Chanjo ya Homa ya Manjano B
Chanjo ya Homa ya Manjano B ni chanjo ambayo huzuia homa ya manjano B.[1] Kiwango cha kwanza kinapendekezwa kuwa ndani ya saa 24 baada ya kuzaliwa na kisha viwango viwili au vitatu kutolewa baada ya hicho. Hii inajumuisha wale ambao wana kinga duni mwilini kama vile kutokana na virusi vya UKIMWI na wale waliozaliwa kabla ya siku ya kuzaliwa kufika. Kwa watu walio na afya nzuri, chanjo ya mara kwa mara hufanya watu zaidi ya 95% kukingwa dhidi ya ugonjwa huo.[1]
Kupima damu ili kuthibitisha kwamba chanjo hiyo imefanya kazi kunapendekezwa kwa wale walio katika hatari ya juu. Viwango vya ziada vinaweza kuhitajika kwa watu walio na kinga duni japo si muhimu kwa watu wengi. Kwa wale ambao wamekuwa kwenye hatari ya homa ya manjano ya B japo hawajapewa chanjo, wanafaa kupewa kinga ya homa ya manjano ya B ya protini za damu juu ya chanjo. Chanjo hii hutolewa kwa kudunga sindano kwenye misuli.[1]
Madhara hatari yanayotokana na chanjo ya homa ya manjano ya B si kawaida sana. Uchungu unaweza kutokea katika sehemu iliyodungwa sindano. Ni salama kwa matumizi wakati wa ujauzito au unaponyonyesha. Haijahusishwa na dalili ya Guillain-Barre. Chanjo za sasa zimetengenezwa kwa ufundi wa viumbe vya msimbo-jeni vinavyoungana tena. Zinapatikana peke yao na kwa mchanganyiko na chanjo nyingine.[1]
Chanjo ya kwanza ya Homa ya manjano B iliidhinishwa Marekani mwaka wa 1981.[2] Toleo salama lilikuja sokoni mwaka wa 1986.[1] Ipo kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika La Afya Duniani, dawa muhimu zaidi inayohitajika kwenye mfumo wa kimsingi wa afya.[3] Gharama ya jumla ni kati ya dola 0.58 na 13.20 kwa kila kiwango mwaka wa 2014. Gharama yake Marekani ni kati ya dola 50 na dola 100.[4]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Hepatitis B vaccines WHO position paper" (PDF). Weekly epidemiological record. 40 (84): 405-420. 2 Oct 2009.
- ↑ Moticka, Edward. A Historical Perspective on Evidence-Based Immunology. p. 336. ISBN 9780123983756.
- ↑ "WHO Model List of EssentialMedicines" (PDF). World Health Organization. October 2013. Retrieved 22 April 2014.
- ↑ Hamilton, Richart (2015). Tarascon Pocket Pharmacopoeia 2015 Deluxe Lab-Coat Edition. Jones & Bartlett Learning. p. 314. ISBN 9781284057560.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chanjo ya Homa ya Manjano B kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |