Zirikoni
Zirikoni ni elementi na metali ya mpito yenye namba atomia 40 katika mfumo radidia. Hutokea ndani ya mitapo na rangi yake ni nyeupe-kijivu ikisafishwa.
Zirikoni (Zirconium) | |
---|---|
Fuwele za Zirikoni tupu
| |
Jina la Elementi | Zirikoni (Zirconium) |
Alama | Zr |
Namba atomia | 40 |
Mfululizo safu | Metali ya mpito |
Uzani atomia | 91.224 |
Valensi | 2, 8, 18, 10, 2 |
Densiti | 6.52 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 2128 K (1855 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 4682 K (4409 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 0.016 % |
Hali maada | mango |
Tabia
haririHutokea katika mitapo ya miamba kama graniti na zaidi kama mashapo. Kwa kawaida hutokea pamoja na elementi ya Hafni. Ni metali ngumu inayofanana na Titani haibabuiki kirahjisi.
Huchimbwa hasa Australia na Afrika Kusini.
Matumizi
haririMatumizi yake ni hasa katika teknolojia ya tanuri nyuklia hasa kama koti za nondo za urani ndani ya tanuri nyuklia. Tabia ya kutobabua kirahisi imesababisha pia matumizi yake katika aloi za feleji za pekee kwa mfano kwa ajili ya vifaa vya upasuaji.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zirikoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |