Rodi
Rhodi (pia: Rodi - kutoka Kigiriki rhodeos, "nyekundu kama waridi" kwa sababu kampaundi zake mara nyingi huwa na rangi nyekundu) ni elementi na metali haba duniani. Kikemia ni elementi ya mpito yenye kifupi cha Rh na namba atomia 45 katika mfumo radidia.
Rhodi au Rodi (Rhodium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Rhodi au Rodi (Rhodium) |
Alama | Rh |
Namba atomia | 45 |
Mfululizo safu | Metali ya mpito |
Uzani atomia | 102.9055 |
Valensi | 2, 8, 18, 16, 1 |
Densiti | 12.41 g/cm³ |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 2237 K (1964 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 3968 K (3695 °C) |
Hali maada | mango |
Mengineyo | metali ghali duniani kutokana na uhaba |
Tabia na matumizi
haririRhodi ni metali ngumu yenye rangi nyeupe-kifedha. Haimenyuki kirahisi na asidi au hewa, hivyo hutafutwa kwa kuunda aloi inamoongeza ugumu na kuzuia kuoksidisha kwa aloi.
Kutokana na uhaba na faida zake ni metali ghali kabisa duniani inayouzwa na kununuliwa sokoni.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rodi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |