Chromi
Chromi ni elementi na metali yenye namba atomia 24 na alama Cr katika mfumo radidia wa elementi. Ni metali ngumu na bambaikaji yenye rangi ya kifedha-kijivu inayopatikana katika madini na kampaundi mbalimbali.
Chromi | |
---|---|
Fuwele ya Chromi
| |
Jina la Elementi | Chromi |
Alama | Cr |
Namba atomia | 24 |
Mfululizo safu | Metali |
Uzani atomia | 51.9961 |
Valensi | 2, 8, 13, 1 |
Densiti | 7.14 g/cm³ |
Ugumu (Mohs) | 8.5 |
Kiwango cha kuyeyuka | 2180 K (1907 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 2944 K (2671 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 1,9 · 10−2 % |
Hali maada | mango |
Hutumiwa sana katika aloi za feleji na kuongeza ugumu.
Madini ya chromi huchimbwa hasa Afrika Kusini (50 % ya mahitaji yote ya dunia), halafu Kazakhstan (15,2 %), Uhindi (12,1 %), Zimbabwe (3,7 %) na Ufini (3 %).
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chromi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |