wayback Machine.