Antioko Epifane
Mandhari
Antioko IV wa Syria alijiita Epifane (kwa Kigiriki Ἀντίοχος Ἐπιφανής) akitaka kujitambulisha kama tokeo la mungu mmojawapo. Lakini watu walimuita Epimane, yaani kichaa, kutokana na madai yake yasiyo na kiasi.
Aliishi miaka 215 KK – 164 KK akitawala dola la Waseleuki kuanzia mwaka 175 KK hadi kifo chake.
Juhudi zake za kueneza ustaarabu wa Ugiriki wa kale kati ya Wayahudi zilishindwa na Wamakabayo waliopigania uhuru wa dini kama inavyosimuliwa katika kitabu cha kwanza cha Wamakabayo na kitabu cha pili cha Wamakabayo (ambavyo ni kati ya Deuterokanoni).
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Antiochus IV Ephiphanes entry in historical sourcebook by Mahlon H. Smith
- Jewish Encyclopedia: Antiochus IV Epiphanes
- Antiochus IV Epiphanes at livius.org