Nenda kwa yaliyomo

Dalmatia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dalmatia (buluu-nyeusi) katika nchi ya Kroatia - (buluu yote)

Dalmatia (kwa Kikroatia: Dalmacija; kwa Kiitalia: Dalmazia) ni jina la eneo la pwani ya Bahari ya Adria kusini mwa Kroatia.

Inaanza kwenye kisiwa cha Rab upande wa kaskazini na kuendelea hadi mpaka wa Montenegro upande wa kusini. Upande wa bara mwisho wake ni mpaka wa Bosnia na Herzegovina.

Wakazi wengi huishi pwani lakini sehemu za bara kuna watu wachache.

Uchumi unategemea hasa utalii: watalii kutoka pande nyingi za Ulaya wanakuja hapa kwa burudani kando ya bahari katika miezi pasipo baridi. Kati ya watalii milioni 10 - 11 wanaofika Kroatia kila mwaka idadi kubwa kabisa inalenga pwani ya Dalmatia. [1]

Kihistoria hili lilikuwa eneo la miji-dola kwenye pwani iliyostawi kutokana na biashara ya baharini. Kati ya miji hiyo kuna Split, Zadar, Šibenik na Dubrovnik.

Kwa karne 3 kati ya mwaka 1400 hadi 1797 pwani ya Dalmatia ilikuwa chini ya utawala wa jamhuri ya Venezia. Hii inaeleza hali ya kwamba miji mingi ya pwani inafanana na miji ya Italia kutokana na namna ya ujenzi ya nyumba na makanisa na mpangilio wa miji.

Tangu 1797 hadi 1918 Dalmatia ilikuwa jimbo la Milki ya Austria, baadaye Austria-Hungaria.

Baada ya 1918 imekuwa sehemu ya Kroatia ndani ya Yugoslavia hadi kuporomoka kwa Yugoslavia mwaka 1991.

Jina la "Dalmatia" limetokana na zamani za Roma ya Kale na hasa kabila la "Dalmatae" waliopigana na Waroma wa Kale.

Lakini leo hii wakazi walio wengi ni Wakroatia, ambao ni jamii ya Waslavi.

  1. Takwimu kuhusu idadi ya watalii nchini Kroatia http://reports.aiidatapro.com/CBE/Tourism_2009.pdf Archived 7 Julai 2011 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Dalmatia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.