Ukuta
Kwa makala juu ya taasisi ya UKUTA, nenda UKUTA.
Ukuta ni muundo wima unaopakanisha nafasi kuwa tofauti, kama maeneo ya ndani na nje au vyumba ndani ya jengo.
Ukuta nje ya jengo
haririNje ya jengo ukuta hujengwa kwa kuonyesha mipaka ya eneo na kuzuia watu au wanyama kuingia ndani. Vivyo hivyo unaweza kulenga kuwazuia wasitoke. Katika matumizi haya ukuta unafanana na madhumuni ya fensi lakini ni imara zaidi.
Uwanja wa nyumba mara nyingi huzungushwa kwa ukuta kwa kuongeza usalama. Ukuta wa Berlin ulijengwa katikati ya jiji la Berlin wakati wa ugawaji wa Ujerumani ili wakazi wa sehemu chini ya utawala wa kidikteta upande wa mashariki wasikimbilie upande wa magharibi.
Katika mazingira ya ugomvi ukuta hujengwa pia kwa kuzuia mashambulio na kwa kusudi la kusaidia utetezi. Katika historia kuna mifano kadhaa ya kuta kubwa kama Ukuta wa China au kuta za mpakani wa Uajemi na Dola la Roma. Mara nyingi kwa kusudi hili miji ilizingirwa kwa ukuta (ngome).
Ukuta una matumizi tofauti tena kwa kuzuia banguko na miporomoko ya ardhi.
Ukuta ndani ya jengo
haririUkuta ndani ya jengo huwa na madhumuni mawili:
Aina za maunzi ya kujenga kuta
haririKuna aina nyingi za maunzi yanayotumiwa kujenga kuta:
- Ukuta wa zege
- Ukuta wa udongo
- Ukuta wa matofali
- Ukuta wa mawe
- Ukuta wa kioo
- Ukuta wa miti/mbao
- Ukuta wa chuma n.k.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ukuta kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |