Kobalti (kutoka Kiingereza cobalt inayotoka Kijerumani kobalt) ni elementi na metali haba duniani. Kikemia ni elementi mpito yenye kifupi cha Co na namba atomia 27 katika mfumo radidia yenye uzani atomia 58.933.

Kobalti
Kobalti
Kobalti
Jina la Elementi Kobalti
Alama Co
Namba atomia 27
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 58.933
Valensi 2, 8, 15, 2
Densiti 8.90 g/cm³
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 1768 K (1495 °C)
Kiwango cha kuchemka 3200 K (2927 °C)
Asilimia za ganda la dunia 4.7 %
Hali maada mango

Kobalti hupatikana mara chache kama metali tupu lakini zaidi ndani ya mitapo hasa za nikeli na shaba.

Tangu kale kampaundi zake hutumiwa kwa rangi na wino mbalimbali, hasa za buluu, kijani na njano. Kampaundi ya CoAl2O4 inatumiwa kutengeneza kioo cha buluu.

Katika karne ya 20 matumizi yalienea katika uzalishaji wa feleji, aloi yake inaongeza ugumu wa feleji.

Tangu kupatikana kwa simu za mkononi na magari ya umeme kobalti imekuwa muhimu sana kwa uzalishaji wa beteri. Hii ilisababisha mlipuko wa soko la kobalti na uchimbaji wake. Mwaka 2016 takriban asilimia 60 za mahitaji yote yalichimmbwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo[1].

Uchimbaji wa kobalti Duniani, nchi kwa nchi (tani)
Land 2006[2] 2013[3] 2016[4]
Australia 6000 6400 5100
Brazil 1000 3000 5800
China 1400 7200 7700
JD Kongo 22000 54000 66000
Kanada 5600 6920 7300
Kuba 4000 4200 4200
Moroko 1500 1700
Kaledonia Mpya 1100 3190 3300
Ufilipino 3000 3500
Urusi 5100 6300 6200
Zambia 8600 5200 4600
Afrika Kusini 3000 3000
nchi nyingine za Dunia 1200 8000 8300
Jumla 57.500 110.000 123.000

Marejeo

hariri
  1. The hottest thing in the markets right now is an obscure metal mined in DR Congo, tovuti ya Quartz.com ya April 27, 2017, iliangaliwa Januari 2018
  2. Cobalt 2007 kwa USGS Mineral Resources.
  3. Cobalt 2014 kwa USGS Mineral Resources
  4. Cobalt 2016 kwa USGS Mineral Resources
  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kobalti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.