Boroni
Boroni ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 5 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 10.811. Alama yake ni B.
Boroni (Boron) | |
---|---|
Jina la Elementi | Boroni (Boron) |
Alama | B |
Namba atomia | 5 |
Uzani atomia | 10,8 u |
Valensi | 2, 3 |
Ugumu (Mohs) | ~9.5 |
Kiwango cha kuyeyuka | 2349 K (2076 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 4200 K (3927 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 0 |
Tabia
haririBoroni ni nusumetali au metaloidi; ina valensi tatu. Elementi peke yake haipatikani katika mazingira asilia duniani ila tu katika kampaundi kama vile borasi (Na2B4O7·10H2O ).
Umbo hobela au la fuwele
haririInapotapaswa kutoka kwa kampaundi zake hupatikana katika umbo hobela kama unga wa rangi ya kahawia au la fuwele nyeusi na ngumu isiyohami umeme. Boroni ni dutu ngumu kuliko zote duniani baada ya almasi na kati ya elementi zote ni imara dhidi ya nguvu ya mvuto.
Matumizi kiteknolojia
haririMatumizi ya boroni ni katika teknolojia ya kihami na katika dawa za kupausha au kung'arisha. Inatumiwa pia kama nyongeza katika aloi kwa ajili ya sehemu za eropleni zinazotakiwa imara ma nyepesi. Katika teknolojia ya kinyuklia hutumiwa kama kinga dhidi ya nyutroni katika matanuri ya nyuklia.
Nafasi ya kibiolojia
haririKwa kiasi kidogokidogo boroni ina kazi katika miili ya wanyama: haijaeleweka ni kazi gani, isipokuwa imeonekana ni muhimu. Asidi ya boroni ni kiuawadudu (insecticide), hasa dhidi ya sisimizi, viroboto na mende, lakini haiudhi wanyama wenye uti wa mgongo.[1]
Picha
haririTanbihi
hariri- ↑ Klotz, J. H.; Moss, J. I.; Zhao, R.; Davis Jr., L. R.; Patterson, R. S. (1994). "Oral toxicity of boric acid and other boron compounds to immature cat fleas (Siphonaptera: Pulicidae)". J. Econ. Entomol. 87 (6): 1534–1536. doi:10.1093/jee/87.6.1534. PMID 7836612.
Viungo vya nje
hariri
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Boroni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |