Raga
Raga (Kiingereza: rugby) ni jina la michezo wa mpira unaochezewa kwa namna mbalimbali na ni aina ya michezo ya timu inayopendwa hasa katika nchi zenye urithi wa utamaduni wa Uingereza kama vile nchi za Jumuiya ya Madola (Australia, Fiji, Samoa, Tonga, Afrika Kusini, Kanada, Kenya, Namibia, Nyuzilandi au Papua Guinea Mpya na mengine) na katika nchi kadhaa ina sifa ya kuwa mchezo wa kitaifa (Fiji, Georgia, Madagaska, Nyuzilandi, Papua Guinea Mpya, Samoa, Tonga, Visiwa vya Cook na Welisi). Nje ya Jumuiya ya Madola mchezo huo ni maarufu Argentina, Brazil, Chile, Georgia, Italia, Japani, Marekani, Romania, Ufaransa, Uhispania, Ureno, Uruguay na Zimbabwe.
Rugby ilianzishwa nchini Uingereza sambamba na mpira wa miguu Wakati wa karne ya 19. Futiboli ya Marekani imezaliwa kutoka kwa rugby ya Kiingereza.
Shabaha ya mchezo ni kubeba au kukanyaga mpira kupitia timu ya wapinzani hadi goli na kuuingiza kwenye goli juu ya mti wa kulala.
Mpira una umbo la duaradufu. Timu mbili ambazo kwa kawaida huwa na wachezaji 15 zinashindana.
Mpira unaweza kushikwa kwa mkono; kuna rukhsa kuupa kwa mchezaji mwingine au kuutupa nyuma. Lakini kuutupa mbele ni kosa ndogo unaofuatwa na tendo la mgandamano ("scrum"). Hapo mpira unawekwa chini na wachezaji 8 wa kila timu wanashikamana na kusukumana hadi mchezaji mmoja anaweza kushika tena mpira.
Kuna rukhsa kumzuia mchezaji na kumwangusha kwa kumshika nyuma ya msari wa mabega. Tendo hili linaitwa kushambulia ("tackle"). Akianguka china anapaswa kuachana na mpira. Wakati mchezaji analala chini wengine hawaruhusiwi kushika mpira kwa mikono.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mgandamano ("scrum")
-
Line-out
-
Mpira wa raga
-
Refa wa raga
-
Goli
-
Kushambulia ("tackle")
-
Timu ya rugby ya Kenya
-
Timu ya rugby ya Cote d'Ivoire
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Henri Garcia (2011). La fabuleuse histoire du rugby. Parys: Éditions de La Martinière. ISBN 978-2-7324-4528-1. (Kifaransa)
- Huw Richards (2007). A Game for Hooligans: The History of Rugby Union. Edinburg: Mainstream Publishing. ISBN 978-1-84596-255-5. (Kiingereza)
- Richard Bath (1997). The Complete Book of Rugby. Seven Oaks. ISBN 1-86200-013-1. (Kiingereza)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- World Rugby (Kiingereza)
- Planet Rugby (Kiingereza)
- ESPNscrum (Kiingereza)
- The Rugby Archive (Kiingereza)
- Rugby Football History (Kiingereza)
- "Rugby". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 2024-11-24. (Kiingereza)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Raga kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |