Gadolini
Gadolini (Gadolinium) ni elementi ya kikemia yenye alama Gd na namba atomia 64. Gadolini ni metali yenye rangi nyeupe-ya kifedha wakati haijaoksidika bado. Gadolini humenyuka na oksijeni ya hewani au unyevu polepole ikiunda mpako mweusi. Chini ya °C 20 ina tabia za kisumaku.
Kiasili hupatikana hasa kwa umbo la oksidi.
Jina lake limetokana na madini ya gadoliniti inamopatikana; madini yalipewa jina kwa heshima ya moja ya madini ambayo gadolinium hupatikana, yenye jina kwa mwanakemia Johan Gadolin kutoka Uswidi.
Gadolinium ina tabia kadhaa zisizo kawaida. Katika kampaundi za feleji nyongeza ndogo ya Gadolini hupunguza hupunguza utendanaji wake na oksijeni katika hali ya joto.[ <span title="This claim needs references to reliable sources. (June 2019)">onesha inahitajika</span> ]
Kampaundi za gadolini hutumiwa katika mikrowevu, uzalishaji wa diski za kompyuta na pia kwa skrini za rada.
Upatikanaji katika ganda la Dunia ni takribani miligramu 6.2 kwa kila kilogramu. Huchimbwa hasa China, Marekani, Brazil, Sri Lanka, Uhindi na Australia. Uzalishaji wa gadolini safi duniani ni karibu tani 400 kwa mwaka. [1] [2]
Marejeo
hariri- ↑ Deliens, M. and Piret, P. (1982). “Bijvoetite et lepersonnite, carbonates hydrates d'uranyle et des terres rares de Shinkolobwe, Zaïre”. Canadian Mineralogist 20, 231–38
- ↑ "Lepersonnite-(Gd): Lepersonnite-(Gd) mineral information and data". Mindat.org. Iliwekwa mnamo 2016-03-04.
Viungo vya nje
hariri- Mfumo wa Nephrojeni Fibrosis - Ugumu wa Gadolinium MR Tofauti (safu ya picha kwenye wavuti ya MedPix)
- Ni ya kwanza - Gadolinium
- Jokofu hutumia madini ya gadolinium ambayo huwaka inapofunuliwa na shamba la sumaku
- Ushauri wa FDA juu ya tofauti ya msingi wa gadolinium
- Kufikiria Mdom ya tumbo: mazingatio muhimu kwa tathmini ya uimarishaji wa Gadolinium Archived 27 Februari 2012 at the Wayback Machine. Rafael OP de Campos, Vasco Herédia, Ersan Altun, Richard C. Semelka, Idara ya Chuo Kikuu cha Radiology Hospitali ya North Carolina Chapel Hill
- Ndani ya safari ya Kijapani ya Super Kamiokande digrii digrii 34 pamoja na maelezo juu ya kuongeza Gadolinium kwa maji safi kusaidia katika kusoma neutrinos
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gadolini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |