Powerless (Heroes)
"Powerless" | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Sehemu ya Heroes | |||||||
Peter Petrelli (Milo Ventimiglia) anamzuia Hiro Nakamura (Masi Oka) asimuue Adam Monroe (David Anders), ambaye alisimamisha muda. | |||||||
Sehemu ya. | Msimu 2 Sehemu 11 | ||||||
Imetungwa na | Jeph Loeb | ||||||
Imeongozwa na | Allan Arkush | ||||||
Tayarisho la | 211 | ||||||
Tarehe halisi ya kurushwa | December 3, 2007 | ||||||
Waigizaji wageni | |||||||
| |||||||
| |||||||
Orodha ya sehemu za Heroes |
"Powerless" ni sehemu ya 11 na ya mwisho ya msimu wa pili wa tamthilia ya ubunifu wa kisayansi inayorushwa hewani na TV ya NBC - Heroes na sehemu ya thelathini-na-nne ya jumla ya sehemu zote. Ilitungwa na mtayarishaji-mwenza Jeph Loeb na imeongozwa na mtayarishaji mkuu Allan Arkush. Kipengele hiki kilianza kurushwa hewani kwa mara ya kwanza mnamo tar. 3 Desemba, 2007 ikiwa kama hitimisho la mtiririko wa hadithi "Volume 2: Generations".[1] Pia ilikuwa sehemu ya mwisho ya Heroes ambayo ilikuwa tayari ishakuwa hewani kabla ya mgomo wa waandishi wa Marekani 2007–2008,[2] ikisimama kama sehemu ya mwisho ya msimu inayosibiri kutatuliwa.[3]
Mtitiriko mkuu wa hadithi ya kipengele inahusisha Peter Petrelli (Milo Ventimiglia) na harakati za Hiro Nakamura (Masi Oka) kuzuia kutolewa kwa kirusi cha Shanti, Sylar nae (Zachary Quinto) na jaribio lake la kurudisha vipawa vyake. Mwisho wa kipengele hiki tunapata muhtasari wa matukio yajayo katika toleo la tatu, "Villains", ambalo linahusisha kipande cha Sylar akionenakana kupata nguvu zake upya.
Awali, virusi vilitakiwa viachiwe, na Tim Kring kasema ya kwamba inatakiwa icheze sehemu kubwa katika Toleo la 3. Kring alisema ya kwamba mwisho wa ilibidi uandikwe upya kwa vile walikuwa hawajui lini kipindi hiki kitarudi tena hewani, na walitaka kuhakikisha kwamba wanakaza kila mahali palipolegea. "Powerless" ilitazamwa na Wamarekani milioni kumi na moja na ilipokea tahakiki njema kutoka kwa wataalamu wa utahikiki.
Hadithi
[hariri | hariri chanzo]Peter Petrelli (Milo Ventimiglia) na Adam Monroe (David Anders) wanavunja katika kiwanda cha Primatech huko mjini Odessa ili waweze kuangamiza kirusi cha Shanti, ugonjwa wa kutishia maisha ambao unazuia wanadamu wasiweze kutumia vipawa vyao, hatimaye na kupelekea vifo vyao. Nathan Petrelli (Adrian Pasdar) na Matt Parkman (Greg Grunberg) wanatambua mahali virusi ipo kutoka kwa Angela Petrelli (Cristine Rose).
Peter anatumia nguvu zake kulazimisha kufungua kuba (vault) kwa nguvu, na kujikuta akipambana na Hiro Nakamura (Masi Oka) na Matt. Nathan anatokea na kumshawishi Peter ya kwamba Adam ndiye anayejaribu kuviachia huru hivyo virusi, na si mpango wa kuviangamiza. Adam, tayarisha keshavitia mkononi virusi, kaviachia vianguke kabla hata Hiro hajaondoka nae.
Peter anaingia katika kuba kwa muda mwafaka na kudaka kirusi kwa kwa kutumia uwezo wa mawazo yake na kisha kuangamiza virusi hivyo kwa kutumia nyuklia ya mikono yake. Hiro kamtia Adam mahali ambapo "hatoweza kujeruhi mtu yeyote tena", ndani ya jeneza katika eneo la makaburi ya Japani.
Baada ya Monica Dawson (Dana Davis) kukamatwa na wahuni wa mtaani, Micah Sanders (Noah Gray-Cabey) anaelekea kwa mama'ke Niki (Ali Larter) kuomba msaada. Licha ya ukweli wa kwamba Niki hana tena nguvu zake kwa kutokana na virusi, anakubalia kusaidia. Wanafuata alama za GPS zinatokana na simu ya mkononi ya Monica na kumkuta katika jumba moja lililotelekezwa.
Kafungwa mikono na jengo hilo linaungua pembeni mwake. Anatumia kile kilichobakia katika nguvu zake, Niki anafanikiwa kumsaidia Monica kutoroka, lakini nguvu zake zinaisha na hatimaye anashindwa kujisaidia huku jengo likilipuka.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Elliott, Sean (2007-12-04). "Review: Heroes – Season Two – 'Powerless'". If. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-08. Iliwekwa mnamo 2008-05-30.
{{cite web}}
: Italic or bold markup not allowed in:|publisher=
(help) - ↑ Strachan, Alex (2007-12-07). "Casualties of the Hollywood writers strike". The Gazette. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-11-10. Iliwekwa mnamo 2007-11-07.
{{cite web}}
: Italic or bold markup not allowed in:|publisher=
(help) - ↑ Jensen, Jeff (2007-11-07). "Heroes Creator Apologizes to Fans". Entertainment Weekly. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-11-09. Iliwekwa mnamo 2007-11-07.
{{cite web}}
: Italic or bold markup not allowed in:|publisher=
(help)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Powerless (Heroes) katika Internet Movie Database
- Beaming Beeman - Season 2, Episode 11 - Director's blog on the filming of this episode.