Kanuni Za Fedha - Ushirikiano Group

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 12

KANUNI ZA FEDHA, 2014

YALIYOMO Ukurasa
1. Kanuni za Fedha …………………………………………………………….2

2. Tafsiri ya maneno ..………………………………………………………….2

3. Akaunti za ushirikiano……………………………………………………....4

4. Mapato ya kikundi…………………………………………...........................4

5. Michango ya wanachama…………………………..…………………….….4

6. Uwasilishaji wa Michango………………………………………………..….5

7. Kuweka kumbukumbu za Michango………………………………….…....5

8. Mapato yatokanayo na Harambee…………………………………………..5

9. Mapato yatokanayo na viingilio……………………………………….…….6

10. Mapato yatokanayo na faini…………………..………………………….….6

11. Madeni yatokanayo na michango……………………………………..…….6

12. Matumizi ya Ushirikiano Fund…………………………………………..….7

13. Vigezo vya mkopo……………………………………………………………7

14. Matumizi ya Uwekezaji Fund..………………………………….…….…….7

15. Utaratibu wa kukopesha kutoka Uwekezaji Fund…………………………7

16. Ulipaji wa Mafao kwa wanachama………………………………..…….…..8

17. Gharama za uendeshaji…………………………………………..………….9

18. Uwekezaji wa Mali za Ushirikiano………………………….……………….9

19. Ukaguzi wa mali za Ushirikiano...……...…………………………..…….….9

20. Kujitoa katika Ushirikiano……………………………….……………..…..10

21. Muda wa kuanza kutumika kanuni hizi……………………………………11

1
SEHEMU YA KWANZA

MASHARTI YA AWALI

1. Kanuni za Fedha
(a) Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Fedha.
(b) Kanuni hizi zimeandaliwa kwa mujibu wa ibara ya 11.7 ya katiba ya
Ushirikiano Group Dar es Salaam na zitasimamiwa na kamati ya Fedha
na Uchumi.
(c) Kanuni hizi zitatumika kwa wanachama wote wa Ushirikiano Group
Dar es Salaam.

2. Tafsiri ya maneno
Katika kanuni hizi, isipokuwa kama itahitajika vinginevyo:-
(a) “Familia” maana yake ni mke na mume/Mke/Mume mwanachama wa umoja.
(b) “Harambee” maana yake ni michango ya ziada kwa ajili ya jambo la dharura.
(c) “Kamati ya Fedha na Uchumi” maana yake ni kamati inayosimamia maswala
ya fedha na uchumi.
(d) “Kamati ya Maadili” maana yake ni kamati inayosimamia utii wa katiba ya
umoja.
(e) “Kanuni za Fedha” maana yake ni mwongozo wa fedha wa Ushirikiano
Group Dar es Salaam.
(f) “Kanuni za maadili” maana yake ni mwongozo unaosimamia mwenendo na
tabia za wanaumoja.
(g) “Kupigika” maana yake ni hali ya kupatwa na majanga ambayo yako inje ya
uwezo wa mwanachama, mfano kuugua kwa muda mrefu, kuuguliwa kwa
muda mrefu, kupata kesi, kuunguliwa nyumba, kupatwa na mafuriko na
majanga mengine yanayofanana na hayo.
(h) “Michango ya ziada” maana yake ni michango ya ziada iliyolipwa na
mwanaushirikiano.
(i) “Mtandao wa mawasiliano” maana yake ni mtandao wa mawasiliano wa e-
mail unaowaunganisha wanaushirikiano.
2
(j) “Mwanaumoja/mwanachama” maana yake ni mtu ambaye ni mwanachama
wa Ushirikiano Group Dar es Salaam kwa mujibu wa katiba ya umoja.
(k) “Sekretarieti” maana yake ni kamati inayojumuisha viongozi wakuu wa
ushirikiano yaani Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina pamoja na
wenyeviti wa kamati nne za kudumu kwa mujibu wa katiba ya umoja.
(l) “Uchapaji na steshenari” maana yake ni gharama za makaratasi na uchapishaji
na kudurufu n.k.
(m) “Umoja” maana yake ni Ushirikiano Group Dar es Salaam.
(n) “Ushirikiano Fund” maana yake ni fedha inayotokana na michango ya
kawaida ya kila mwezi ya wanaushirikiano, harambee, pamoja na viingilio.
(o) “Uwekezaji Fund” maana yake ni fedha zinazotokana na michango ya
uwekezaji ya wanaushirikiano, faini, riba, faida, na misaada au mikopo.
(p) “Watia saini” maana yake ni watu wanaoruhusiwa kusaini malipo ya
Ushirikiano Group Dar es Salaam kwa mujibu wa taratibu za kibenki.

3
SEHEMU YA PILI

USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMOJA

3. Akaunti za Ushirikiano
(a) Kutakuwa na akaunti za Ushirikiano ambazo watia saini watakuwa
Mwenyekiti, Mweka Hazina, Katibu na Mwenyekiti wa kamati ya
Fedha na Uchumi.
(b) Kutakuwa na makundi mawili ya watia saini kama ifuatavyo:
(i) Kundi “A” watakuwa ni Mwenyekiti wa Ushirikiano Group na
Mweka Hazina.
(ii) Kundi “B” watakuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya Fedha na
Uchumi na Katibu .
(c) Malipo kutoka kwenye akaunti za Ushirikiano yatasainiwa na kundi
mojawapo lililotajwa kwenye kifungu cha 3(b).

4. Mapato ya kikundi
(a) Mapato ya kikundi yatatokana na michango ya kila mwezi ya
wanachama, michango ya ziada (contribution in advance),
harambee, faini, riba ya mikopo, faida itokanayo na uwekezaji,
viingilio kwa wanachama wapya, misaada n.k.
(b) Mapato yatokanayo na michango ya uwekezaji, faini, riba, faida, na
misaada au mikopo yatawekwa kwenye “Uwekezaji Fund”.
(c) Mapato yatokanayo na harambee, viingilio, michango ya kawaida ya
kila mwezi na michango ya ziada (contribution in advance)
yatawekwa kwenye “Ushirikiano Fund”.

5. Michango ya wanachama
(a) Wanachama waanzilishi walichangia kiasi cha shilingi 200,000/= kila
mmoja kwa mkupuo kama ada ya kuanzisha kikundi (kiingilio) na
baada ya hapo kila mwanachama analipa ada kiasi cha shilingi
20,000/= kila mwezi.
4
(b) Mwanaushirikiano anaweza kutoa michango yake kwa mwaka mzima
au miezi kadhaa mbele.
(c) Kiwango cha mchango wa kila mwezi kitabadilika kulingana na
wakati na kitapitishwa na Mkutano Mkuu.

6. Uwasilishaji wa Michango
Mwanachama atawasilisha michango kwa njia zifuatazo:-
(a) Atatoa fedha taslimu kwa Mweka Hazina na kupewa stakabadhi.
(b) Atalipa kwenye akaunti ya umoja na kutuma “pay in slip”.
(c) Atatuma kupitia mtandao kama vile M-Pesa, Tigo Pesa n.k na Mweka
Hazina atakiri kama amepokea.

7. Kuweka kumbukumbu za Michango


Mweka Hazina ataweka kumbukumbu za mapato yote na matumizi kwa
mujibu wa kanuni hizi. Wanachama watagawanywa kwenye makundi
kutegemeana na uwasilishaji wa michango yao kama ifuatavyo:
(a) Kundi A- Hawa ni wanachama wanaoudai Ushirikiano, yaani
wametoa michango ya ziada (advance).
(b) Kundi B- Hawa ni wanachama wazuri wanaolipa michango yao
kwa wakati.
(c) Kundi C- Hawa ni wanachama wanaodaiwa hadi miezi miwili.
(d) Kundi D-Hawa ni wanachama wanaodaiwa zaidi ya miezi miwili,
Kamati ya Maadili itapeleka mapendekezo yake kwenye Sekretarieti
ili wajadiliwe na kisha Sekretarieti itawasilisha mapendekezo yake
kwenye mkutano wa kila mwezi wa wanachama wote kwa
maamuzi.

8. Mapato yatokanayo na Harambee


(a) Mwenyekiti kwa kushauriana na Sekretarieti na Kamati ya Fedha na
Uchumi wanaweza kuitisha harambee iwapo kuna jambo la dharura
na iwapo wazo hilo litaungwa mkono na (theluthi moja) 1/3 ya
wanaushirikiano wote.
5
(b) Mapato yatokanayo na harambee yatatumika kukidhi lengo la
harambee hiyo na kama fedha itabaki itawekwa kwenye Ushirikiano
Fund.

9. Mapato yatokanayo na viingilio kwa wanachama wapya


Mwanachama mpya atakayejiunga na Ushirikiano atapaswa kutoa
kiingilio cha shilingi 300,000/= pamoja na michango ya mwanachama
kuanzia mwezi Julai, 2012. Kiwango hiki kitabadilika kulingana na
maamuzi ya mkutano mkuu.

10. Mapato yatokanayo na faini


(a) Mwanachama atatozwa faini kama ataenda kinyume na katiba na
kanuni mbalimbali za umoja.
(b) Mwanaushirikiano anaweza akatozwa faini kwa viwango
vinavyoanishwa kwenye Kanuni za Jamii.
(c) Faini hiyo italipwa kwa Mweka Hazina kama itakavyoamuriwa na
Kamati ya Jamii.

11. Madeni yatokanayo na michango


(a) Mwanachama ambaye hatakuwa ametoa mchango wake wa mwezi
atahesabiwa mdaiwa wa Umoja.
(b) Iwapo atakuwa mdaiwa zaidi ya miezi miwili atapoteza haki ya
kukopa pamoja na haki nyingine kama zilivyofafanuliwa kwenye
Kanuni za Jamii.
(c) Iwapo hatalipa kwa kipindi kinachozidi miezi minne, atalazimika
kujieleza kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi.
(d) Iwapo atajieleza kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi na
kuonekana kuwa hana fedha (amepigika), basi anaweza kuomba
kukopeshwa kutoka kwenye Uwekezaji Fund.

6
12. Matumizi ya Ushirikiano Fund
(a) Kusaidia wanaushirikiano kwa mambo ya kijamii kama
yanavyoainishwa katika Katiba.
(b) Kugharamia uendeshaji wa Umoja.
(c) Kuwakopesha wanaushirikiano baada ya kutuma maombi na
kukubaliwa na Sekretarieti kwa riba ya asilimia 10 kwa mwaka.

13. Vigezo vya mkopo


(a) Vigezo vitakavyotumika kukopesha ni ulipaji mzuri wa michango
ya kila mwezi. Makundi yanayostahili kukopeshwa ni A, B na C.
(b) Kiasi kitakachokopeshwa kitakuwa kinaamuriwa na mkutano mkuu
wa mwaka wa wanachama.
(c) Maombi yanayohusu ada za shule na matibabu yatapewa
kipaumbele.
(d) Ili kupata mkopo, mwanachama lazima adhaminiwe na
mwanachama hai mmoja.
(e) Iwapo mkopaji atashindwa kulipa deni, mdhamini atawajibika
kulipa deni hilo na iwapo naye atashindwa, Kamati ya Fedha na
Uchumi itampeleka mkopaji kwenye Sekretarieti kwa hatua za
kinidhamu.

14. Matumizi ya Uwekezaji Fund


(a) Kugharamia miradi mbali mbali ya maendeleo itakayoanzishwa na Umoja.
(b) Kutumika kama bima kwa mwanachama aliyeshindwa kulipa mchango
wa kila mwezi na kuwasilisha ombi lake la kulipiwa mchango wake wa
mwezi.

15. Utaratibu wa kukopesha kutoka Uwekezaji Fund


(a) Sekretarieti itamjadili mwombaji na kuidhinisha fedha zihamishwe kutoka
Uwekezaji Fund kwenda Ushirikiano Fund.
(b) Mwanachama hatapewa fedha taslimu kutoka uwekezaji Fund, badala
yake deni litahamishwa kutoka Ushirikiano Fund kwenda Uwekezaji Fund
7
na mwanachama ataendelea kuwa hai na kustahili mafao yote kwa mujibu
wa katiba.
(c) Sababu za mwanachama kuomba kutumia uwekezaji fund ni kupigika
kifedha baada ya mume na mke kukosa ajira kwa wakati mmoja, kuugua
muda mrefu, kuuguliwa muda mrefu na matatizo mengine ya kijamii kama
Sekretarieti itakavyoona inafaa.
(d) Mkopo kutoka uwekezaji Fund hautakuwa na riba na mkopaji atalazimika
kurudisha mkopo mapema mara baada ya hali yake kifedha kuimarika.
(e) Mwanachama ambaye hali yake kifedha itaimarika lakini akaendelea
kutorudisha deni hilo, Sekretarieti itapendekeza deni la mwanachama
huyo lihamishiwe Ushirikiano Fund ili mwanachama achukuliwe hatua
kwa mujibu wa kanuni za maadili.

16. Ulipaji wa Mafao kwa wanachama


Umoja utamsaidia mwanachama wake wakati wa shida na raha kama ifuatavyo
hapa chini: -
(a) Utatoa msaada kwa mwanachama pale anapokuwa amefiwa/amefariki.
Wanaostahili kuchangiwa na umoja ni:
Kundi la kwanza
(i) Mwanachama----------------------------------------- shilingi 700,000/=
(ii) Mtoto wa mwanachama------------------------------shilingi 700,000/=
Kundi la pili
(iii) Baba/baba mkwe--------------------------------------shiilingi 600,000/=
(iv) Mama/mama mkwe----------------------------------- shilingi 600,000/=
(v) Mtu mwingine aliyefia nyumbani kwa mwanachama shs. 500,000/=
(b) Kila familia itachangia kwenye msiba unaotokea nyumbani anapoishi
mwanaushirikiano shilingi 50,000/=.
(c) Umoja utatoa msaada kwa mwanachama atakayeunguliwa na nyumba
kiasi cha shilingi 500,000/=.
(d) Kila familia itachangia harusi/Send off ya mwanachama na mtoto wa
mwanachama kwa mujibu wa viwango vilivyokubalika kwenye kamati ya
maandalizi lakini kiwango hicho kisipungue shilingi 100,000/=.
8
(e) Umoja utatoa zawadi au fedha taslimu kama ifuatavyo:-
(i) Harusi/send off ya mtoto wa mwanachama--------- shilingi 400,000/=
(ii) Harusi/send off ya mwanachama------------------- shilingi 500,000/=
(f) Viwango tajwa hapo juu vitabadilika kulingana na muda na vitafanyiwa
marekebisho kadri itakavyoonekana inafaa.
(g) Malipo yanaweza kulipwa kwa hundi, kulipwa kwenye akaunti ya
mhusika, kulipa fedha taslimu kwa mhusika, kulipwa kwa kutumia
mitandao ya simu kama vile M-Pesa, Tigo Pesa n.k.
(h) Malipo yanayofanywa na Ushirikiano yataandaliwa kwa kutumia hati za
malipo.

17. Gharama za uendeshaji


(a) Gharama za uendeshaji kama vile uchapaji na steshenari zitalipwa
kutoka Ushirikiano Fund na zitaidhinishwa na Sekretarieti.
(b) Mweka Hazina ataandaa bajeti ya mwaka mzima ya Ushirikiano na
kuiwasilisha kwenye kamati ya Fedha na Uchumi na baadaye kamati
ya Fedha na Uchumi itaiwasilisha kwenye Sekretarieti na hatimaye
kuwasilishwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka.

18. Uwekezaji wa Mali za Ushirikiano


Kamati ya Fedha na Uchumi, kupitia mpango wa mwaka wa umoja,
itawasilisha mapendekezo ya uwekezeji katika Sekretarieti na hatimaye
kwenye mkutano mkuu wa mwaka ili kuidhinishwa.

19. Ukaguzi wa mali za Umoja


(a) Wanaushirikiano watateua miongoni mwao watu wasiozidi watatu
wenye elimu ya uhasibu na ukaguzi mara moja kwa mwaka au
watakavyoona inafaa, ili wafanye ukaguzi wa mali za Ushirikiano.
(b) Watu watakaoteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 19(a) watakuwa
nje ya wajumbe wa Sekretarieti.

9
(c) Kama wataona inafaa, Mkutano Mkuu wa mwaka utateua mkaguzi
wa nje wa hesabu za umoja na ripoti ya ukaguzi huo itawasilishwa
kwenye mkutano wa kila mwezi wa umoja.
(d) Watu hao watafuata taratibu za kimataifa za ukaguzi ikiwa ni
pamoja na kukaa na viongozi wa umoja na kujadili hoja zao kabla
ya kutoa taarifa ya mwisho.
(e) Wakaguzi wa ndani hawatalipwa fedha yoyote kwa kazi hiyo bali
watafanya kazi ya kujitolea kwa niaba ya wanaushirikiano wenzao.
(f) Iwapo kutaonekana kuna ubadhirifu, wanaushirikiano wanaweza
kufanya maamuzi yafuatayo:-
(i) Kuwataka wabadhirifu warudishe fedha yote
iliyoibiwa/iliyopotea na kuwafungulia mashitaka wezi hao
kwa mujibu wa taratibu za nchi.
(ii) Kuwataka warudishe fedha na kuwafukuza uanachama.
(iii) Kuwawajibisha viongozi waliozembea na kuruhusu
ubadhirifu huo kwa kuwaondoa madarakani.
(g) Iwapo miongoni mwa viongozi kuna mbadhirifu, maamuzi ya
vifungu 19 (f)(i) na 19(f)(ii) yatatumika.

20. Kujitoa katika Ushirikiano


(a) Mwanachama aliyefukuzwa au kujitoa kwenye umoja hatarudishiwa
sehemu yoyote ya kiingilio wala michango yake aliyochangia umoja
tangu kujiunga kwake.
(b) Hata hivyo, mwanaumoja anayepoteza uanachama hatapoteza fedha
alizowekeza katika kampuni shirika.
(c) Ikitokea familia yote, yaani mume na mke wakafariki, wategemezi
wao watalipwa malimbikizo ya michango sambamba na mafao
mengine kwa mujibu wa katiba ya umoja.

10
21. Muda wa kuanza kutumika kanuni hizi
(a) Kanuni hizi zimeanza kutumika mara baada ya kupitishwa na
Mkutano wa wanachama wote kwa mujibu wa Katiba tarehe
25/05/2014.
(b) Kanuni hizi zitakuwa zikifanyiwa marekebisho mara kwa mara
kadiri wanaushirikiano watakavyoona inafaa.

11

You might also like