Calgary Herald
The Calgary Herald | |
---|---|
Jina la gazeti | The Calgary Herald |
Aina ya gazeti | Gazeti la kila siku |
Lilianzishwa | 31 Agosti ,1883 |
Eneo la kuchapishwa | Calgary |
Nchi | Kanada |
Mwanzilishi | *. Andrew Armour *. Thomas Braden |
Mmiliki | Kampuni ya CanWest Global Communications |
Makao Makuu ya kampuni | Calgary, Alberta |
Nakala zinazosambazwa | *. 115,612 - Kila siku *. 110,737 - Jumapili[1] |
Machapisho husika | *. Neighbours *. Swerve |
Tovuti | http://www.calgaryherald.com/ |
The Calgary Herald ni gazeti la kuchapishwa kila siku lililochapishwa katika mji wa Kanada wa Calgary, Alberta.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Jarida hili lilichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo tarehe 31 Agosti ,1883 na Andrew Armour na Thomas Braden chini ya jina la The Calgary Herald, Mining and Ranche Advocate and General Advertiser. Jarida hili lilianza kama gazeti la kila wiki likiwa na kurasa nne zilizochapishwa kwa kutumia mashine yaliyotumia nguvu ya mikono. Operesheni zilikuwa ndogo, zikitumia hema iliyokuwa kando ya makutano ya mito Bow na Elbow kama ofisi yake. Katika mwaka wa 1885, Herald likawa gazeti la kuchapishwa kila siku lakini uchapishaji huo wa kila siku haukuanza hadi mwisho wa mwaka wa 1883. Tangu wakati huo mpaka Aprili 1985, lilikuwa gazeti la alasiri lakini hivi sasa ni gazeti linalosambazwa asubuhi. Mnamo Novemba 2000, gazeti la Herald likawa sehemu ya Kampuni ya Magazeti ya Southam (hivi sasa linaitwa Canwest News Service ambao ni mgawanyiko wa kampuni ya mawasiliano ya CanWest Global Communications)
Gazeti la Herald ,pia, huchapisha gazeti la kila wiki la jamii la Neighbours (Swahili: Majirani) ambalo husambazwa pamoja na Herald katika maeneo (lakini si yote) ya Calgary, na gazeti la Swerve la kila wiki. Katika mwaka wa 2005, gazeti la Herald liliungana na kampuni shirika za CanWest Global katika kuanzisha gazeti la Dose. Dose lililenga wasafiri takriban 20; liliacha kuchapishwa baada ya mwaka mmoja.
Tarehe 8 Novemba 1999, wafanyikazi ,waliokuwa wameunda muungano yao hivyo majuzi, walifanya mgomo. Mgomo huo uliendelea hadi mwezi wa Julai 2000 huku wanahabari wengi wa Herald wakitoka katika gazeti hilo. Baadhi yao walikubali malipo ya kutoka kampuni ilhali wengine walirudi kazini huku muungano wao ukibanduliwa.[2] Nafasi za waandishi wengi mashuhuri zilichukuliwa na wafanyikazi wachanga katika kazi hiyo. Ilichukua miaka kadhaa kabla ya gazeti la Herald kupata wasomaji wake tena baada ya mgomo. Wafanyikazi wengi wa zamani wa Herald waliotoka wakti wa au baada ya mgomo huweza kupatikana katika majarida mengine mbalimbali ,hasa jarida la kibiashara la kila wiki ,Business Edge.
Katika siku za 29 Aprili hadi 31 Agosti 2008, Herald lilichapishwa kurasa za mbele za zamani katika makumbusho ya mwaka wake wa 125 (1883 - 2008).
Usambazaji wa nakala
[hariri | hariri chanzo]Calgary Herald ni mojawapo wa magazeti mawili yanayohudumia eneo hilo la Calgary. Gazeti la pili ni lile la Calgary Sun. Usambazaji hufanyika kwa njia ya kuagiza, uuzaji kwa maduka ya mgazeti ama kwa kutumia sanduku la gazeti. Mtindo huo wa masanduku ya magazeti ulileta mjadala mkali kutoka Halmashauri ya Jiji katika mwanzo wa mwaka wa 2008 baada ya kiongozi mmoja kudai kuwa masanduku hayo yalisababisha maongezeko ya takataka.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- The Calgary Herald Archived 13 Februari 2010 at the Wayback Machine.
- Mapitio ya Ryerson ya Uandishi Archived 22 Machi 2008 at the Wayback Machine.